Basi la wachezaji wa timu ya
taifa ya Tanzania, limekamatwa kwa amri ya mahakama kutokana na deni la
shilingi milioni 140 (zaidi ya dola 85,000), ambalo kampuni ya Punchline
kutoka Kenya, inadaiwa kulidai shirikisho la kabumbu Tanzania (TFF).
Madalali ndiyo walilikamata basi hilo likiwa kama dhamana huku TFF ikitakiwa kulipa deni husika kabla ya kurejeshewa mali zao.
Msemaji wa Shirikisho la Soka
Tanzania (TFF), Boniface Wambura, amesema tayari wamelipa shilingi
millioni 70 ikiwa ni malipo ya awali.
Deni hilo linatokana na gharama za uchapishaji
tiketi za kuingilia uwanjani katika mechi za ligi kuu ya Tanzania tangu
mwaka 1997.
TFF kwa sasa iko katika mpango wa kuuza tiketi
za uwanjani kwa njia ya ki-eletroniki (umeme) ikiwa ni sehemu ya
jitihada ya kupunguza adha kwa wapenzi wa soka na kudhibiti wizi na
ulanguzi wa tiketi.
Wambura amesema jitihada zinafanyika kumaliza
deni hilo, ila TFF italifuatilia kwa umakini na kuchunguza mwenendo
mzima uliosababisha kuwepo deni hilo.
chanzo"bbc
No comments:
Post a Comment