Timu ya
Tanzania veterani imewachabanga timu ya maveterani wa Kenya kwa jumla ya magoli 2-1 katika
mechi ya kirafiki ya maveterani hao mapema mwishoni mwa wiki katika uwanja wa
Sheik Amri Abeid ya jijini Arusha.
Timu ya
Maveterani kutoka Kenya ijulikanayo kama Senious Footbal club walionesha uwezo
mkubwa wa kusakata kandanda safi mithili ya Serengeti boy lakini pamoja na
uwezo huo walishindwa kulinda lango lao vema na kuipa nafasi timu ya maveterani wa Tanzania “Arusha
all stars” kutikisa nyavu zao dakika ya 35 kupitia kwa mchezaji wao Abdulrazaki
Hussein matokeo yaliyodumu hadi mda wa mapumziko.
Kipindi cha
pili kilianza huku mashambulizi makali yakielekezwa zaidi kwa lango ya Tanzania
kwa mikwaju mikali ambayo hata hivyo iliokolewa na mlinda mlango mahiri wa
Arusha all stars Godrich Samweli na baadae dakika ya 75 Kenya walisawazisha
goli hilo kwa njia penalt iliyopigwa na Varees Aura, baada ya mchezaji wao
kufanyiwa madhambi eneo la hatari.
Matokeo hayo
yalionekana dhahiri kuwaamsha usingizini timu ya Arusha All stars na kuanza
kuchangamkia lango la Senious fc ya Kenya ambapo mbali na mikwaju kadhaa kuchomolewa
lakini dakika ya 80 Richard Lukas Manyika alifanikiwa kupiga shuti kali
lililomuacha mlinda mlango wa Kenya na mpira huo kujaa nyavuni matokeo
yaliyodumu hadi mwamuzi wa kati Gasper Ketto alipopuliza kipenga cha kuashiria
mchezo kwisha.
Akizungumzia
mechi hiyo, Katibu wa Arusha All stars alisema kuwa wameamua kuvuka mipaka ya
Tanzania kwa kuwaalika maveterani wenzao wa Kenya wacheze pamoja huku ikiwa
kama mazoezi kwao katika mashindano makubwa ya pasaka sambamba na kufahamiana
lakini pia kujenga undugu wa kisoka baina ya nchi hizi.
“Sisi kama
Arusha all stars tumevuka mipaka na kucheza na timu ya Senious ya Kenya ambapo tunadumisha undugu
wetu lakini pia ikiwa ni kama sehemu ya kutafuta marafiki wa soka ili
kuendeleza soka la mkoa wetu na nchi kwa ujumla”
Mwisho……………………….
No comments:
Post a Comment