Pages

Pages

Monday, May 11, 2015

Mmoja afariki kwa kutumbukia bwawani- Arusha.

mwili wa Ibrahim baada ya kuopolewa kwenye bwawa hilo na wasamaria wema baada ya wataalam wavamiaji kukosekana

Arusha. Mtu mmoja,  Ibrahim Issa (25) amekufa maji baada ya kutumbukia kwenye bwawa lenye maji linalomilikiwa na kampuni ya Kili flora lililoko eneo la Mlangarini Wilayani Arumeru mkoani Arusha.
mwili ukipelekwa pembezoni mwa bwawa tiyari kutolewa kwenye maji
baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya maua ya kili flora wakiwa wanashuhudia mwili wa mwenzao baada ya kuopolewa kwenye bwawa.

jeshi la polisi pamoja na maafisa wa zima moto wakiondoa mwili eneo la tukio kuupeleka chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya mkoa mount meru tiyari kwa mazishi
Mwili huo uliodumu kwenye maji kwa muda wa masaa 26, uliokolewa na wasamaria wema waliojitolea kuutafuta mwili huo ili kuutoa kwenye bwawa alikotumbukia lenye kina cha maji mita 20 chini na mita 500 urefu.
Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo ya Kili flora walisema  kuwa marehemu alitoka mapumziko ya kunywa chai saa nne asubuhi may 8 mwaka huu na kubeba waya aliyotengenezea ndoano kwa ajili ya kwenda kujipatia samaki lakini kwa bahati mbaya aliteleza na kuangukia ndani ya maji.
“Kwa mbali tulisikia kama kuna kelele bwawani nyuma ya mashambani na tulipokwenda kutazama tulimuona Ibrahim (Mrehem) Akiomba msaada na tukafanya juhudi za kumrushia kamba kuvuta lakini haikuwezekana kwani alishachoka na ndipo alipozama”alisema Jane Macha
Macha alisema Tulitoa taarifa kwenye uongozi kumuokoa mapema lakini hata hivyo ilishindikana kwa kutolewa ruhusa ya haraka kutokana na makao makuu ya uongozi kuwa USA, eneo ambalo ni mbali na hapa hivyo baadae uongozi ulipofika ulikuwa unasua sua kufanya taratibu za kumuokoa mapema hivyo wananchi walijitosa kwenye maji na kuanza kumtafuta  kucha bila mafanikio.
Mwenyekiti wa mtaa wa Olomitu, kata ya Mlangarine, Absalom Kambaine  alisema kuwa ingawa alichelewa kupata taarifa lakini siku ya pili asubuhi ya May, 9 alikwenda  kuomba msaada wa kuupata mwili kwa wataalam wa maafa wakiwemo jeshi la polisi, jeshi wananchi kikosi 977kj, na kikosi cha zima moto lakini hakufanikiwa kwa kile kinachodaiwa ukosefu wa vifaa.
“Kiukweli nimepata taarifa asubuhi hii nikaamka na kukimbia kimbia kwa wataalam ambapo zimamoto walifika eneo la tukio lakini walisema hawawezi kuupata mwili huo kwani hawana vifaa vya uokoaji majini pia wataalam wa kuzama, nikaenda kambi ya jeshi hii hapa karibu moshono nao wakasema hakuna wataalam wa uzamiaji majini bali wapo wavuvi pekee na hawataweza kufanya kazi hiyo hadi kibali makao makuu pia polisi walifika hapa lakini wao wakasema wamekuja kuweka ulinzi na kusubiri mwili tu” alisema mwenyekiti Kambaine.
Kwa upande wa baba mzazi wa marehem Joseph Issa alisema  kuwa hali hiyo ya mwanae kuzama na kukaa ndani ya maji kwa zaidi ya masaa 26 ni uzembe wa vikosi husika na serikali kwa pamoja kukosa vifaa vya uokoaji ndio maana maafa yanatokea mara kwa mara huku hakuna anaejishughulisha na tahadhari hivyo wanamuachia Mungu swala hilo,
Mwisho……

No comments:

Post a Comment