Pages

Pages

Tuesday, July 28, 2015

Mtanzania Singh bingwa wa michuano ya Utrack nane nane Rally, 2015

magari tiyari kwa kuondoka check point mmoja mmoja
Displaying rally miller.jpg
gari la dereva maarufu kwa mbio za magari kutokana na kushinda kwake Gerald Miller akikata nyika katika michuano ya Utrack nane nane Rally yaliyofanyika Arusha.

Bertha Ismail - Arusha

“Nimefurahi sana kuona  jinsi kiwango changu kinapanda na naamini hii ni mwanzo wa kutimiza ndoto zangu za kuwa mtaalamu wa mchezo wa gofu niweze kushindana kwa kulipwa na kuwa mchezaji maarufu wa mchezo huu na kuiwakilisha nchi yangu vema”.

Ni maneno ya kijana mdogo aliyeko kundi la Junior Mohamed Ally alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuibuka mshindi wa jumla katika michuano ya Arusha Open yaliyoshirikisha wachezaji 82 wa gofu kutoka mikoa mbali mbali nchini pamoja na nchi za Dubai na Kenya.

“Mimi ndoto zangu ni kuwa profesheno wa gofu nchini ili niweze kuwa mchezaji wa kulipwa na kuchuana katika mashindano mbalimbali ya kitaifa na kimataifa na kuitangaza nchi yangu hivyo watu wasishangae uwezo wangu wakalinganisha na umri wangu wa chini ya miaka 18 bali waangalie kipaji change na ndoto zangu ambazo siri hii ni mazoezi ya mara kwa mara kama sala kwangu”

Ally wa Arusha ametwaa ushindi wa jumla baada ya kupata nyavu 131,  (131 nett) katika kumbi 36 (36 halls) kwa siku mbili, huku kwa daraja la kwanza Richard Gomes (Arusha) akitwaa ushindi kwa kupata nyavu 152 nett akifuatiwa na Victor Joseph wa  Dar –es-salaam kwa kupata pia nyavu 152.

Kwa upande wa daraja la pili Prabvir Singh alitwaa ushindi kwa nyavu 146 akifuatiwa na Muzzafer Yusufally  kwa nyavu 156 wote wa Arusha na daraja la tatu Hiten Nathwan ambae ni mwenyekiti wa Arusha Gymkana Club kwa nyavu 150 akifuatiwa na Mona Singh kwa vyavy 151.

Akizungumzia mashindano hayo mwenyekiti wa mashindano kutoka chama cha Gofu Taifa alisema mashindano hayo ya Taifa yaliyoko kwenye kalenda ya TGU yana lengo la kutambua wachezaji wazuri wa machezo huo, kukuza vipaji vya vijana wadogo sambamba na kuvinoa vilivyopo.

“Kwanza niseme tu nimefurahishwa na uwezo mkubwa aliyoonyesha kijana mdogo Ally ukilinganisha na umri wake hali ambayo inatia moyo kuwa kwa sasa vilabu vina wachezaji wazuri watakaounda timu ya nchi yetu na kuna baadhi ya wachezaji wengine tumewaona na tutawaangalia tena kwenye michuano ya Taifa yatakayofanyika Moro goro”

“Lengo la mashindano hayo ya Morogoro ni kutafuta wachezaji wazuri watakaounda timu ya Taifa itakayokaa kambini kwa kujinoa kushiriki michuano ya nchi za  Afrika mashariki na kati yatakayofanyika Octoba nchini Kenya”

Mashindano hayo ya Arusha Open yaliyodhaminiwa na I&M bank yajulikanayo kama “I&M Golf Arusha Open” yameshirikisha wachezaji 82 kutoka vilabu vya Arusha, Dar, Moshi, TPC, Lugalo, Nairobi na Dubai.

Displaying IMG-20150725-WA0030.jpgDisplaying IMG-20150725-WA0021.jpg

Kijana Mohamed Ally atwaa ushindi wa "I&M Arusha open Golf competition"

Mwisho…………….

Nangolo : Lowassa alionewa kukatwa jina na Kamati ya CCM

Bertha Ismail

Arusha . Pamoja na kuwa chama cha mapinduzi imekamilisha zoezi la kumpata mgombea Urais wa chama hicho mwezi Octoba mwaka huu lakini Dhambi ya  kumkata  aliyekuwa  mmoja wa wagombea Urais Edward Ngoyai Lowassa imeendelea  kukitafuna chama hicho baada ya mwenyekiti mkoa wa Arusha Onesmo Ole Nangole kuonyesha wazi kuumizwa na matokeo hayo.

 Hali hiyo imejitokeza jana mkutano maalumu  wa uchaguzi wa wabunge viti maalumu kupitia Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) uliofanyika  katika ukumbi wa mikutano wa AICC mjini hapa ambao ulihudhuriwa na wajumbe kutoka wilaya zote za mkoa wa Arusha ambazo ni Longido, Ngorongoro, Karatu, Arumeru, Arusha mjini na Monduli.

Nangole alisema kuwa pamoja na kamati kuu ya CCM kumpitisha Dr. Magufuli lakini uchaguzi huo haukuwa wa haki na usawa kwani hata Lowassa alikuwa na sifa zote za kupitishwa kwenye hatua za awali lakini alikatwa jambo ambalo limewaumiza sana na hadi leo wana Arusha wanaumwa kutokana na haki haikutendeka pamoja na kujitokeza kunyosha mkono kutoa hoja kwenye mkutano huo lakini walizuiliwa

“Naomba niseme kwa hili CCM iliyofanya imesababisha chama chetu kuingia kwenye hali ya chuki na kuendesha mapambano ya sisi kwa sisi badala ya mapambano hayo kuelekeza upinzani hali ilipelekea baadhi yetu kuchukua maamuzi magumu ya kuhama chama na kusaliti ,.. na kutokana na hili chama chetu hakitafika mbali kama watakuwa wanawafanyia hivi watu wenye sifa, na ijulikane kuwa chama hiki ni cha watu wote hivyo tusijione wengine wakubwa na kuwadharau wengine kwa kutumia vyeo vyetu kuwadhalilisha”

  “Ndugu zangu baadhi yenu hamkuwepo kwenye huu uchaguzi hivyo niwaambie wazi kuwa Lowasa alionewa kwani sifa za kamati ya maadili kumpitisha lakini kutokana na chuki binafsi bila kujali ni chaguo la wananchi wengi wanamkubali wakamkata” alisema Mwenyekiti Ole Nangolo ambae alishangiliwa mda wote kuonyesha maneno hayo yanawagusa wajumbe.

Nangole akizungumza kuhusiana na uchaguzi huo wa UWT, aliwataka
wanawake kufanya maamuzi sahihi ya kuwachagua viongozi wenye uchungu na mapenzi mema na wanawake hao ambao watakuwa tayari wakati wowote kubeba matatizo yao.

Aliwataka wanawake hao kuchagua  viongozi  ambao  watakuwa tayari
kufika katika maeneo ya wananchi kusikiliza kero zao na kuzipatia
ufumbuzi na sio viongozi wanaofika kwa mwaka mara moja pindi
wanapohitaji  kura .

‘kila mmoja anajua kuwa kazi ya mbunge ni kushughulikia kero za
wananchi usiku na mchana na sio kuwafuata wananchi kwa msimu  na nyie wenyewe mnawafahamu vizuri msifanye makosa katika uchaguzi huu chagueni kiongozi kwa manufaa yenu wenyewe ‘alisisitiza Nangole.

Naye Katibu  wa UWT Mkoa wa Arusha, Fatuma Hassan aliwataka wanawake hao kuhakikisha wanawachagua viongozi wanaojali maslahi ya wananchi hususani wanawake  kwani hivi sasa ndipo wanapotakiwa kufanya maamuzi yaliyo sahihi.

Aliwataka  wanawake hao kuwa  makini katika kuwachagua viongozi wenye kujali shida na changamoto za wananchi na watakaokuwa tayari kuleta maendeleo kwa wakazi wa jiji la Arusha na wasikubali kurubuniwa na mtu yeyote bali maamuzi wafanye wao wenyewe.

Kwa upande wake msimamizi wa Uchaguzi huo ambae ni mkuu wa mkoa wa Arusha Daudi Filex  Ntibenda alisema kuwa endapo wajumbe hao watafanya makosa ya kumchagua mtu asiyekubalika basi wasilalamike kuwa hawana maendeleo bali wawalaumu waliompa dhamana.

Mwisho.

Panone fc yazitamani simba na Yanga

Bertha Mollel,

Displaying IMG-20150706-WA0004.jpg
TIMU YA PANONE FC YA KILIMANJARO

 Ama kweli timu ya Panone fc ya mkoani Kilimanjaro imepania kupanda daraja msimu ujao wa ligi na hii ni baada ya Kocha wake mkuu Atuga Manyundo kuweka wazi ratiba ya mazoezi yake ikiwemo wiki mbili za mwisho kucheza mechi za kirafiki na timu kubwa za Simba, Mbeya city na Yanga.

Timu hiyo iliyoingia kambini kwa kujinoa ili kujiwinda na ligi daraja la kwanza msimu ujao chini ya kocha mkuu Manyundo alisema kuwa mara baada ya timu kuingia kambini yapo mapungufu mengi wameyaona ikiwemo Ubutu wa nafasi ya mlinda mlango, fowadi na kiungo hivyo kwa sasa anashauriana na benchi zima la ufundi kuanza usajili mapema.

“Nimeona nafasi butu ambazo nimekueleza ambazo kwa sasa tuko njiani kupiga hodi katika sehemu mbali mbali kusaka wachezaji watakaojaza hizo nafasi na kuwa kali kweli kweli lengo ni kutowaangusha wana Kilimanjaro katika msimu ujao lazima tupae hadi ligi kuu”

“Ila kikubwa kwa sasa ni kuwapa wachezaji waliopo mazoezi ya pumzi, kasi ya mpira na ukabaji na baada ya hapo ratiba yetu inasema tucheze mechi za kirafiki na timu kubwa kujua mapungufu, kama unavyojua sisi ni timu ya ligi kuu ijayo hivyo lazima tucheze na timu za ligi kuu na kama unavyojua Simba na Yanga ndio chaguo letu la kwanza”

“Ila kwa sasa macho na masikio yetu ni kucheza na vilabu vya Mbeya city, vilabu vya hapa Tanga kama Prison ili tujue wanavyocheza na sisi tujue mapengo yetu ni yapi na kuyajaza mapema maana huu mwaka kwetu ni kazi tu hakuna kuremba” alisema Atuga”

Kwa upande wake katibu mkuu wa kikosi hicho Augustino Mwakatumbula alisema kuwa kutokupanda kwa timu hiyo hawatakuwa na sababu yoyote kutokana na tiyari mazingira mazuri ya kupanda yamewekwa ikiwemo malazi, chakula na usafiri pamoja na posho nzuri za wachezaji .

“Yaani mimi niseme tu kuwa kama wachezaji wetu wasipotufurahisha kwa mwaka huu basi kwani hawatakuwa na sababu yoyote ya msingi ya kushindwa kushinda kutokana na mazingira mazuri tuliyowawekea na sasa tunaangalia kocha tu usajili anaoutaka ndio tuufanye hadi kieleweke”

Mwisho…………………

Jiji la Arusha yajivunia BVR.

MKURUGENZI WA JIJI LA ARUSHA

Halmashauri ya jiji la Arusha limefanikiwa kuitimisha zoezi la uandikishaji wa daftari la wapiga kura kwa kuandikisha jumla ya wananchi 321,575, huku mkurugunzi wa jiji hilo akiwataka wote waliojiandikisha kujitokeza kupiga kura.

Akizungumza na gazeti hili wakala wa uandikishaji jiji la Arusha, Iddi Juma ambaye pia ni Mkurugenzi wa jiji alisema kuwa awali walitarajia kuandikisha watu 265,087 lakini wamefanikiwa kuvuka lengo kwa zaidi ya asilimia 21 kwani wameandikisha watu 321,575 ambayo ni sawa na asilimia 121.

“Tunajivunia kuvuka lengo letu la idadi ya walioandikishwa lakini hatuwezi kujivunia kwa uandikishaji tu bali tutajivuania zaidi pale idadi hii waliyojiandikishwa wakijitokeza wote kupiga kura octoba kwenye uchaguzi mkuu wa kupata viongozi mbali mbali wa nchi”

“Nimesema hivyo kwa sababu vijana wengi walioonekana kupata vitambulisho hivyo walifurahia tu kuwa itawasaidia katika mambo yao binafsi lakini siyo kupia kura, lakini naomba niwaambie kuwa kupata kitambulisho ni jambo moja lakini kupiga kura ni jambo la msingi zaidi hasa ikizingatiwa ni haki ya msingi kupata kiongozi aliyepatikana kwa kura yako hivyo wajitokeze kwa wingi kupiga kura”

Mkuu huyo amesema kuwa kumekuwa na mazoea ya wananchi kutokujitokeza katika zoezi la upigaji kura kutokana na kuendekeza starehe pamoja na biashara na kusema kuwa swala hil ni kosa kwa sheria ya nchi hasa kutokana na gharama kubwa serikali inayotumia kuhakikisha zoezi hilo linafanikiwa hivyo kwa mwaka huu Arusha wasifanye kosa hilo bali wajitokeze kuchagua kiongozi wanaemtaka kwa maendeleo ya jiji, mkoa na nchi kwa ujumla.

Zoezi la uandikishaji wa wapiga kura jiji la Arusha lilianza june 16 na kufikia tamati julai 18 huku wanawake 160, 143 wakijiandikisha na wanaume 161, 432 katika vituo 183 katika kata 25 za jiji la Arusha.

“Katika zoezi hili naamini hakuna mtu asiyejiandikisha hasa baada ya kuruhusu watu wenye kazi au biashara wajiandikishe kwenye vituo vya biashara zao kutokana na ugumu wa kutoka, na pia hili linajidhihirisha siku tatu za mwisho hakukuwa na foleni kabisa kwenye vituo vya uandikishaji huku vituo vingine wakala wakikosa kabisa wateja la kushinda wakipiga soga hii inaonyesha kabisa watu wamemalizika na kama kuna watu wasiojiandikisha basi hawakutaka tu”

Mwisho…………

Arusha FC yahitaji milioni 28 kumudu SDL.

Timu ya Arusha fc inayoshiriki ligi daraja la pili msimu ujao wa ligi ya Tanzania bara imejikuta ikihitaji zaidi ya milioni 28 kwa ajili ya kugharamia timu hiyo hadi kumalizika kwa SDL msimu wa 2015/2016, hivyo kuwaomba wadau watoe ushirikiano wao kuhakikisha fedha hizo zinapatikana.

Zaidi ya hayo wamewaomba wadau wa soka mkoani Arusha, kujitokeza katika kudhamini chochote katika timu hiyo ili kuwezesha kuwatangaza katika mikoa yote watakayocheza lengo ikiwa ni kutimiza azma yao ya kupanda hadi ligi daraja la kwanza.

Hayo yamejiri katika mkutano maalum wa wadau wa timu hiyo iliyofanyika hivi karibuni katika viwanja vya Sheik Amri Abeid uliokuwa na lengo la kujadili namna ya kuanza maandalizi ya ligi yao ya daraja la pili ikiwemo kufanya usajili, kutafuta kocha sambamba na benchi la ufundi na viongozi.

Katika mkutano huo uliohudhuriwa na wadau mbali mbali, Katibu Omari Kombo alisema kuwa hadi kumalizika kwa ligi timu inahitaji milioni 28 kwa ajili ya kugharamia usajili, malazi, usafiri pamoja na posho za wachezaji hivyo wadau watoe ushirikiano wao kuhakikisha hili linafanikiwa ikiwemo kutafuta wafadhili wa ndani na nje ya mkoa.

Katika mkutano huo wadau pia waliamua kuteua viongozi watakao isimamia timu hiyo hadi watakapo chagua viongozi wapya kwa mujibu wa katiba ya timu hiyo ambapo Abass Utanga alipewa nafasi ya mwenyekiti, Wille Mollel makam mwenyekiti, Salim Kombo katibu mkuu, Charles Mwaimu katibu msaidizi, Dr Kilavu mweka hazina.

Pia kamati ya usajili na ufundi walioteuliwa ni Denis Shemtoi, Denis Nyambele, John Change, Idd Mkulu, Azizi Nyoni, na Ally Wingi ambao Ndio watakao hakikisha AFC inakuwa katika hali ya ushidani zaidi ya msimu ulipita na kufanikiwa kupanda ligi daraja la kwanza.

SDL msimu wa 2015/2016, inayotarajia kuanza kutimua vumbi mwezi wa kumi tarehe 17 kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na TFF huku AFC ikiwa imepangwa kundi B pamoja na Alliance FC [Mwanza], Madini FC [Arusha], Bulyanhulu FC [Shinyanga], JKT Rwankome [Mara], na Pamba ya Mwanza.

Mwisho…………….