Historia
fupi sana ya Maisha yangu.
bertha ismail |
Mimi Bertha
Ismail mwandishi wa habari wa kampuni ya MCL Tanzania, pia ni mkurugenzi wa
kampuni ya BIMO Media information iliyoko Arusha, nilizaliwa tarehe 6-12- 1990 eneo la Ilboru
jijini Arusha na kwa sasa naishi Kijenge juu.
happy birthday yangi ni decemba 6, |
Nilianza
elimu yangu ya msingi katika shule ya Olturoto iliyoko wilayani Arumeru mkoani
Arusha mwaka 1999, nilihama shule hiyo mwaka 2001 baada ya wazazi wangu waliokuwa
wananilea kutengana.
Mwaka 2002
nilihamia shule ya msingi Unga ltd na kuingia darasa la Tatu hadi nilipohitimu
elimu yangu ya msingi hapo mwaka 2005.
Nilifaulu
kuendelea na elimu yangu ya sekondari katika shule ya sekondari ya Kinana mwaka
2006 na kuhitimu elimu hiyo mwaka 2009.
Hata hivyo
kutokana na ugumu wa maisha na malezi ya kuishi na mzazi wa kambo (baba)
sikufanikiwa kuendelea na elimu ya kidato cha tano badala yake nilitafuta chuo
cha kusoma.
Kwa kuwa
tangu nikiwa mdogo nilipenda kazi ya Utangazaji sikuwa na chaguo lingine zaidi
ya kuomba wazazi wangu waliokuwa wananilea kulipiwa ada ya kwenda chuo cha
Uandishi wa habari na Utangazaji.
nimemaliza chuo naingia mtaani |
Katika
kipindi hicho chote sikuwa namjua wala kumfaham baba yangu mzazi ni yupi bali
nilijua ni yule wa awali niliyekuwa namuona tangu nakua na baadae kuja
kutengana na mama yangu na kuhama kijiji cha Olturoto na baadae alifariki hivyo
nilijua ni baba yangu ndie aliyefariki na kuondoa matumaini ya kuja kuonana na
baba yangu tena.
Kama
ijulikanavyo maisha ya mzazi wa kambo mambo yalikuwa magumu sana hasa katika
kukubalika katika mahitaji yangu mbele ya baba wa kambo hali iliyoleta ugomvi
mkubwa kati ya baba yangu na mama yangu lakini kiubishi-ubishi niliamua kwenda
kuchukua fom na kujiunga na chuo bila ada.
Kwa kutumia
uongo uongo siku moja moja baba akisafiri mama huwa rafiki yetu hivyo nilitumia
mda huo kutoa mahitaji yangu na mama kutimiza ambapo ada ya awali ililipwa na
kuanza chuo hivyo angalau kuaminika lakini mambo yalienda hivyo hivyo kipindi
ambacho mama hanielewi nililazimu kutumia uongo shuleni hadi kuhitimu masomo
yangu ya cheti katika chuo cha Uandishi wa habari na Utangazaji Arusha (AJTC).
Ingawa
nilikuwa na madeni na siku ya mitihani wanafunzi hawakuruhusiwa kufanya
mitihani ya kumaliza chuo bila ada hivyo ilibidi nidanganye kadri nilivyoweza
hadi kuruhusiwa kufanya mitihani na kuingia mitaani kuanza kutafuta habari na
kuripoti redio five Arusha ambayo ilinisaidia kuanza kupata fedha kidogo kidogo
ambazo nilipeleka shule kupunguza deni la Ada.
Katika
kipindi hicho nilianza kusikia fununu kuwa baba yangu mzazi yupo hai na anaishi
hapa Arusha hali ambayo sikuamini hadi nilipomuona ambapo nilitaka kujua
historia ya kwanini hakutaka kunijua mwanae katika kipindi hicho chote cha
mateso na mahangaiko lakini haikuzaa matunda ya kufahamu historia kamili bali
fununu za mtaani.
Baada ya mda
kidogo baba wa kambo akawa hataki nifanye kazi hali iliyopelekea kunifukuza
nyumbani endapo nitaendelea na kufanya kazi kwa madai kuwa haoni faida ya kazi
yangu, hivyo niliamua kutorokea kwa baba yangu mzazi ambapo hata huko nako
mambo hayakuwa shwari kwa mama yangu wa kambo hali iliyopekekea mimi kutafuta
namna ya kuanza maisha ya kupanga nyumba.
Kwa kutumia
vijisent nilivyokuwa Napata katika kazi yangu ya kutafuta habari niliweza
kupanga chumba cha udongo mwaka 2010 na kuanza maisha ambayo hata sikujua
niyaendesheje.
Kwa bahati
mbaya mkosi nao haukuniacha nyuma bali uliendelea kuniandama ambapo baada ya
mda kulitokea maneno ya uongo katika ofisi hizo za Redio 5 Arusha kwa
kuhujumiwa na hatimaye bila kusikilizwa niliamuliwa kufukuzwa kazi, kiukweli
iliniuma lakini sikuwa na la kufanya.
Nilianza
kusaka kazi kwa mara nyingine na Mungu nae hakuwa nyuma sana kunivuta mkono
nilipopata tatizo, kwani nilibahatika kupata kazi katika kituo cha redio ya
sunrise Arusha kama mtangazaji na mwandishi na baada ya mda nikawa naandika gazeti pia moja lililoanzishwa
na aliyekuwa mtangazaji wa star TV,
Anjelo Mwoleka liitwalo “kutoka Arusha” hali iliyonifanya niwe mwandishi mzuri
hapa jijini Arusha.
Baada ya mafanikio
hayo na kumaliza deni hilo niliamua kujiandikisha shule na kuendelea na elimu
yangu ya diploma ya uandishi wa habari na utangazaji Arusha huku maisha yangu
mapya niliyoyaanzisha yakiwa mazuri kila kukicha kwani nilifanikiwa kumiliki
godoro, kitanda. Na hata meza moja niliyokuwa naweka begi langu la nguo n.k.
Baada ya mda
niliamua kuachana na utangazaji wa sunrise radio na kuhamia moja kwa moja
gazeti hilo la kutoka Arusha ambapo hata hivyo baadae lilikuja kufa bila
kuzikwa.
Mwaka 2013
nilihamia gazeti la “Tanzania Daima”
kama mwandishi wa michezo wa kujitegemea huku nikiwa nimeachana na redio
sunrise kabisa.
Kama
ijulikanavyo mwandishi wa kujitegemea ni kama mchezaji wa timu kubwa duniani, mwaka
2014 nilibahatika kununuliwa na kampuni ya “Mwananchi Communication Ltd” (MCL).
Kama mwandishi wa michezo katika gazeti la mwanaspoti ambapo pia habari zangu kwa sasa zinatumika
hadi gazeti la Mwananchi na “the citizen”.
Pia mwezi wa
11 mwaka 2014 ni kuhitimu elimu yangu ya Diploma ya chuo cha uandhishi wa
habari na utangazaji.
Kwa sasa
mbali na uandishi pia nimesajili kampuni yangu kwa kutumia jila langu la “BIMO
Media company” ambayo inajihusisha na kuandaa na kuratibu matukio mbali mbali
ikiwemo la “shindano la uandishi wa insha kuhusu maswala ya utalii” pia
matamasha na shoo mbali mbali za wasanii.
moja ya tuki la uandaaji wa tukio la uanshi wa insha iliyoandaliwa na kampuni ya BIMO Media information, hapa nikisoma risala mbele ya mdeni rasmi. |
Mungu
ameonekana kunipigania kila kukicha na kamwe sitasahau nilikotoka katika maisha
yangu ambapo mbali na kuwa nina baba lakini bado sioni kama ninae bali ninae
mama pekee ambae kwa sasa ameshaachana na baba yetu wa kambo na anafanya
biashara zake katika vibanda vya soko kuu Arusha na mahusiano yetu kwa sasa ni
kama mtu na rafiki yake siyo mtu na mzazi wake tena.
nikisindikiza moja ya wageni kama mkurugenzi wa kampuni kwenye tukio la ushindani wa uandishi wa insha |
Naomba niwatie moyo watu wanaopitia magumu katika maisha yao kuwa Mungu yupo na anatenda hivyo kila mtu amtegemee yeye na kumuangalia kwa macho yote mawili kwani anatenda.
E-
mail berthaarusha@gmail.com mediabimo@gmail.com
Mwisho……………
0 comments:
Post a Comment