HATIMAYE
kile kitendawili cha muda mrefu cha Nani ata twaa taji la Redds Miss
Tanzania 2012, kimeteguliwa usiku wa Novemba 3, 2012, baada ya Mrembo kutoka Kitongoji cha Sinza na Kanda
ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, Brigitte Alfred kutwaa taji hilo.
Brigitte
ambaye nyota yake katika mashindano hayo ya urembo nchini ilianza kung’aa tangu
Kitongoji cha Sinza baada ya kutwaa taji la Sinza na Baade kutwaa Taji la Redds
Miss Kinondoni amedhihirisha ukali wake baada ya kuwabwaga warembo wenzake 29
waliokuwa wakiwania taji hilo kutoka Kanda mbambali.
Mpinzani
mkubwa wa Brigitte katika shindano hilo alikuwa ni Mrembo kutoka Kanda ya Ziwa
ambaye nae alianza kuwika baada ya kutwaa taji la Redds Mkoa wa Mara na baade
kutwaa taji la Kanda ya Ziwa, Eugene Fabian.
Enagene
alifanikiwa kushika nafasi ya pili katika shindano hilo kubwa ambalo Brigitte
ameondoka akiendesha gari aina ya NOAH na kitita cha Shilingi Milioni 8.
Nafasi
ya tatu ilikwende kwa Malkia wa Kitongoji cha Kigamboni City na Miss Temeke
2012, Edda Sylvesta huku nafasi ya Nne ikichukuliwa na Mrembo wa Dar Indian
Ocean na Kinondoni, Magdalena Roy na nafasi ya Tano ikienda Kanda ya Ziwa tena
kwa Mkoa wa Mwanza, Happyness Daniel.
Brigitte Alfred akipunga mkono kwa furaha mara baada ya kutangazwa kuwa ndie mshindi na kuwabwaga washiriki wenzake 29. |
Mshindi
wa Taji la Redds Miss Tanzania 2012, Brigitte Alfred (katikati) akipunga mkono
kwa furaha katika picha ya pamoja na mshindi wa Pili, Eugene Fabian (kushoto)
na Mshindi wa Tatu, Edda Sylvester mara baada ya warembo hao kutangazwa kuwa
washindi wa shindano hilo. Brigitte anatokea Kitongoji cha Sinza na Kanda ya
Kinondoni wakati, Eugene anatoka Mkoa wa Mara na Kanda ya Ziwa huku Edda ni
Miss Kigamboni na Kanda ya Temeke, na picha ya chini ni washindi waliochukua nafasi tano
0 comments:
Post a Comment