UTEUZI
wa Mawaziri wapya kwenye Baraza la Mawaziri baada ya Rais Jakaya
Kikwete kutengua uteuzi wa Mawaziri wanne Desemba 20, 2013 na mmoja
kufariki dunia, umeanza kuibua maswali mengi miongoni mwa viongozi,
wananchi.
Rais Kikwete alitengua uteuzi wa
Mawaziri hao kutokana na shinikizo la wabunge baada ya kuipitia Ripoti
ya Kamati ya Bunge iliyoundwa kuchunguza athari zilizotokana na
utekelezwaji wa "Operesheni Tokomeza Ujangili".
Mawaziri ambao uteuzi wao
ulitenguliwa ni aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dkt.
Emmanuel Nchimbi, Mifugo na Uvuvi, Dkt. David Mathayo, Ulinzi na Jeshi
la Kujenga Taifa, Bw. Shamsi Vuai Nahodha pamoja na Waziri wa Maliasili
na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki.
Nafasi nyingine ambayo iko wazi ni
ile ya Waziri wa Fedha, ambayo aliyekuwa Waziri wake, Dkt. William
Mgimwa, alifariki dunia Januari mosi mwaka huu.
Macho na masikio ya Watanzania yapo
kwa Rais Kikwete wakiamini kiongozi huyo, ana kazi ngumu ya kufanya
uteuzi makini ambao utarudisha heshima ya Serikali hasa kwa wananchi
walioathirika na operesheni hiyo.
Wakizungumza na Majira ili kutoa
maoni yao kwa sharti la kutotajwa majina yao gazetini, baadhi ya
mawaziri ambao hawakuguswa na rungu hilo, walisema kuchelewa kwa Rais
Kikwete kufanya uteuzi huo ni dalili nzuri ya kuteua mawaziri wenye sifa
na uwezo wa kumsaidia katika wizara husika.
Alisema suala la uteuzi wa nafasi
nyeti za uwaziri, si kazi ndogo ndio maana amekaa kimya muda mrefu ili
kuangalia nani anayeweza kutekeleza majukumu atakayompa ili kuleta
matokeo mazuri kwa wananchi, Taifa kwa ujumla.
Waliongeza kuwa, kazi kubwa ipo
kwenye uteuzi wa Waziri wa Fedha ambaye uwezo wake utafanana na ule wa
marehemu Dkt. Mgimwa kwani kifo chake ni pigo kubwa kwa Serikali
iliyotambua uwezo wake na kumpa dhamana.
"Dkt. Mgimwa alikuwa na uwezo mkubwa
katika masuala ya fedha, aliweza kufanya mambo mengi ambayo kimsingi
yameiletea sifa kubwa Serikali yetu ndani na nje ya nchi.
"Imani yangu ni kwamba, Rais Kikwete
ana washauri wazuri ambao watafanya kazi nzuri ambayo itakubalika na
wananchi wote... tusubiri uteuzi wake," alisema mmoja wa Mawaziri wakati
akitoa maoni yake.
Kwa upande wao, baadhi ya wa n a n c
h i wa l i o z u n g umz a na Majira, wamemshauri Rais Kikwete
asikilize kilio cha wabunge ambao walishauri kuwajibishwa kwa mawaziri
wengine ambao uwajibikaji wao si mzuri katika.
Serikali yake.
Walisema
mbali na mawaziri ambao ametengua uteuzi wao, wapo watendaji katika
wizara hizo ambao nao wanapaswa kuwajibishwa kwa kuondolewa katika
nafasi hizo kwani kama wataendelea kuwepo, bado wataendelea kuwa kikwazo
kwa mawaziri wapya watakaoteuliwa.
"Mimi naamini CCM bado ina watendaji
wazuri ambao wanaweza kupewa nafasi za uongozi na wakafanya kazi
waliyopewa kwa ufanisi mkubwa.
"Ni fursa nzuri kwa Rais Kikwete na
wasaidizi wake, kukaa chini na kuteua viongozi ambao uteuzi wao
utapokewa vizuri na wananchi... kati ya mawaziri ambao alitengua uteuzi
wao, wapo ambao anaweza kuwarudisha ila si wote kwani ajali iliyowakuta,
imechangiwa na wasaidizi wao," alisema Bw. Suleiman Sadif ambaye
kitaaluma na mchumi.
Akizungumzia suala la mawaziri ambao
Kamati Kuu ya CCM iliwaita na kuwahoji, mjini Dodoma, Bw. Sadif alisema
dhamira ya chama hicho si kutaka wafukuzwe kazi bali lengo ni
kuwakumbusha viongozi hao watekeleze wajibu wao.
Alimpongeza Rais Kikwete, kwa
kuchukua uamuzi mgumu wa kutengua uteuzi wa Mawaziri wake kwani hiyo
ndiyo demokrasia na uamuzi huo umeepusha malalamiko ambayo yangeweza
kutolewa kwa Serikali kwani matokeo ya Operesheni Ujangili hayakuwa
mazuri kwa Taifa.
Uchunguzi uliofanywa na Majira
umebaini kuwa, wananchi wengi wana hamu kubwa ya kuona Rais Kikwete
akiteua Mawaziri vijana ambao utendajikazi wao umeonekana katika majimbo
yao, Kamati za Bunge na kwenye mijadala mbalimbali yenye masilahi kwa
Taifa.
MAJIRA.
Home
»
»Unlabelled
» UTEUZI WA MAWAZIRI WAPYA NI MTIHANI KWA RAIS KIKWETE KURUDISHA HESHIMA YA SERIKALI
Tuesday, January 14, 2014
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment