Pages

Pages

Wednesday, February 11, 2015

ligi ya mkoa wa ARUSHA kuingia hatua ya sita bora

na Bertha Ismail - Arusha

Ligi ya mkoa wa Arusha imefanikiwa kuingia hatua ya sita bora huku kila timu ikijitamba kutwaa ubingwa huku wakiionya chama cha soka mkoa huu ARFA kutangaza bingwa wa uwanjani na siyo kubeba baadhi ya tim.

Timu hizo sita zilizofanikiwa kuingia hatua ya sita bora ni pamoja Kaloleni, Chacky, Madini, mana, namanga pamoja TPF ambapo wataanza kupambana karibuni kusaka bingwa wa mkoa huku kila timu ikitambia mwenzake.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, Mmiliki wa timu ya Kaloleni Charles Mwaim alisema kuwa timu ya kaloleni imekuwa ikipigwa majungu kwenye ligi hiyo hali ambayo wanakosa kuwa bingwa halali miaka na miaka katika ligi hiyo.

“Sisi kwa kujiangalia lazima tushinde kutokana na alama zetu hivyo tuwatake chama cha soka mkoa waache kuingilia matokeo ya mpira bali waache timu itakayofanya vema ndio awe mshindi na kama watafanya hivyo lazima tuchukue”

Kwa upande wake kocha Mkenya wa timu ya TPF fc, Abdallah Shakir alijitamba kuwa hatua ya sita bora ni moja ya malengo yao waliyokuwa nayo ya kufanikisha safari yao ya kuwa bingwa wa mkoa watakaokwenda kuleta mabadiliko katika ligi ya mabingwa wa mikoa.

“Mimi nimetoka Kenya kuja hapa kufanya kazi siyo kueneza injili na kazi kubwa ni kuifanikisha timu hii inakuwa bingwa hivyo niwatake wenzako wasiache kutusindikiza katika kupata ubingwa huu kihalali kama chama cha soka hawatatukandamiza” Alisema Shakir

Kwa upande wake mmiliki wa timu ya tajiri ya madini fc, Athumani Mhando alisema kuwa kwa mazoezi ya timu yake hawezi kuzungumza mechi kwani dakika 90 za uwanja ndio zitaamua kutoa matokeo.

mwisho.........

No comments:

Post a Comment