KINDA wa muziki wa kizazi kipya nchini, Abdulaziz Abubakari ‘Dogo
Janja’, amesema kwa sasa atakuwa anafanya kazi zake za muziki jijini
Arusha kutokana na mashabiki wengi wa Dar es Salaam kutomthamini.
Dogo Janja, alisema jana kuwa kuanzia sasa akitaka kufanya kazi zake
atasafiri kwenda Arusha maana amegundua kama ndiko anakokubalika zaidi
kuliko mikoa mingine.
“Sio kwamba sitafanya kazi kabisa Dar es Salaam, nitafanya, lakini
asilimia nyingi nitazifanyia nyumbani maana kule nathaminiwa sana,
huku dharau nyingi na watu tunachukuliana poa tu, lakini mimi nataka
kufanya kazi zangu nyumbani na sio Dar es Salaam tena.
“Unajua mwenye asili haachi asili na akiacha asili hana akili,
nyumbani nakubalika sana hivyo sina budi kwenda kuwafurahisha mashabiki
pamoja na familia yangu,” alisema msanii huyo mwenyeji wa Arusha.
Dogo Janja ni kati ya wasanii ambao wanatamba kupitia kazi zao
kutokana na uwezo walionao pamoja na kukubalika katika jamii
inayowazunguka
No comments:
Post a Comment