Katibu
mkuu wa chama cha waigizaji nchini Twiza Mbarouk amewaonya wasanii wa kike
kuacha kutumia miili yao vibaya kwa kujirahisi kingono ili kupata umaarufu
utakaopelekea kujiongezea kipato badala yake wafanye kazi za sanaa kwa ubora
itakayojiuza sokoni.
Mbarouk aliyasema hayo jijini Arusha kwenye uchaguzi
mkuu wa kuchagua viongozi wa chama cha waigizaji mkoani hapa iliyohudhuriwa na
wanachama zaidi ya 50 wanaotengeneza filamu mbalimbali na kusambaza nchini.
“Kwa sasa
jamani mabinti ifikie mahali mseme basi kujidhalilisha wenyewe kwa kutumia
miili yenu kujipatia umaarufu
utakaozalisha pesa badala yake tungeni na fanyeni kazi nzuri
itakayouzika sokoni kwani kwa njia hiyo umaarufu huja wenyewe na kipato
vilavile kuliko kutumika miili yenu”
“Mimi
niwaambie tu umaarufu wa ngono haudumu hata siku moja kwani magonjwa nayo
hayakai mbali na wewe pia unaweza ukajirahisi upate umaarufu na usipate lakini
ukifanya kazi nzuri itakupa umaarufu mzuri utakaodumu na usio na majuto wala
mateso pia kipato kitakuwa mara dufu”
Mbali na
hilo aliwataka wasanii kutumia nafasi walizonazo kujiendeleza kielim ili kuweza
kufanya kazi nzuri zitakazokwenda na wakati sokoni sambamba na kuimarisha vyama
vyao vya sanaa ili kupata maendeleo zaidi kuliko kutumia mda mwingi
kusambaratisha umoja wao.
Kwa upande
wake mwenyekiti aliyepita bila kupingwa Fredy Elifas alisema kuwa kazi kubwa
kwa sasa ya kufanya ni kuongeza wanachama kutoa 80 waliopo hadi 200 katika
mwisho wa uongozi wake lengo ikiwa ni kuongeza nguvu katika chama hicho.
“Mbali na
kuongeza nguvu lakini ni ili wanachama tunufaike na SACCOS watakayoianzisha ili
kuacha kutegemea chanzo kimoja cha mapato pekee ambacho hakitawalipa wao na
maisha yao ya baadae bali wawe na miradi itakayoendeshwa kwa fedha za mikopo
watakazopata kutoka katika taasisi mbali mbali za kifedha”.
No comments:
Post a Comment