Mashidano ya kimataifa ya mpira wa
miguu kwa vijana chini ya umri wa miaka 15 (Rolling store) yanayoshirikisha
nchi za ukanda wa maziwa makuu yamehairishwa kwa mwaka huu kufuatia kuwepo na maswala
ya uchaguzi pamoja na kura za katiba mpya.
Mashindano ya Rolling store yenye
makao yake makuu mkoani Arusha, na kufanyika kila mwaka hapa nchini kwa
kuwaalika nchi za ukanda wa maziwa makuu kushindana kisoka yamehairishwa
kutokana na kuwepo kwa uchaguzi mkuu wa maraisi na wabunge huku pia kukiwa na
mchakato wa kupiga kura za maoni.
Akizungumza na gazeti hili,
mkurugenzi wa Taasisi hiyo ya Rolling store, Ally Mtimwa alisema kuwa makao
makuu ya taasisi hiyo yako Tanzania hivyo kutokana na kuwepo na shughuli maalum
ya kiserikali kwa mwaka huu wameamua kupisha shughuli hiyo kama kuipa heshima
nchi katika shughuli zake.
“Mashindano ya rolling store kwa
mwaka huu hakuna kutokana na kuwepo kwa shughuli za uchaguzi na pia ni mwaka wa
katiba ambapo kutakuwa na vuguvugu la kisiasa pia misukosuko ya kiuchaguzi
hivyo na sisi kama wadau wa nchi hii hatuwezi kuingilia ratiba hiyo kwani
hatuwezi kuwaalika wadau waje kushindana kindi nchi iko na shughuli maalum”
“Mbali na hilo pia hatufanyi
mashindano kutokana na mikakati mipya tunayotaka kuanza ikiwemo kufanya
mashindano kwa kuvuka mwaka mmoja mfano tukifanya mwaka huu hatufanyi mwaka
kesho hii yote ikiwa ni kuyaboresha mashindano yetu pia kupata mda wa kufanya
tathmini yetu juu ya mashindano yaliyopita”
Mtumwa alitumia nafasi hiyo pia
kuwataka wadau wa soka wa mashindano hayo kujiandikisha kuwa wenyeji wa
mashindano hayo katika nchi mbali mbali kwa mfumo huo mpya sambamba na
kuwakaribisha wadhamini kujitangaza kupitia mashindano hayo ya kimataifa
“Mimi niseme tu kuwa kutokana na
kuboreka kwa mashindano haya na kufanikiwa kwa kiwango cha hali ya juu kwa sasa
tunakaribisha nchi zingine sasa kuwa wenyeji wa mashindano haya kwa miaka ijayo
pia wadhamini watumie fursa hiyo kujitangaza kwani hadi sasa hatuna wadhamini
wakuu wa mashindano haya kwani kwa mwaka jana tulikuwa na wadhamini ambao ni
Azam tv hivyo wengine wajitokeze” alisema Mtumwa.
No comments:
Post a Comment