Timu ya Arusha mpira wa kikapu (wa kwanza kushoto ndie katibu wa mchezo huo Mkoa) |
Bertha Ismail - Arusha
Timu ya
mpira wa kikapu ya Jiji la Arusha ni miongoni mwa timu za majiji za Nchi za
Afrika yanayoshiriki mashindano ya mpira wa kikapu kila mwaka, lakini kwa mwaka
huu Ukata unaoindama timu hiyo imeshindwa kabisa kuwakilisha katika mashindano
hayo ya mwaka huu yaliyoanza kutimua vumbi katika uwanja wa ndani wa Taifa
jijini Dar es salaam jana.
Akizungumza
kwa uchungu mkubwa, katibu wa Mpira wa kikapu mkoa wa Arusha Bariki Kilimba
aliliambia gazeti hili kuwa wameshindwa kwenda kushiriki michuano hiyo
kuwakilisha jiji la Arusha kutokana na kukosa kiasi kidogo cha pesa
kilichopelea huku wadau wakishindwa kuwasaidia.
“Kiukweli
imeniuma sana kushindwa kushiriki mashindano haya makubwa Afrika kwa sababu tu
ya kukosa kiasi kidogo cha pesa kwani bajeti yetu ilikuwa ni milioni 1.6 hivyo
tulitembea kwa wadau ikiwemo jiji la Arusha na kwa mkuu wa mkoa lakini
tuliambulia patupu, ila kwa sababu tuna moyo tuliamua kuchangishana kwa wale
wenye uwezo ambapo tulipata laki 8 na wachezaji wengine ni wanafunzi hivyo
walishindwa kuchanga na fedha ikapelea”
“kUfuatia
hali hiyo tulianza kutafuta marafiki wa karibu yetu lakini wengi hawakuwa na
uwezo wa kutusaidia hivyo tukaamua tu kutulia na nafasi yetu bado ipo hewani
hivyo tunaomba kwa watu wenye uwezo jamani watusaidie bado tuna nafasi ya
kuwakilisha jiji letu kwenye nchi za
Afrika au kampuni na taasisi zitusaidie nasi tutawatangaza kwenye nchi hizi
shiriki” alisema Kilimba.
Timu hiyo ya
wanaume yenye jumla ya wachezaji 10 ilianza mazoezi makubwa tangu mwezi
uliopita huku wakifanya mashindano ya
mara kwa mara za kirafiki kujifua kwa ajili ya mashindano hayo ya majiji wakiwa
na matumaini makubwa ya kurudi na ushindi lakini ukata umekatisha ndoto zao.
Aidha
michuano ya mpira wa kikapu kutoka majiji ya Afrika yameanza jiji Dar huku timu
kutoka sehemu mbali mbali zikishiriki ikiwemo majiji ya Tanga, Mwanza, Kampala,
Kigali Entebe, Nairobi Mombasa, Mogadishu, Hargeisa (Somalia), Bujumbura,
Garowe, Diaspora, Bentieu, Malakal,Juba, Cairo n.k.
No comments:
Post a Comment