Pages

Pages

Monday, August 25, 2014

J.K kutunuku kamisheni monduli


Rais Kikwete atunuku Kamisheni Kwa maofisa wapya wa Jeshi

Amiri Jeshi Mkuu,Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimpa zawadi na kumpongeza luteni Usu Mohamed Ramadhani Mgalawe baada ya kuibuka mwanafunzi bora wakati wa hafla ya kuwatunuku kamisheni maafisa wapya 179 wa jeshi la Wananchi waliohitimu vyema mafunzo yao katika chuo cha Jeshi Monduli Mkoani Arusha jumamosi.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitunuku kamisheni kwa maafisa wapya 179 wa jeshi waliohitimu vyema mafunzo yao ya muda mrefu katika chuo cha jeshi Monduli mkoani Arusha.
Maofisa wapya wa Jeshi wakila kiapo mbele ya Amiri jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa hafla ya kuwatunuku kamisheni iliyofanyika katika chuo cha jeshi kilichopo Monduli Mkoani Arusha .
Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na maofisa wapya wa jeshi baada ya kuwatunuku kamisheni katika sherehe zilizofanyika katika chuo cha jeshi Monduli mkoani Arusha.
Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza Luteni Usu Mohamed Ramadhani Mgalawe aliyeibuka mwanafunzi bora(Best Oficer Cadet Traineer Overall) wakati wa mafunzo ya muda mrefu ambapo maafisa 179 wa jeshi walihitimu vyema na kutunukiwa kamisheni katika chuocha jeshi Monduli .
Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na mwanafunzi Bora katika kozi ya muda mrefu ya jeshi Luteni Usu Mohamed Ramadhani Mgalawe(watatu kushoto) pamoja na wazazi wake muda mfupi baada ya Rais Kuwatunuku kamisheni maofisa 179 wa jeshi katika chuo cha Monduli Mkoani Arusha .
Mtoto mdogo akimsalimia Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete muda mfupi baada ya kumalizika kwa sherehe za kuwatunuku kamisheni Maofisa 179 wa jeshi katika chuo cha jeshi Monduli Mkoani Arusha. (picha na Freddy Maro)

Wednesday, August 20, 2014

NJIA YA MWANAMKE YA KUPUNGUZA UNENE WA TUMBO NA KUWA FLATI

Tumia salad yenye mchanganyiko wa nyanya, pilipili. Chkula chenye protini nyingi kinasaidia kuondoa njaa hivyo kupunguza mafuta mwilini.
LEO NI MAZOEZI YA YOGA.
Leo tunaendelea na mfululizo wa mazoezi ambayo yatakufanya wewe mwanadada uongeze urembo wako kwa kuondokana na tumbo kubwa lililojaa nyama-uzembe na mafuta ili uwe na tumbo flat.


Haina haja ya kutumia makemikali ambayo yatakuletea madhara hapo baadaye. 



Unachotakiwa kufanya ni mazoezi tu na kuzingatia maelekezo ili uyafanye mazoezi hayo kwa ustadi wa hali ya juu. unatakiwa kufanya mazoezi ya yoga. 


Mazoezi haya yatakusaidia kupata pumzi na kuimarisha misuli yako huku ukiondoa kiasi kikubwa cha mafuta mwili.
Kula chakula chenye protini
 

 
  Salad hiyo unaweza kuichanganya pia na matango.
chanzo: jumamtanda

Waandishi kortini kwa rushwa

WAANDISHI wawili wa habari wa Kampuni ya New Habari (2006), wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha wakikabiliwa na kosa la kupokea rushwa ya sh.150,000 kutoka kwa mmiliki na Chuo cha Savana Bridge, kilichopo jijini hapa.
Waandishi hao, Isack Longwe (28) mkazi wa Tegeta, Tanki bovu na Fredy Okoth (36) mkazi wa Kimanga Tabata jijini Dar es Salaam, wanadaiwa kushawishi kupatiwa sh. laki tatu ili waharakishe usajili wa chuo hicho kwenye Baraza la Taifa la Vyuo vya Ufundi (Nacte).
Walifikishwa mahakamani jana na kusomewa mashtaka  mawili ya kushawishi na kupokea rushwa na Mwanasheria wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (Takukuru), Vailet  Machali mbele ya Hakimu Mkazi, Rose Ngoka.
Alidai kuwa washtakiwa hao walikamatwa Agosti 16 mwaka huu mchana, baada ya kupokea kiasi hicho cha fedha ikiwa ni sehemu ya sh. 300,000 walizokuwa wameshawishi kupatiwa.
Akiwasomea maelezo ya kosa, Ngoka aliieleza mahakama hiyo kuwa washtakiwa wote kwa pamoja mnamo Agosti 14 mwaka huu, wakiwa Jiji la Arusha walimshawishi mmiliki ambaye pia ni Mkuu wa chuo hicho, Mselemu Kombe kuwapatia sh. 300,000, ili wakaharakishe usajili wake Nacte.
Katika shtaka la pili, washtakiwa hao walidaiwa kuwa Agosti 16 mwaka huu, majira ya mchana, walipokea rushwa ya sh.150,000 toka kwa Mselemu kwa lengo hilohilo.
Ngoka alidai kuwa washitakiwa hao walifanya makosa hayo huku wakijua wao kama waandishi wa habari hawawezi kufanya shughuli za usajili wa chuo.
Hadi Tanzania Daima linaondoka mahakamani hapo, waandishi hao walikuwa rumande ya mahakamani hapo wakisubiri kupata wadhamini wawili wenye vitambulisho na mali isiyohamishika yenye thamani ya sh. milioni moja, vinginevyo wangepelekwa gereza la Kisongo hadi Septemba 2, mwaka huu, shauri hilo litakaporudi kwa ajili ya kutajwa.

chanzo tz daima

Friday, August 15, 2014

Azam ni moto wa kuotea umbali


Mashindano ya vilabu bingwa Afrika Mashariki na Kati maarufu kama kombe la Kagame yanaendelea mjini Kigali.

Timu ya Azam Fc ya Tanzania ni moto wa kuotea mbali hasa baada ya kuweka nguvu zake kubwa katika kuhakikisha anabaki juu baada ya jana kukataa kufungwa na kutoka sare ya kufungana magoli 2 na Atlabara ya Sudan Kusini katika katika mashindano ya kombe la Kagame .
Mechi ilichezwa katika uwanja wa Nyamirambo jijini Kigali.
Azam wameongoza mchezo na kumaliza kipindi cha kwanza wakiwa mbele kwa goli 1 lililotiwa kimiani na mshambuliaji Borou kunako dakika ya 44.
Goli hilo lilikombolewa na mshambuliaji Thomas kunako dakika ya 48 kabla ya Martin Bonny kufunga goli la pili la Atlabara kunako dakika ya 54
Azam imesubiri dakika ya 85 kumuona mshambuliaji wake Kavumbagu akirudishia matumaini ya angalau kupata alama moja.
AZAM inaongoza kundi la A ikiwa na alama 5 ikifwatiwa na Rayon Sport ya Rwanda yenye alama 4.
Mechi iliyotangulia imeshuhudia sare ya goli moja kati ya timu ya Adama City ya Ethiopia na KMKM ya Zanzibar.
Goli hilo lilifungwa kimiani na mshambuliaji Wendesoni Mishido kunako dakika ya 60 ya mchezo.
Matumaini ya Adam City kusonga mbele yakazimwa na Juma Faki aliyekomboa goli hilo kunako dakika ya mwisho.
Kesho pia zitachezwa mechi mbili KCCA ya Uganda itamenyana na Atletico ya Burundi huku APR ya Rwanda ikizipiga na Telecom ya Djibuti.
Police FC ya Rwanda ndiyo timu pekee iliyokwisha jihakikishia tiketi ya kufuzu katika robo fainali hata kabla ya mechi za mchujo kumalizika.

Basi la TFF lakamatwa Kenya


Basi la wachezaji wa soka Tanzania  lakamatwa ili kulipa madeni

Basi la wachezaji wa timu ya taifa ya Tanzania, limekamatwa kwa amri ya mahakama kutokana na deni la shilingi milioni 140 (zaidi ya dola 85,000), ambalo kampuni ya Punchline kutoka Kenya, inadaiwa kulidai shirikisho la kabumbu Tanzania (TFF).
Madalali ndiyo walilikamata basi hilo likiwa kama dhamana huku TFF ikitakiwa kulipa deni husika kabla ya kurejeshewa mali zao.
Msemaji wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniface Wambura, amesema tayari wamelipa shilingi millioni 70 ikiwa ni malipo ya awali.
Deni hilo linatokana na gharama za uchapishaji tiketi za kuingilia uwanjani katika mechi za ligi kuu ya Tanzania tangu mwaka 1997.
TFF kwa sasa iko katika mpango wa kuuza tiketi za uwanjani kwa njia ya ki-eletroniki (umeme) ikiwa ni sehemu ya jitihada ya kupunguza adha kwa wapenzi wa soka na kudhibiti wizi na ulanguzi wa tiketi.
Wambura amesema jitihada zinafanyika kumaliza deni hilo, ila TFF italifuatilia kwa umakini na kuchunguza mwenendo mzima uliosababisha kuwepo deni hilo.

chanzo"bbc

Thursday, August 14, 2014

SHIRIKA YA MOSHI MABINGWA WA MAVETERANI ARUSHA


timu ya maveterani ya Kivale fc ya jijini Dar (wenye jezi ya blue) wakichuana vikali na timu ya Ushirika ya Moshi (wenye njano) kwenye fainali ya bonanza la maveterani iliyofanyika katika uwanja wa sheik Amri Abeid ya ARUSHA
 
Na Bertha Ismail - Arusha

Timu ya Ushirika ya mjini Moshi imefanikwa kuwa washindi katika bonanza la maveterani baada ya kuichapa timu ya Kivule ya jijini Dar- es-salaam kwa magoli 2-0 katika uwanja wa Sheik Amri Abeid ya jijini Arusha.

Bonanza hilo lililoandaliwa na timu ya maveterani ya jijini Arusha “All Stars” lilihudhuriwa na timu sita za maveterani kutoka mikoa mbalimbali ya hapa nchini ambapo walishindana katika kusakata soka huku wenyeji Arusha wakionekana kutamba dakika za awali na baadae kuzidiwa nguvu na timu za wageni na kuzima ndoto za kutwaa ubingwa.

Katika bonanza hilo, timu za maveterani zilizokuwa kundi ‘A’ ni pamoja na timu ya Mwanza Veterani “Mwanza starehe”, Dar-es-salaam “Kivule” pamoja na Dodoma Veterani, huku zilizokuwa kundi ‘B’ ni pamoja na Arusha All Stars, Ushirika na Namanga Veterani.
Michuano hiyo iliyokuwa ikichezwa kwa dakika 30 ilifunguliwa dimba na wenyeji, Arusha all stars na Namanga ambapo timu ya Arusha ilifanikiwa kuichapa Namanga kwa magoli 2-0, mechi iliyofuatiwa na timu ya Kivule ya Jijini Dar na kuichapa Dodoma Veterani kwa goli 1-0.
Timu ya Namanga ilizidi kuonewa baada ya kushuka dimbani na timu ya Ushirika ya Moshi na kugaragazwa 1-0, ambapo Timu ya Dodoma walitoshana nguvu na timu ya Mwanza Veterani baada ya kumaliza mchuano bila kufungana, na baada ya mchuano huo timu ya Arusha all Stars ilishuka dimbani tena kuminyana na timu ya Ushirika ya Moshi lakini wenyeji hao walionekana kuzidiwa nguvu na majirani zao baada ya kufungwa goli 1-0.
Baada ya michuano hiyo kila kundi lilitoa mshindi, ambao ni Arusha All Stars pamoja na Mwanza Starehe na kushuka dimbani ambapo Arusha ilifanikiwa kuichapa Mwanza 1-0, huku Kivule ya Dar-es-salaam ikishuka Dimbani na timu ya Ushirika ya Mjini Moshi ambapo Kivule ilizidiwa nguvu dakika za mwisho na kuchapwa magoli 2-0 mfululizo.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa waandaji wa bonanza hilo, Laurence Sabuni, alisema kuwa kufuatia ushindi huo wa Timu ya Ushirika ya Moshi itazawadiwa kikombe kikubwa huku mshindi wa pili ambae ni Kivule ya jijini Dar-es-salaam ikizawadiwa kikombe kidogo ambazo hata hivyo hadi bonanza linafikia tamati majira ya saa 12:30 jioni vikombe hivyo havikuwasili eneo la tukio.
Wakizungumzia Matokeo hayo, Tumaini Andrew wa timu ya Ushirika Pamoja na Joseph Mbewa wa timu ya Kivule ya Dar walisema kuwa matokea hayo ni ya haki wala hakuna wa kumlaumu kwani katika mashindano yeyote ile kuzidiana kupo hivyo kutumia udhaifu wa mwenzio kupata ushindi ni sawa zaidi kuliko kutumia ubabe kununua ushindi.
Aidha bonanza hilo la maveterani hufanyika kila mwaka mwezi wa nane kwa kuzunguka mikoa mbalimbali kwa lengo la kuwaenzi maveterani watatu (Francis Lungu, Judicate Estomili, Amani Mwalim) wa timu ya All stars waliofariki mwaka 1999 kwa ajali mbaya ya gari eneo la Mwanga mkoani Kilimanjaro walipokuwa wakitokea jijini Dar-es-salaam kwenye mashindano ya maveterani wa mikoa mbalimbali hapa nchini na wengi kujeruhiwa.
Mwisho……..
 
 

Tuesday, August 12, 2014

VILABU SABA VYA GOFU KUKUTANA TANZANIA OPEN K-VANT GIN GOLF CO-OPERATE TOURNAMENT 2014.

Makamu Mwenyekiti wa klabu ya Gofu ya Moshi ,Christopher Martin  maarufu kama "Mbe"akizungumzia Mashindano ya mchezo wa Gofu ya Tanzania Open K-Vant Gin Golf Co-operate Tournament 2014 yatakayofanyika Agosti 16 na 17 mwaka huu.
Meneja Mauzo wa Kanda ya Kaskazini wa kampuni ya Megatrade Investment Ltd ya jijini Arusha Edmund Rutaraka akizungumzia udhamini wao katika Mashindano ya Gofu ya Tanzania Open K-Vant Gin Golf Co-operate Tournam2014   ent .
Makamu Mwenyekiti wa klabu ya Gofu ya Moshi ,Christopher Martin  maarufu kama "Mbe"akihakiki hundi kabla ya kukabidhiwa rasmi.
Meneja Mauzo wa Kanda ya Kaskazini wa kampuni ya Megatrade Investment Ltd ya jijini Arusha Edmund Rutaraka akikabidhi hundi ya kiasi cha shilingi milioni 3.5kwa Makamu mwenyekiti wa klabu ya Gofu ya Moshi ,Chris Martin  ikiwa ni sehemu ya udhamini katika Mashindano ya Gofu ya Tanzania Open K-Vant Gin Golf Co-operate Tournament 2014.   .
Makamu mwenyekiti wa klabu ya Gofu ya Moshi ,Chris Martin  akikabidhi hundi iliyotolewa na kampuni ya Megatrade kwa katibu wa klabu ya Gofu ya Moshi Mohamed Nkya.
Viongozi wa Kabu ya Gofo ya Moshi wakiwa katika picha ya pamoja na Staff wa kampuni ya Megatrade muda mfupi baada ya kukabidhi hundi ya kiasi cha shilingi milioni 3.5.
Makamu mwenyekiti wa klabu ya Gofu ya Moshi ,Chris Martin akimuonesha uwanja utakaotumika kwa mashindano hayo Meneja Mauzo wa kampuni ya Megatrade Investment Ltd kanda ya kaskazini ,Edmund Rutaraka      chanzo libeneke 

UNESCO KUPITIA READ INTERNATIONAL WATOA MSAADA WA VITABU VYA SAYANSI KWA SHULE YA SEKONDARI MWEDO ARUMERU


DSC_0019
Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph akipolewa na Mwalimu wa Taalum na msimamizi wa Maktaba wa Shule ya wasichana ya Mwedo, Joseph Mangomes alipofika shuleni hapo kukabidhi msaada wa vitabu vya masomo ya Sayansi uliotolewa na Shirika la Read International kupitia UNESCO.
Na Mwandishi wetu, Arumeru
Wanafunzi wa shule ya Mwedo sekondari iliyopo wilayani Arumeru wamelishukuru Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kupitia Read International la nchini Uingereza kwa kuweza kuwapatia vitabu vya kiada vya masomo ya Sayansi hali itakayowafanya kupiga hatua katika masomo hayo.
Akizungumza kwa niaba ya wanafunzi hao Kaimu mkuu wa shule hiyo Clara Meijo alisema kuwa kutokana na changamoto mbalimbali za masomo ya Sayansi wanalishukuru Shirika la Read International kwa kuweza kuwapatia vitabu hivyo tulivookabidhiwa na UNESCO.
Meijo alisema kuwa shule hiyo ilianzishwa mwaka 2011 ikiwashirikisha wasichana wa kimasai wanaoishi katika mazingira magumu wakiwa ni wanafunzi waliokosa nafasi ya kupata elimu kwa kuwachukua wanafunzi kutoka maeneo mbalimbali kwenye jamii ya kifugaji.
DSC_0026
Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph (kulia) akisalimiana na Mwalimu Clara Meijo mara baada ya kuwasili shuleni hapo.
Aidha alisema kuwa wanafunzi hao ni wale waliokuwa kwenye maeneo ambayo upatikanaji wa elimu yalikuwa mbali, shule hiyo inayomilikiwa na Shirika la Wanawake wa Kimasai (MWEDO) lenye makao makuu yake jijini Arusha huku shule hiyo ikiwa imejengwa kwa michango mbalimbali ya wafugaji kwa kutoa mifugo yao.
“Changamoto kubwa inayoikabili shule yetu ni upungufu wa mabweni, maji na umeme wa kudumu ikisababisha wanafunzi kushindwa kujianda kwa mitihani yao kwa kujisomea nyakati za usiku hali inayoangusha ufaulu kwa wanafunzi hao” alisema Meijo.
Ameiomba Serikali na wafadhili kuwasaidia kupata umeme kwa haraka ilikuweza kuongeza ufaulu na idadi ya wanafunzi huku akiomba pia kusaidiwa upatikanaji wa maji safi kwenye shule hiyo na kuongeza kuwa msaada huo wa vitabu umekuja wakati muafaka kwao na utasaidia kukua kwa ufaulu shuleni hapo.
DSC_0037
Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph akisaini kitabu cha wageni shuleni hapo. Kulia ni Afisa Mradi wa uchumi wa kijani ndani ya hifadhi hai (GEBR) Kitengo cha Sayansi kutoka UNESCO na mwakilishi wa KOICA, Myoung Su Ko aliyeambatana na Bw. Al Amin.
Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph alisema kuwa wanaimani kubwa kuwa vitabu hivyo vitatumika kuongeza uelewa kwa wanafunzi na kuwa vitabu hivyo vinatambuliwa na Wizara ya Elimu katika kufundishia masomo ya Sayansi hivyo ni wajibu wenu kama wanafunzi kujifunza kwa bidiii ili muwe mabalozi wazuri katika ujenzi wa taifa.
Bw. Al Amin aliongeza kuwa wanampango wa kuiboresha maktaba ya shule hiyo kwa kuongeza matumizi ya Tehama kwa upatikanaji wa taarifa mbalimbali kwa ajili ya masomo.
Shule hiyo inawafanyakazi 18 wakiwemo walimu kumi na idadi ya wanafunzi wakiwa 153 huku wanafunzi kumi ni wakutwa na waliobakia ni wa bweni.
DSC_0041
Afisa Miradi Kitengo cha Sayansi kutoka UNESCO na mwakilishi wa KOICA, Myoung Su Ko akisaini kitabu cha wageni shule ya sekondari ya wasichana ya Mwedo iliyopo wilayani Arumeru jijini Arusha.
DSC_0057
Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph (kulia) akizungumza na Mwalimu wa Taalum na msimamizi wa Maktaba wa Shule ya wasichana ya Mwedo, Joseph Mangomes (wa pili kulia) wakati akikagua maktaba ya shule hiyo kabla ya kukabidhi msaada wa vitabu vya masomo ya sayansi vilivyotolea na Shirika la Read International kupitia UNESCO. Kutoka kushoto ni Mwalimu Clara Meijo, Afisa Mradi wa Shirika la Wanawake wa Kimasai (MWEDO) liliojenga shule hiyo Martha Sengeruan na Afisa Miradi Kitengo cha Sayansi kutoka UNESCO na mwakilishi wa KOICA, Myoung Su Ko.
DSC_0065
Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph akitoa maelekezo ya namna ya upangiliaji wa vitabu kwenye maktaba hiyo kwa Mwalimu wa Taalum na msimamizi wa Maktaba wa Shule ya wasichana ya Mwedo, Joseph Mangomes.
DSC_0162
DSC_0101
Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph (wa pili kulia) akipitia rekodi za uhifadhi wa maktaba hiyo kabla ya kuwaahidi kuleta Kompyuta itakayokuwa "Software" ya kisasa zaidi na kuweza kuwarahisisha kuhifadhi na utunzaji wa kumbukumbu za maktaba hiyo.
DSC_0141
Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph (kulia) akisikiliza maelezo ya mwanafunzi Evaline Gerald wa kidato cha pili shuleni ya sekondari ya wasichana MWEDO anayesaidiana na Mwalimu wake katika kutoa huduma za maktaba ya shuleni hapo.
DSC_0129
Sehemu ya mashelfu ya kuhifadhia vitabu kwenye maktaba ya shule hiyo.
DSC_0386
Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph (kulia) na fisa Miradi Kitengo cha Sayansi kutoka UNESCO na mwakilishi wa KOICA, Myoung Su Ko wakipata maelezo ya maabara ya shule y sekondari ya wasichana MWEDO kutoka kwa Mkuu wa kitengo cha Sayansi shuleni hapo Bw. Edickiel Mturi.
DSC_0231
Mwalimu wa Taalum na msimamizi wa Maktaba wa Shule ya wasichana ya Mwedo, Joseph Mangomes akiutambulisha ugeni wa UNESCO kwa wanafunzi na walimu wa shule ya sekondari ya wasichana MWEDO wakati wa hafla ya kukabidhi msaada wa vitabu shuleni hapo.
DSC_0248
Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph, akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari ya wasichana ya MWEDO wakati wa halfa ya kukabidhi vitabu vilivyotolewa na Shirika la Read International kupitia UNESCO ambao aliwaasa wanafunzi hao kusoma kwa bidii kuweza kukomboa familia zaidi hapo baadae kupitia elimu.
DSC_0308
Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph akionyesha baadhi ya vitabu vya masomo ya sayansi vilivyotolewa na Shirika la Read International kupitia UNESCO. Kulia ni Afisa Miradi Kitengo cha Sayansi kutoka UNESCO na mwakilishi wa KOICA, Myoung Su Ko.
DSC_0313
Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph, akikabidhi sehemu ya msaada wa vitabu vya masomo ya sayansi kwa Mwanafunzi Evaline Gerald wa kidato cha pili shule ya sekondari ya wasichana MWEDO uliotolewa na Shirika la Read International kupitia UNESCO. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Afisa Miradi Kitengo cha Sayansi kutoka UNESCO na mwakilishi wa KOICA, Myoung Su Ko (kulia) na kushoto ni Afisa Mradi wa Shirika la Wanawake wa Kimasai (MWEDO) liliojenga shule hiyo, Martha Sengeruan.
DSC_0315
Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph, Walimu na Wanafunzi wa shule hiyo wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kukabidhiwa msaada wa vitabu vya masomo ya sayansi vilivyotolewa na Shirika la Read International kupitia UNESCO.
DSC_0332   DSC_0356
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari ya wasichana ya MWEDO wakishusha maboksi yaliyosheheni vitabu vya masomo ya sanyansi vilivyotolewa na Shirika la Read International kupitia UNESCO.
 
chanzo ; libeneke

Sunday, August 10, 2014

Wanawake wa Arusha wako hatarini


Wanawake wanaoendesha magari katika Jiji la Arusha, wamekumbwa na hofu kutokana na kuibuka watu  wasiojukikana ambao wanawashambulia kwa risasi.
Washambuliaji hao ambao hutumia pikipiki, katika siku saba wamemuua mwanamke mmoja na kuwajeruhi wanne kwenye matukio tofauti lakini bila kuiba chochote.
Mwanamke aliyeuawa ni Shamim Rashid, mkazi wa Sakina baada ya kupigwa risasi alipokuwa akijiandaa kuingia nyumbani kwake juzi , tukio ambalo limekuja takriban siku tatu tangu mwanamke mwingine, Frola Porokwa kunusurika kifo.
Porokwa mke wa mkurugenzi wa Shirika la Pingos a Forums, Edward Porokwa, alipigwa risasi akiwa jirani kuingia nyumbani kwake kwake pia eneo la Sakina, iliyompata pembeni ya kifua na kutokea mgongoni.
Katika matukio yote mawili, watuhumiwa hao hawakupora chochote huku wakitoweka na pikipiki zao aina ya boxer .
Wakizungumza na mwananchi Juzi katika msiba wa Shamin, baadhi ya waombolezaji walitaka Jeshi la Polisi kuimarisha uchunguzi juu ya matukio hayo.
“ Tunaimani na jeshi letu litawakamata wahusika, lakini jambo hili linatutia hofu wanawake kuendesha magari usiku,”alisema Khanifa Haji.
Kufuatia matukio hayo Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha, limeanza msako mkali dhidi ya watuhumiwa hao.
Kamanda wa Polisi mkoani Arusha, Liberatus Sabas alisema katika kukabiliana na uhalifu huo  jeshi lake , Serikali kwa kushirikiana na wadau wataweka Kamera maalumu zenye uwezo za kubaini vitendo viovu kwenye sehemu mbalimbali ili iwe rahisi kuwakamata wahusika.
“Msako mkali umeanza na tuna uhakika wa kuwakamata watuhumiwa hawa na wengine,”alisema.
Wakati huo huo, polisi imefanikiwa  kumkamata Adam Mussa Pakasi mkazi wa Siwandeti wilayani Arumeru akiwa na  bunduki iliyotengenezwa kienyeji inayotumia risasi za Shotgun,risasi 38 na ganda moja la risasi iliyotumika pamoja na mafuta ya kusafishia bunduki.
Sabas alisema matukio ya uhalifu yanayohusiana na kupotea kwa maisha ya watu ni miongoni mwa mambo nyeti yanayochunguzwa kwa umakini na tahadhari.