Pages

Pages

Tuesday, April 22, 2014

Chadema wamshukuru Rais Kikwete




Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wilayani Karatu kimeeleza kufurahishwa kwake na mchango unaotolewa na Rais Jakaya Kikwete katika kuchochea maendeleo bila upendeleo.
Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, ilisema kuwa pongezi hizo zilitolewa jana mchana na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu, Lazaro Titus Massey wakati wa sherehe za uzinduzi wa jengo la Halmashauri hiyo mjini Karatu. Halmashauri ya Wilaya ya Karatu inaongozwa na Chadema.
“Ni lazima tutoe shukurani kwako kwa sababu bila wewe kuwa Rais wa Tanzania, sisi Karatu tusingepata jengo hili. Pamoja na kwamba Halmashauri yetu ni Chadema bado umeamua kuchangia maendeleo ya wilaya yetu kwa kuchangia kiasi kikubwa ujenzi wa jengo hili. Sisi hata robo ya fedha za ujenzi huu hatukuweza kuzitoa,” alisema Massey huku akishangiliwa na wananchi.
Jengo la Halmashauri ya Wilaya ya Karatu limegharimu Sh1.412 bilioni na kati ya hizo, Serikali imetoa Sh1.394 bilioni na halmashauri imechangia Sh18 milioni.
Rais Kikwete alisema sera ya Serikali yake ni kusambaza maendeleo kwa Watanzania wote bila kujali misimamo yao ya kisiasa wala kuongozwa na hisia nyingine mbali na ukweli kuwa kila mtu anataka maendeleo.

No comments:

Post a Comment