Aliyekuwa
mgombea mwenyekiti kupitia chama cha mapinduzi mtaa wa lolovono
amejikuta akiwekwa chini ya ulinzi mkali wa mgambo wa kata ya sokon one
baada ya kusaini posho ya halmashauri ya jiji la Arusha shilingi 20,000
bila kibali.
Mgombea
huyo aliyejulikana kwa jina la Sudy Salum Kienda alikamatwa kufuatia
barua enye tamko la mkurugenzi wa jiji la Arusha kumtaka mtendaji wa
kata ya sokon one Meery Laurence kumtia hatiani mgombea huyo baada ya
kubainika kusaini posho ya shilingi 20,000 kama mwenyekiti wa mtaa huo
hali isiyo halali.
Akizungumza
na mtuhumiwa huyo, Merry alisema kuwa january saba mwaka huu washindi
wa kiti cha wenyeviti waliitwa kwenye semina elekezi ya utendaji wa kazi
ambapo baada ya semina hiyo mtuhumiwa (Sudy )alihudhuria mkutano huo
kimakosa na kusaini posho isiyokuwa yake hivyo kuichafulia jina
halmashauri ya jiji la Arusha.
Akiwa
chini ya ulinzi alipotakiwa kujibu tuhuma hizo sudy alikiri kuchukua
fedha hizo huku akijitetea kuwa hakujua kama ni kosa ambapo hata hivyo
aliamua kuirejesha mikononi mwa mtendaji huyo.
“Mimi
sikuwa na nia ya kuiba hii hela kama mnavyonituhumu bali mimi nilifika
pale nikimuulizia mtu aliyeniita ndio nikaambiwa saini hapo uchukue hela
na mimi nikachukua sikujua ni ya wenyeviti maana nisingechukua kuepuka
kunidhalilisha kiasi hiki.
Akizungumzia
hali hiyo, mwenyekiti halali wa mtaa huo wa lolovono, Priscus Kwai
(CHADEMA) alisema kuwa si mara ya kwanza kwa mwenyekiti huyo wa CCM
kutaka kiti hicho kwa nguvu kwani awali siku ya kuapishwa pia alijaribu
kumrubuni mtendaji huyo ili kuapishwa kama mshindi wa kiti hicho ambapo
mtendaji alikataa.
“Huyu
jamaa ameshika nafasi ya tatu lakini amekuwa akitaka kiti hiki kwa
nguvu ambapo mwanzo alisambaza mtaani nimemuuzia kura na amenipa nyumba
na gari na akaja kwa mtendaji alfajiri siku ya kuapishwa na kusema yeye
ndio mshindi lakini mtendaji aligundua hilo na kunisubiri hadi saa tatu
mda wa kuapishwa nikafika na akaona aibu akaondoka” alisema Kwai
“Baada
ya kushindwa kuapishwa siku hiyo akaanza kunitishia maisha kuwa nitaona
kama nitafika mbali, ambapo siku ya semina iliyofanyika golden rose
iliyoendeshwa na mkurugenzi alienda na kujitambulisha yeye kama
mwenyekiti halali wa lolovono na kusaini hela ambayo baadae baada ya
kufuatilia ilijulikana kuwa amechukua hela bila halali na ndio
tukapigiwa sim tukaenda kumkamata”
0 comments:
Post a Comment