Bertha
Ismail - Hanang’
Mwanariadha
Emmanuel Giniki amezidi kung’ara katika mbio mbali mbali za hapa nchini, baada
ya mwishoni mwa wiki hii kung’ara tena katika mbio za may day kwa kukata upepo
wa km 21 kwa kutumia saa 1: 01:17 na kuwaacha wenzake zaidi ya 70.
Mbio hizo
zilizofanyikia Katesh makao makuu ya wilayani hanang’ kwa ajili ya kuadhimisha
sikukuu ya wafanyakazi, Giniki alifanikiwa kuwa wa kwanza kumaliza mbio hizo
akifuatiwa na Msandiku Mohamed aliyemaliza kwa saa 1:03:18 na aliyeshika nafasi
ya tatu ni Stephano Huche 1:03:21.
Kwa Upande
wa wasichana Anjelina Tsere alifanikiwa kutwaa ushindi baada ya kumaliza mbio
hizo za km 21 kwa kutumia saa 1 :16: 43 akifuatiwa kwa karibu na Rozalia
Fabiano kwa kutumia saa 1:21;15 na Amina Mohamed akishika nafasi ya tatu kwa
kutumia saa 1:21:43.
Mgeni rasmi
katika mbio hizo ni aliyekuwa waziri mkuu zamani Fredrick Sumaye ambapo mbali
na kupongeza uongozi wa riadha manyara na waandaji aliwataka kuendeleza
mashindano ya mara kwa mar ili kuwaweka wanariadha katika hali ya kufanya
mazoezi ya mara kwa mara na kufanikiwa kushinda mbio za kimataifa hatimaye
kurudisha heshima ya mkoa huo katika historia riadha.
Kwa upande
wa waandaji , Alfredo Shahanga alisema kuwa kwa sasa wameamua kuendesha
mashindano ya mara kwa mara ya mchezo huo ili kuwaweka wachezaji sawa kupambana
katika michuano ya kimataifa iliyoko mbele yao ikiwemo ya All afrika game hivyo
waweze kujitathimini mapema.
Mwisho……………….
No comments:
Post a Comment