Bertha
Ismail – Arusha
Kamati huru
ya uchaguzi wa uongozi mpya wa chama cha soka wilaya ya Arusha, imefunga Rasmi pazia la uchukuaji fom wa
kugombea nafasi mbali mbali katika chama hicho.
Zoezi la
uchukuaji fom wa kugombea uongozi wa ADFA, ulianza rasmi April 15 na kufungwa
mapema jana april 20 ambapo wadau wengi wa soka wameonekana kuogopa nafasi hizo
zilizoachwa wazi na kupelekea idadi ndogo ya wagombea huku nafasi zingine
zikikosa wagombea.
Awali wadau
wengi jijini Arusha walionekana kutolea macho viti hivyo kabla tarehe ya
uchaguzi kuanza lakini baada ya tarehe ya uchaguzi kutangazwa wengi wameonekana
kukaa nyuma kutazama wachuaji fom bila kujishughulisha.
Akizungumza
na gazeti hili, katibu wa kamati huru ya uchaguzi, Hussein Lembarity alisema
kuwa nafasi zilizo wazi ni nafasi 10 ambazo kila mmoja ingefaa kuwa na wagombea
watatu hadi watano lakini ambao ni zaidi ya watu 30 lakini anashangazwa na watu
waliojitokeza ni watu 10 tu huku baadhi ya nafasi zikigombewa na mtu mmoja au
wawili na zingine zikikosa kabisa wagombea.
“Mwanzo
tulipochgauliwa tu watu wengi sana walijitokeza kuponda uongozi uliopo na
kuahidi kuchukua fom za kupindua uongozi huu lakini baada ya kuanza kutoa fom
watu wanachenga hali iliyopelekea nafasi zingine kukosa wagombea huku zingine
zikiwa na mashaka ya kupita ila kwa sababu tumefunga pazia hilo hatuna budi
kukubali matokeo na sasa ni nafasi ya kuweka pingamizi hadi april 24 kwa
gharama ya 50,000”
Akitaja
majina ya wagombea hao alisema kuwa nafasi ya mwenyekiti imegombewa na mtu
mmoja ambae ni Omary Walii, makamu mwenyekiti mgombea mmoja Elisha Sironga huku
nafasi ya katibu mkuu Zakayo Mjema akitetea nafasi yake na mpinzani ni Abdul
Kondo na katibu msaidizi mgombea ni Athumani Juma na mweka hazina mmoja, Omary
Kondo.
Kwa upande
wa wajumbe wa mkutano mkuu wagombea ni Mwalizo Nassoro na Ayub Juma Kilabula
huku nafasi ya uwakilishi wa vilabu akigombea mtu mmoja, Robert Munisi.
“Hao ndio
wagombea na tumebandika majina hayo ukutani mwa uwanjan wa Sheik Amri Abeid kwa
ajili ya watu kuleta pingamizi za wagombea hawa kama hawajatimiza sifa ya
kugombea uongozi wa soka wilaya ikiwemo kuwa mkazi wa hapa jijini, elimu ya
kidato cha nne, au kama hana uzoefu wa mpira wala taaluma ama aliwahi
kuhukumiwa kwa kosa lolote”.
Uchaguzi huo
wa ADFA unatarajiwa kufanyika mapema may 2 mwaka huu katika ukumbi wa viwanja
vya Sheik Amri Abeid huku wajumbe na vilanu vyote vikitakiwa kulipa ada au
kusajiliwa ili kuwa wajumbe halali wa mkutano huo na kupata kiongozi
watakaempenda na kumwamini.
Mwishoo………………………
0 comments:
Post a Comment