Jeshi
la polisi kanda maalum ya Dar es Salaam limepiga marufuku maandamano ya
jumuia ya vijana wa chama cha wananchi CUF yaliyokuwa yafanyike Feb 13
mwaka huu.
Kamishna wa polisi kanda maalum ya Dar es Salaam Suleiman Kova
akizungumza na waandishi wa habari amesema .
hata hivyo licha ya jeshi la
polisi kupiga marufuku maandamano hayo vijana hao wamesisitiza kuwa
maandamano yao ya kuitaka tume ya uchaguzi kuongeza siku za kuandikisha
daftari la kudumu la wapiga kura yanayotarajiwa kufanyika Feb 13 yako
palepale.
Mwenyekiti wa JUVICUF taifa Bw Hamidu Bobali ameyasema hayo jijini
Dar es Salaam ambapo amesema maandamano yao mbali na kuishinikiza tume
kuongeza siku za kujiandikisha pia yana lengo la kulani ukiukwaji wa
haki za binadamu unaofanywa na jeshi la polisi nchini na kuongeza kuwa
hawawezi kusitisha kutokana na hoja wanazotaka kuwasilisha zina maslahi
mapana kwa taifa.
No comments:
Post a Comment