Bertha Ismail - Arusha
Chama cha
soka wilaya ya Mbulu, Kimeipongeza shirikisho la Soka nchini kwa kutambua
umuhimu wa wilaya hiyo kimichezo na kuwapa nafasi ya kuwa moja ya vituo vitatu
vya michuano ya ligi ya mabingwa wa mikoa Tanzania inayotarajia kutimua vumbi
may 2 mwaka huu.
Michuano
hiyo ya RLC itashirikisha jumla ya timu 27 nchini katika vituo vitatu vya Mbulu
(Manyara) , lindi na Sumbawanga ambapo kila kituo inatarajiwa kuwa na timu tisa
ambapo kwa Mbulu kutakuwa na timu ya Madini (Arusha), alliance school (Mwanza),
Bariadi united (Simiyu) zingine ni Baruti (Mara), Lukirini fc (Geita), Mtwivila
City (Iribga), RAS Kagera fc (Kagera) pamoja na Small Prison (Tanga) na
Watumishi fc (Shinyanga).
Ugeni huo
mkubwa umewapa motisha kubwa wakazi na viongozi wa soka wilaya ya Mbulu na
kufurahia nafasi hiyo adimu huku wakitoa shukrani zao za dhati kwa shirikisho
la soka Tanzania kwa kutambua mchango wao huku wakisema kutumia michuano hiyo
kama mafunzo kwao.
“Kiukweli
tumefurahi sana TFF kutuletea michuano hii kwani itakuwa kama fursa kwetu ya
kujifunza nini wenzetu wanafanyaga na tujifunze kwa kuiga ili na sisi tusonge
mbele kisoka kwani imekuwa ikituuma sana zaidi ya miaka 10 hatujaonja ligi kuu
na miaka mitano hatujui ligi daraja la kwanza likoje” alisema katibu wa soka
wilaya ya Mbulu Fortunatus Kalewa.
“Tunashukuru
timu nyingi zimeshaweka oda ya sehemu za malazi na viwanja vya mazoezi ikiwemo
timu ya madini fc ya Arusha hivyo naamini itakuwa fursa kwetu kuwaleta
wachezaji wa timu mbali mbali za mkoani hapa kuja kuiba mbinu wanazotumia
wenzetu katika mashindano hadi wanasonga mbele na kuwakilisha mikoa yao katika
ligi za ngazi za juu”
Kituo hicho
cha Mbulu mashindano ya ligi ya mabingwa wa mikoa inatarajiwa kuanza kutimua vumbi may 9 katika
viwanja vya Nyerere wilayani mbulu mkoani Manyara ambao uko katika hali nzuri
kimandhari na uzio ingawa majukwaa bado ni changamoto.
Mwisho………………….
No comments:
Post a Comment