Pages

Pages

Wednesday, June 18, 2014

polisi wawashikilia watu 30 kwa vurugu na uharibifu wa mali

Jeshi la Polisi mkoani Kagera linawashikilia watu 30 wakazi wa Wilaya ya Muleba kwa tuhuma za vurugu na uharibifu wa mali uliotokea wilayani humo, ikiwemo kuvunja chumba cha kuhifadhia maiti katika Kituo cha Afya Kaigara na kuchoma nyumba moto.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, George Mayunga, aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa chanzo cha uharibifu huo ni kifo cha Asera Triphone (16) kilichotokea Juni 12, mwaka huu katika Hospitali ya Mount Meru mkoani Arusha.
Alisema kuwa baada ya kufariki kwa mtoto huyo, mwajiri wake, Valentina Maxmilian, alichukua jukumu la kusafirisha mwili wa marehemu kwenda kwa wazazi wake wilayani Muleba kwa ajili ya mazishi.
Alisema wakati mwili unafikishwa nyumbani kwa baba wa marehemu, Triphone Joseph, alikuwa na taarifa kuwa mwanae ameuawa kwa mateso, ikiwa ni pamoja na kuondolewa baadhi ya viungo vyake vya mwili, zikiwemo sehemu za siri.
Alisema wazazi hao walitoa taarifa kituo cha polisi wakiomba mwili wa marehemu upelekwe kituo cha afya cha Kaigara kwa ajili ya uchunguzi wa kidaktari ombi lililopingwa na polisi ambao walitaka mwili huo ukafanyiwe uchunguzi katika Hospitali ya Mkoa wa Kagera.
Alisema kutokana na msimamo wa polisi, kundi la wananchi lilihamasishwa na kuamua kubeba jeneza la marehemu kutoka Kijiji cha Bukono na kulipeleka Muleba kisha kulitelekeza barabarani, lakini mwili huo ulichukuliwa ukahifadhiwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti cha kituo cha Kaigara ili kusubiri utaratibu wa kufanya uchunguzi.
Kwa mujibu wa kamanda, wazazi wa mtoto bado walikuwa wakishinikiza uchunguzi wa kidaktari ufanyike kubaini chanzo cha kifo cha binti yao.
Alisema kabla ya utafiti huo kufanyika, wananchi wakaamua kuvunja mlango wa chumba cha kuhifadhia maiti cha kituo hicho ambapo polisi waliingilia kati na kutumia nguvu kuwadhibiti.
Alisema wazazi wa marehemu walikubali kuchukua mwili wa mtoto wao kwa ajili ya taratibu za mazishi huko kijijini kwao Bukono na kuwa tayari wameshazika.
Aliongeza kuwa ilipofika usiku saa mbili, uhamasishaji uliendelea, likatoka kundi la watu na kwenda nyumbani kwa Veronica Maxmilian, mama wa mwajiri wa marehemu katika Kijiji cha Buyango, na kuchoma moto nyumba mbili.
Alisema hatua za kisheria zimechukuliwa kwa kuwakamata waliohusika na uvunjaji wa kituo cha afya, kutelekeza maiti barabarani na uchomaji wa nyumba mbili za familia ya mwajiri wa msichana huyo.
Alisema watu 30 wanashikiliwa kwa lengo la kuwahoji ili kuwabaini vinara wa vurugu hizo na kuwa ukamataji huo ulifanyika baada ya kupata taarifa mbalimbali zilizolifikia jeshi hilo.
Hata hivyo, alisema mwajiri wa marehemu anashikiliwa na jeshi hilo kwa ajili ya upelelezi wa kina ambao utafanyika hapa Kagera na mkoani Arusha pamoja na jirani wanaomzunguka.

MASTER PLAN YA ARUSHA KUBUNIWA NA WATAALAM KUTOKA SINGAPORE

Mpango kabambe waja Mwanza, ArushaSERIKALI imeipa kazi ya kuandaa mpango kabambe (Master Plan) wa mipango miji kampuni ya kimataifa ya Surbana International Pty Ltd ya nchini Singapore kwa ajili ya majiji ya Arusha na Mwanza.
Kampuni hiyo inatakiwa kukamilisha shughuli hiyo ndani ya miezi 13 tangu kusainiwa kwa mkataba huo.
Mkataba huo ulisainiwa wiki iliyopita jijini hapa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Alphayo Kidata na Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo, Kong Wu Mun.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo na Waziri wa Nchi wa Mambo ya Nje na Mambo ya Ndani wa Singapore, Masagos Zulkiflg walikuwepo kushuhudia tukio hilo la utiaji saini.
Akizungumza mara baada ya kusaini mkataba huo, Kidata alisema tukio hilo ni mwendelezo wa mchakato uliokuwa umeanza kufuatia mkataba wa makubaliano ambao Wizara ya Ardhi ilisainiana na Singapore Desemba 2013 kwa niaba ya Tanzania.
Alisema lengo la kuanzisha mradi huo ni kuwezesha miji iliyopangiliwa vizuri na yenye maendeleo na kuondokana na msongamano wa magari pamoja na nyumba zisizokuwa na mpangilio jijini Arusha.
“Kuwepo kwa mpango huu kutawezesha kwa kiasi kikubwa sana kuishi katika mpangilio unaohitajika na kuchangia nchi kupata maendeleo kwa kuwa na miundombinu ya kutosha katika maeneo yenye mpangilio,” alisema Kidata.
Alisema kuwa wanatarajia kusaini mkataba na kampuni ya China kwa ajili ya kuandaa mpango kabambe kwa ajili ya mikoa ya Lindi na Mtwara ambayo inatazamiwa kukua kwa kasi kubwa kutokana na kugunduliwa kwa nishati ya gesi.
Zulkiflg alisema kuwa nchi yake imejikita katika kusaidia mataifa yanayoendelea, hasa kwa kuwasaidia kuandaa uwepo wa mipango miji jambo alilodai kuwa litaharakisha maendeleo kwa kuhamasisha uwekezaji toka mataifa mbalimbali

MASTER PLAN YA ARUSHA KUBUNIWA NA WATAALAM KUTOKA SINGAPORE

Mpango kabambe waja Mwanza, ArushaSERIKALI imeipa kazi ya kuandaa mpango kabambe (Master Plan) wa mipango miji kampuni ya kimataifa ya Surbana International Pty Ltd ya nchini Singapore kwa ajili ya majiji ya Arusha na Mwanza.
Kampuni hiyo inatakiwa kukamilisha shughuli hiyo ndani ya miezi 13 tangu kusainiwa kwa mkataba huo.
Mkataba huo ulisainiwa wiki iliyopita jijini hapa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Alphayo Kidata na Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo, Kong Wu Mun.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo na Waziri wa Nchi wa Mambo ya Nje na Mambo ya Ndani wa Singapore, Masagos Zulkiflg walikuwepo kushuhudia tukio hilo la utiaji saini.
Akizungumza mara baada ya kusaini mkataba huo, Kidata alisema tukio hilo ni mwendelezo wa mchakato uliokuwa umeanza kufuatia mkataba wa makubaliano ambao Wizara ya Ardhi ilisainiana na Singapore Desemba 2013 kwa niaba ya Tanzania.
Alisema lengo la kuanzisha mradi huo ni kuwezesha miji iliyopangiliwa vizuri na yenye maendeleo na kuondokana na msongamano wa magari pamoja na nyumba zisizokuwa na mpangilio jijini Arusha.
“Kuwepo kwa mpango huu kutawezesha kwa kiasi kikubwa sana kuishi katika mpangilio unaohitajika na kuchangia nchi kupata maendeleo kwa kuwa na miundombinu ya kutosha katika maeneo yenye mpangilio,” alisema Kidata.
Alisema kuwa wanatarajia kusaini mkataba na kampuni ya China kwa ajili ya kuandaa mpango kabambe kwa ajili ya mikoa ya Lindi na Mtwara ambayo inatazamiwa kukua kwa kasi kubwa kutokana na kugunduliwa kwa nishati ya gesi.
Zulkiflg alisema kuwa nchi yake imejikita katika kusaidia mataifa yanayoendelea, hasa kwa kuwasaidia kuandaa uwepo wa mipango miji jambo alilodai kuwa litaharakisha maendeleo kwa kuhamasisha uwekezaji toka mataifa mbalimbali

Monday, June 16, 2014

Monday, June 9, 2014

abunge wa Tanzania katika bunge la jumuiya ya Afrika mashariki wapinga hoja za kumuondoa spika wa bunge hilo

WABUNGE wa Tanzania katika Bunge la jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA), wamesisitiza kutounga mkono hoja ya kumng’oa Spika wa bunge hilo, Margaret Zziwa, kwa kuwa haina maslahi na Tanzania na wana Afrika Mashariki kwa ujumla.

Hayo yameelezwa jana na wabunge watatu miongoni mwa wabunge hao wakiongozwa na Mwenyekiti wa Wabunge wa EALA Tanzania, Adam Kimbisa ambapo alisema baada ya kuchunguza kwa umakini walibaini kuwa katika jaribio hilo la kumng’oa spika kuna ajenda ya siri.

Alisema kuwa hoja hiyo haina maslahi ya Tanzania na iko kinyume na malengo ya ushirikiano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, pia wamebaini kuwa hoja yenyewe ni sehemu ya mchezo mchafu wa ajenda ya siri ya kujaribu kuweka mbele maslahi ya baadhi ya wanachama wachache ndani ya jumuiya hiyo badala ya kuzingatia maslahi mapana ya jumuiya hiyo.

“Tuhuma zilizotajwa dhidi ya Spika wa EALA kuhusu yeye kuonesha upendeleaji, ujeuri na mapungufu mengine ya uongozi zimegundulika kuwa hazina mashiko wala mantiki,” alisema Kimbisa.

Aidha, alisema kitendo kilichowashtua ni kumekuwa na majaribio ya baadhi ya wabunge wa EALA kutoka nje ya Tanzania na viongozi wa sekretarieti ya jumuiya hiyo kutaka kulazimisha sahihi za baadhi ya wabunge wa Tanzania kutumika kinyume na utaratibu kuunga mkono azimio hilo, jambo linalodhihirisha kuwepo kwa ajenda ya siri katika sakata hilo dhidi ya maslahi ya Tanzania na jumuiya kwa ujumla.

Alisema wabunge watatu wa EALA kutoka Tanzania ambao awali waliunga mkono hoja hiyo kwa sahihi zao, baadae waliamua kuipinga kwa kutoa sahihi zao kwa hiari yao wenyewe baada ya kuchunguza kwa umakini zaidi na kugundua mchezo huo, ambapo walimwandikia barua Katibu wa Bunge wa EALA kumweleza uamuzi wao.

“Hoja yenyewe kisheria ni batili kwa kuwa haikuwasilishwa bungeni ndani ya siku saba tangu ilipopelekwa kwa Katibu wa Bunge na pia imekosa sahihi za kuungwa mkono na wabunge wanne kutoka kila nchi mwanachama wa jumuiya kama kanuni zinavyotamka.

“Tunaomba uongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa ngazi zote, ikiwemo sekretarieti ya jumuiya kuheshimu maamuzi ya wabunge wa EALA kutoka Tanzania,” alisema.

Alisema awali wabunge watano wa bunge hilo wa Tanzania kati ya tisa walionesha kuunga mkono hoja hiyo lakini baada ya kubaini kuwepo kwa mchezo mchafui na ajenda ya siri wabunge watatu waliondoa sahihi zao na kufanya idadi ya wabunge kutoka Tanzania kupinga hoja hiyo kufikia saba kati ya tisa.

Alisema wabunge hao wameshapoteza muda mwingi, fedha na rasilimali nyingine katika kujadili hoja hiyo isiyo na tija.

Alisema sasa wanahitaji kuweka jitihada zao katika kazi myuhimu ya kutetea maslahi ya wananchi wa Afrika Mashariki.

Naye Katibu wa Wabunge wa EALA wa Tanzania, Shy-Rose Bhanji alisema, awali alikuwa mstari wa mbele kuunga mkono hoja hiyo lakini alikuja kubaini kuwa kuna vikao vya siri vinaendelea juu ya sakata hilo, jambo lililofanya aamuue kupinga hoja hiyo.

“Ni kweli nilikuwa mstari wa mbele kutaka aondolewe lakini baada ya kutafakari na kuchunguza kwa makini chanzo halisi niligundua kuwa hoja hii haina maslahi kwa Watanzania na sisi ni wazalendo tuko kwa ajili ya kuiwakilisha Tanzania,” alusema.

Alisema kuwa Spika huyo ni binadamu hivyo hawezi akakosa mapungufu hivyo baadhi ya wabunge wanataka kutumia udhaifu huo kumngo’oa katika nafasi hiyo.

BAJETI YAMKIMBIZA RAIS KIKWETE DODOMA

Rais Jakaya Kikwete anatarajiwa kuwasili Dodoma keshokutwa, ikiwa ni siku moja kabla ya kuwasilishwa kwa Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2014/15.

Habari zilizopatikana jana zinasema Rais ataongoza kikao cha Baraza la Mawaziri kitakachopewa muhtasari kuhusu Bajeti ya Serikali ya mwaka ujao wa fedha na baadaye atafuatilia uwasilishaji wa bajeti hiyo bungeni akiwa Dodoma.

Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Salva Rweyemamu alisema asingeweza kuzungumzia suala hilo kwa kuwa yuko likizo lakini akaweka bayana kwamba kwa kawaida kabla ya bajeti kuwasilishwa bungeni, lazima Baraza la Mawaziri lipewe muhtasari wa bajeti husika.

“Ni kawaida kabla ya bajeti kuwasilishwa, Rais huongoza kikao cha Baraza la Mawaziri yaani pre budget cabinet meeting ambako Waziri wa Fedha hutoa briefing (muhtasari) kuhusu maeneo muhimu ya bajeti, kwa hiyo siyo jambo jipya ni suala la kawaida,” alisema Rweyemamu.

Itakumbukwa kuwa mwaka jana kabla ya kusomwa kwa bajeti ya 2013/14, Rais Kikwete alikuwa Dodoma ambako pamoja na kukutana na mawaziri, pia alifanya kikao na Kamati ya Bunge ya Bajeti.

Hata hivyo, uwepo wake mjini Dodoma safari hii umekuja wakati kukiwa na dalili za mvutano mkubwa kati ya Bunge na Serikali kutokana na kutotolewa kwa fedha za kutosha za maendeleo kwa mwaka wa fedha unaoisha Juni 30 mwaka huu.

Taarifa zinasema bajeti inayomalizika mwishoni mwa mwaka huu, inapungukiwa kiasi cha Sh1.8 trilioni, huku Serikali ikilaumiwa na wabunge kwa kutoa misamaha ya kodi inayofikia Sh1.52 trilioni, ambayo ingepunguza nakisi iliyopo kwenye bajeti kwa asilimia 84.4.

Wakati wa mjadala wa bajeti za wizara tangu kuanza kwa Bunge la Bajeti Mei 6 mwaka huu, wabunge wamesikika mara kadhaa wakilalamika kwamba fedha za maendeleo zilizotolewa kwa wizara katika bajeti ya 2013/14 ni kati ya asilimia 25 na 30, jambo ambalo limesababisha kukwama kwa miradi mingi.

Keshokutwa itakuwa siku ya mwisho ya mashauriano baina ya Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Bunge kupitia Kamati yake ya Bajeti inayoongozwa na Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge.

Mazungumzo hayo yaliyoanza Juni 5 mwaka huu, yalilenga kuangalia uwezekano wa kutafuta vyanzo vipya vya mapato ili kuwezesha kuzingatiwa kwa ushauri wa wabunge, pamoja na kusaka fedha kuziba pengo la Sh1.8 trilioni katika bajeti ya 2013/14.

Alipoulizwa jana, Chenge hakuwa tayari kuzungumzia hatua iliyofikiwa katika mashauriano hayo na badala yake alisema kwa ufupi: “Ndugu yangu mambo ya Bunge, tutakutana kwenye taarifa yetu ya kamati tutakayoiwasilisha bungeni.”

Mbunge waArumeru Mashariki Joshua Nassary Kufanya kweli kuukimbia Ukapera

Hatimae mbunge wa Arumeru mashariki mh. Joshua Nassari na Bi. Anande Nnko wafunga pingu za maisha na kuwa mwili mmoja katika kanisa la Kilinga na baada ya hapo kuelekea katika viwanja vya Usa- River Academy ambako ndiko sherehe ilipofanyika.
Siku ya Jumamosi tarehe 7 Juni 2014 itakumbukwa na wawili hawa kama siku yao ya kumbu kumbu ya ndoa yao, pamoja na wageni wengi waliojitokeza, viongozi wa kiserikali pamoja na wale wa kisiasa, taasisi na dini walikuwepo kwa wingi. Tunawatakia ndoa njema na Mungu awalinde.

Sunday, June 8, 2014

LILIAN DEUS KUTWAA TAJI LA REDD'S MISS ARUSHA

   
Lilian Deus aliyetwaa taji la Redd's Miss Arusha (Aliyekaa) na kulia ni mshindi wa pili Evaline Baasa ambae ndiye anayeshikilia taji la miss Karatu na kushoto ni mshindi wa tatu Rahisa Mboya

Saturday, June 7, 2014

jeshi lapolisi lafichua maficho ya biashara wa watoto wa kigeni kingono

Na Mwandishi wetu Dina Chahali. Idara ya Uhamiaji nchini Tanzania imegundua maficho ya wasichana waliosafirishwa kutoka nchi za India na Nepal mjini Dar es Salaam ambao wanatumikishwa katika biashara zisizo halali katika maeneo mbalimbali jijini humo.
Katika siku tano zilizopita, idara ya uhamiaji jijini Dar es salaam inasema imewaokoa wasichana 51 raia wa India na Nepal waliohifadhiwa katika nyumba kadhaa na kutumikishwa katika biashara ya ngono na nyinginezo na kuwakamata wafanyabiashara wenye asili ya kiasia wanaotuhumiwa kusafirisha wasichana hao na kuwatumikisha hapa nchini
Mwishoni mwa mwezi uliopita wasichana wengine 17 walikutwa wamehifadhiwa katika nyumba moja eneo la Msasani jijini Dar es salaam kwa zaidi ya miezi mitatu huku wakidaiwa kutumika kwenye biashara ya ngono huku wengine 34 wakikamatwa jana  eneo la Mwananyamala jijini humo.

Wafanyabiashara waliotiwa nguvuni wanadai kuwa waliwaleta nchini humo wasichana hao kushiriki kucheza ngoma za asili kutoka mataifa yao katika club mbali mbali za usiku maarufu-Mujra na walikuwa wamehifadhiwa katika jengo moja huku pasi zao za kusafiria zikiwa zimechukuliwa na aliyetambuliwa kama meneja wao

Afisa Uhamiaji Mkaguzi wa mipaka  Doto Selasini amesema wasichana hao wenye umri wa chini ya miaka 26 waliingizwa nchini kwa njia halali kwa ahadi ya meneja wao kukaa nchini kwa siku 14 kwa ajili ya kushiriki ngoma za utamaduni wa mataifa yao, lakini wamekuwa wakitafutiwa wateja na baadae kulazimishwa kufanya vitendo vya ngono na kwamba wamefanikiwa kupata taarifa zao kupitia raia wema

Meneja wa wasichana hao Savio Menes ambaye naye ametiwa mbaroni na maafisa wa uhamiaji amesema wasichana hao aliwaingiza nchini kupitia wakala aliyeko nchini India na kudai kuwa walikuja kushiriki ngoma za utamaduni za bara la Asia

Hata hivyo wasichana wenyewe walipohojiwa na maafisa wa uhamiaji walikiri kuishi katika mazingira magumu na kufanya biashara isiyo halali na kwamba wako tayari kurejeshwa makwao India na Nepal. Wamedai kuwa wamekuwa chini ya ulinzi mkali huku wakitolewa usiku na kupelekwa katika mahoteli na kurejeshwa alfajiri na hawakuruhusiwa kuwa na mawasiliano na mtu yeyote.

Taarifa zilizopatikana  baadaye zilieleza kwamba wasichana 17 waliokamatwa Mei 30 wamesafirishwa na kurejeshwa makwao India na Nepal huku wafanyabiashara waliowaleta wakisubiri taratibu za kufunguliwa mashtaka.

Friday, June 6, 2014

Komba alia na picha chafu zilizosambaa mtandaoni


Baada ya kusambaa kwa picha ambazo si nzuri katika mazingira ya kawaida zikimuonyesha Mhe. Kaptein Komba akiwa amepiga picha na msichana chumban huku zikimuonyesha msichana huyo amevaa kanga na wakati mwingine bila kuwa na nguo.
Kuzungumzia tukio hilo moja kwa moja kutoka Dodoma Mhe. Komba anasema hajui kuhusiana na picha hizo kwani hajawahi kabisa kuwa katika mazingira hayo na binti huyo bali hao ni mtu ambaye amezitengeneza na hajui kwanini amefanya hivyo.

Mhe. Komba anasema “Picha nimewahi kupiga nyingi tangu utotoni lakini hizi za leo hata mimi zinaniogopesha, siwezi kuwa mwaguzi kujua nani amefanya hivyo lakini ukiangalia kuna roho ya uadui kati yangu mimi na huyo mtu ambaye ameamua kunifanyizia, kaamua kuingia vitani na anaweza kufanya hivyo kwa namna nyingi inaweza kuwa kisiasa au kiurafiki lakini zimenipa tabu sana, zimeisumbua familia yangu, marafiki zangu kwakweli zimenisumbua sana.”

Mhe. Komba anaendelea kwa kusema kuwa “Nimepokea simu nyingi sana mpaka nafunga simu kila anayepata anantakia mema, ni wachache wanaontukana lakini wengine wanantakia mema. Ukiangalia shingo si yangu, mwili si wangu yule binti mara akae uchi kwahiyo aliyetuma ana sababu zake na kama kweli mimi ningekuwa nafanya mambo hayo basi angezituma picha ambazo hata mimi niko uchi kama huyo mwanamke.”

“Mke wangu kanipigia simu kunipa pole , watoto wangu wote ni watu wazima wamepigia simu kunipa nguvu. Jamii imuogope Mungu mimi namwachia Mungu apigane na maadui zangu, usifanyie watu usiyotaka kutendewa.”

“Nikijua aliyenifanyia hivyo akija kwa kuniomba msamaha ntamsamehe lakini hili suala limeniathiri sana kisaikolojia hata bungeni leo sijaenda.”

Redd's Arusha wafanya ziara marie stopers

JOSE KAMILION KUNOGESHA SHINDANO LA KUMSAKA REDD'S MISS ARUSHA KESHO KATIKA VIWANJA VYA TRIPLE A

 MMOJA  wauguzi wa hospitali ya maria stopes Hamza Mzira akiwa anagawa vipeperushi kwa warembo

 Dr,Sober Mzighani  akiwa anawapa elimu warembo wanaogombania ulibwende wa jiji la Arusha waliotembelea hospitali ya maria stopes




 Picha ikionyesha warembo wakiwa wanatembelea baadhi ya ofisi za hospitali hiyo



warembo wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wauguzi wa hospitali hiyo wakati walipomaliza kupewa elimu
warembo wanaogombania taji la redd’s miss arusha wakiwa na mrembo ambae anasubiri kuachia ngazi ya urembo wa jiji la arusha Glory Stephen   nje ya hospitali ya maria stopes







Picha ikionyesha warembo wakiwa wanatembelea baadhi ya ofisi za hospitali hiyo



WAREMBO 13 wa Redd’s Miss Arusha 2014 jana  wametembelea kituo cha uduma za afya cha Maria stopes kwa ajili ya kujifunza Afya  ya uzazi wa mpango na maradhi mbalimbali ya saratani ya kizazi
Akiongea na warembo hao Msimamizi wa hospitali hiyo ya mariastopes ya jijini hapa  Dr,Sober Mzighani alisema kuwa hospitali yao imeamua kutoa elimu hiyo kwa warembo hawa ambao ni vijana ili waweze kusambaza ujumbe kuhusu uzazi wa mpango na afya ya uzazi.

Alisema kuwa elimu hii watatoa kwa  vijana wote ili wasambaze kwa wananchi nchi wote uku akisema kuwa ,vijana wengi ndio wananguvu  na uwezo wa kusambaza taarifa hizi kwa jamii .
Kwa upande wa mrembo ambaye anashikilia taji la Redd’s missArusha Glory Stephen  alisema kuwa anawashukuru sana wauguzi wa maria stopes kwa jinsi walivyowapa elimu kwani wengi wao walikuwa awajui elimu ya uzazi .

Alisema kuwa vijana wengi wamekuwa wafanya ngono uzembe wengine wamekuwa wanapata mimba pasipo mpangilio lakini kwa kutumia elimu hii na kwa kutumia nafasi zao ambazo wanazo watajitaidi kuelimisha wengine kuhusiana na uzazi wa mpango

Kwa upande wa muaandaji  wa Redd’s Miss Arusha, Faustine Mwandago, alisema kuwa warembo hao ni washindi waliotokana na mashindano ya ngazi ya vitongoji yaliyomalizika hivi karibuni.
Mwandago, aliwataja warembo hao kuwa ni Janeth Alex (20), Neema Urio (19), Lilian Deus (18), Leila Thomas (19), Husna Hamis (20), Happyness Tarimo (19), Eveline Baasa (19), na Marry Joel (21).
Wengine ni Neema Charles (19), Dyness Peter (21), Rahisa Mboye (21), Joselyn Mirashi (21), na Amber Gladys (20).
Mwandago alisema kuwa shindano hilo litasindikizwa na burudani ya aina yake kutoka kwa msanii anaewika katika nchi za afrika mashariki  Jose kamilione pamoja na wasanii mbalimbali wa Mkoa wa Arusha.

Shindano hili la kusaka mlimbwende wa mkoa wa Arusha (Redd’s miss Arusha) linatarajiwa kufanyika Juni 7 katika viwanja vya ukumbi wa Triple A na kiingili katika shindano hili vip watalipa kiasi cha shilingi 60000 huku viti vya kawaida wakilipa 30000.

CHATU MKUBWA AUWAWA KANISANI; NI BAADA YA KUDAIWA KUFUGWA NA MFANYABIASHARA NA KUHUSISHWA NA USHIRIKINA.


 ​​Kijana akiwa amembeba nyoka baada ya kucharangwa kwa mapanga akitoka naye nje ya uzio wa kanisa hilo
 Nyoka aina ya chatu aliyetolewa nyumbani kwa mfanyabiashara maarufu jijini Arusha Joseph Magesse akivutwa na wananchi kuelekea kwenye kanisa katoliki la karsamatiki eneo la Sakina jijini Arusha ambapo aliuawa kwa kucharangwa na shoka na wananchi wenye hasina na imani hizo za kishirikina
 MMOJA wawananchi akiwa ameshika shoka akiendelea kumchoronga chatu huyo
 Mabaki ya mwili wa chatu huyo baada ya kucharanwa
​​Nyumba yamfanyabishara ambapo alikutwa nyoka huyo na chini ni sehemu ya magari ya mfanyabiashra huyo

Katika hali isiyokuwa ya kawaida tukio la kuonekana kwa chatu mkubwa eneo la sakina. kata ya kiranyi lilivuta hisia ya wakazi wa jiji la Arusha na viunga vyake.

Tukio hilo la aina yake kutokea katika jiji hili lilitokea majira ya saa moja na nusu asubuhi wakati wenyeji wakiwa katika pilikapilika za kujiandaa kwenda kwenye shuguli za ujenzi wa taifa.

Chanzo cha habari hizi zinasema kuwa mmiliki wa chatu huyo ni Tajiri maarufu ambaye pia ni mfanyabiashara wa madini aitwae Joseph Magessa mwenyeji wa Musoma

Taarifa zinadai kuwa mmiliki wa chatu huyo leo alikuwa na safari ya kwenda Dar na familia yake ambapo huku nyuma alimuacha kijana ambaye anasadikiwa kuwa mtoto wa ndugu yake ambaye aliwafungulia geti na kutoka na gari

Chanzo hichi ambacho jina lake limehifadhiwa zinadai kuwa baada tu ya kijana huyo kurudi ndani alikutana na chatu huyo kitendo kilichomfanya atoke ndani kwa kasi huku akipiga kelele za kuomba msaada kwa majirani.

Baada ya kelele hizo majirani walitoka kusaidia ambapo kwa wakati huyo taarifa zilisha sambaa hali iliyofanya idadi ya watu kuwa wengi katika eneo hilo.

Mashuhuda wanadai kuwa chatu huyo alikuwa amefunikwa kichwani na kitambaa cha baibui huku kiwiliwili chake kikiwa kimefunikwa na kitambaa cheupe kilichokuwa kimeandikwa maandishi yanayo fanana ya kiharabu.

Wanachi kwa kuona hali hiyo waliamua kumburuza chatu huyo kuelekea katika Kanisa la KKKT Lutheran ambalo alipo mbali na eneo hilo.

Hata hivyo baada ya kufika hapo chanzo kilidai kuwa mmiliki wa chatu huyo hakuwa wa kanisa hilo hali iliyopelekea wananchi kumburuta tena kanisa la ST. Monica ambapo mmiliki alikuwa muumini wa kanisa hilo

Chatu huyo mwenye ukubwa wa futi 12 alipigwa na wananchi ambao walikuwa na hasira kali

Katika harakati za kumuua chatu huyo ambaye anakisiwa kufikia ulefu wa zaidi ya futi 12 zilidumu kwa takriban nusu saa, huku mashuuda wakisema kuwa joka huyo alizidi kuwa mkubwa kila alipopigwa au kukatwa.

Taarifa za ndani zinadai kuwa mmiliki wa chatu huyo alipopigiwa na mlizi wa nyumba hiyo juu ya tukio hilo alitoa kauli ya kutokuuwawa kwa chatu wake huku akidai kuwa huyo ni mama yake mzazi na kutoa onyo kuwa akikuta kauwawa atampiga mtu risasi

“Huyo chatu hawawausu naomba mumuache msimuuwe kama kuna mtu mama yake amemleta basi amuuwe

chanzo; jamii blog