Pages
▼
Pages
▼
Monday, March 23, 2015
Zitto kuvuta 13 ACT
Aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto
ALIYEKUWA Mbunge wa Kaskazini, Zitto Kabwe amejiunga rasmi na chama cha siasa cha ACT, huku akisema ana kundi kubwa la watu watakaomfuata, wakiwemo wabunge 10 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano ya Tanzania.
Aidha, Diwani wa Chadema Kata ya Mabogini Moshi Vijijini, Wakili maarufu Albert Msando, naye amejiunga na chama hicho kipya, akiutema rasmi udiwani wake.
Zitto, mmoja wa wanasiasa mahiri vijana, alitangaza kuhamia ACT jana katika mkutano wake na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Alisema anajua anachokifanya, hivyo kuhamia kwake ACT si kwa bahati mbaya, huku akisema pamoja na uchanga wa chama hicho, atahakikisha kinakua kwa kasi na hata kupiku baadhi ya vyama vya siasa vyenye umaarufu kwa sasa.
Akizungumza na gazeti hili jana jijini Dar es Salaam, baada ya kuzungumza na waandishi wa habari, Zitto alisema nyuma yake wapo wabunge zaidi ya 10, watakaojiunga na ACT muda sio mrefu.
“Siko mwenyewe wapo wenye mapenzi mema na tunataka kufungua ukurasa mpya kwa nchi yetu wa siasa za kujenga nchi, wabunge mahiri wa CCM na Chadema zaidi ya 10, watajiunga nami, ila sitakutajia majina kwa sasa kwa sababu ya sheria za vyama vyao, acha wamalizie vipindi vyao vya ubunge,” alisema Zitto ambaye jana alishawishi watu 12 kujiunga ACT, akiwemo msanii nyota wa muziki wa kizazi kipya, Selemani Msindi ‘Afande Sele’.
Awali, Zitto akizungumza na gazeti hili, alisema yeye ni mwanachama rasmi wa ACT mwenye kadi ya uanachama namba 7184, na kwamba amelipia ada ya miaka 10, ya uanachama wa chama hicho, ambayo kila mwaka ada ni Sh 1,000.
“Nimejiunga rasmi na ACT na nimelipa ada ya miaka 10 ya uanachama, nawakaribisha wote wenye mapenzi mema ya kujenga nchi wajiunge nasi”,alisema Zitto. Majimbo 6 yanamsubiri.
Akizungumzia uchaguzi mkuu ujao, Zitto alisema atagombea nafasi ya ubunge kwa kuwa umri wake hauruhusu kugombea nafasi ya rais, na kwamba jimbo atakalogombea litawekwa wazi baada ya yeye kushauriana na washauri wake, kwa kuwa majimbo zaidi ya sita nchini yanamtaka agombee.
“Nitasema hapo baadaye ninagombea jimbo gani, kwa sababu majimbo mengi yananiita nikagombee; Kawe wananitaka, Segerea, Kasulu, Kahama, hivyo nitazungumza na wenzangu halafu nitasema nitagombea wapi”, alisema Zitto.
Alitetea uamuzi wake wa kuhamia ACT, akisema ni uamuzi sahihi kwa kuwa chama hicho kinaendana na kile alichokuwa anakipigania kwa miaka
No comments:
Post a Comment