Bertha Mollel,
TIMU YA PANONE FC YA KILIMANJARO |
Ama kweli
timu ya Panone fc ya mkoani Kilimanjaro imepania kupanda daraja msimu ujao wa
ligi na hii ni baada ya Kocha wake mkuu Atuga Manyundo kuweka wazi ratiba ya
mazoezi yake ikiwemo wiki mbili za mwisho kucheza mechi za kirafiki na timu kubwa
za Simba, Mbeya city na Yanga.
Timu hiyo iliyoingia kambini kwa kujinoa ili kujiwinda na ligi daraja la kwanza msimu ujao chini ya kocha mkuu Manyundo alisema kuwa mara baada ya timu kuingia kambini yapo
mapungufu mengi wameyaona ikiwemo Ubutu wa nafasi ya mlinda mlango, fowadi na
kiungo hivyo kwa sasa anashauriana na benchi zima la ufundi kuanza usajili
mapema.
“Nimeona
nafasi butu ambazo nimekueleza ambazo kwa sasa tuko njiani kupiga hodi katika
sehemu mbali mbali kusaka wachezaji watakaojaza hizo nafasi na kuwa kali kweli
kweli lengo ni kutowaangusha wana Kilimanjaro katika msimu ujao lazima tupae
hadi ligi kuu”
“Ila kikubwa
kwa sasa ni kuwapa wachezaji waliopo mazoezi ya pumzi, kasi ya mpira na ukabaji
na baada ya hapo ratiba yetu inasema tucheze mechi za kirafiki na timu kubwa
kujua mapungufu, kama unavyojua sisi ni timu ya ligi kuu ijayo hivyo lazima
tucheze na timu za ligi kuu na kama unavyojua Simba na Yanga ndio chaguo letu
la kwanza”
“Ila kwa
sasa macho na masikio yetu ni kucheza na vilabu vya Mbeya city, vilabu vya hapa
Tanga kama Prison ili tujue wanavyocheza na sisi tujue mapengo yetu ni yapi na
kuyajaza mapema maana huu mwaka kwetu ni kazi tu hakuna kuremba” alisema Atuga”
Kwa upande
wake katibu mkuu wa kikosi hicho Augustino Mwakatumbula alisema kuwa
kutokupanda kwa timu hiyo hawatakuwa na sababu yoyote kutokana na tiyari
mazingira mazuri ya kupanda yamewekwa ikiwemo malazi, chakula na usafiri pamoja
na posho nzuri za wachezaji .
“Yaani mimi
niseme tu kuwa kama wachezaji wetu wasipotufurahisha kwa mwaka huu basi kwani
hawatakuwa na sababu yoyote ya msingi ya kushindwa kushinda kutokana na
mazingira mazuri tuliyowawekea na sasa tunaangalia kocha tu usajili anaoutaka
ndio tuufanye hadi kieleweke”
Mwisho…………………
No comments:
Post a Comment