Pages

Pages

Thursday, March 26, 2015

kigogo wa simba UKAWA lanaswa ndani ya jengo la wana jangwani

MFUASI wa kundi la ‘Simba Ukawa’, wapinzani wa uongozi wa SImba SC chini ya Rais Evans Aveva, Hassan Msumari jana amenusurika kupigwa, baada ya kuvamia makao makuu ya klabu ya wapinzani, Yanga SC.
Msumari aliyewahi kuwa Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Chama cha Soka Temeke (TEFA), aliingia makao ya Yanga SC, makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari.
Hata hivyo, baadhi ya wanachama wakamshitukia na kumripoti, ndipo kundi la wanachama wachache wa klabu hiyo waliokuwapo klabuni lilipomvania kutaka kumpiga
Kulia Msumari anapandishwa kwenye karandinga, kushoto ameshapatiwa siti kwenye gari hilo
Hassan Msumari akitolewa na Polisi makao makuu ya Yanga SC mchana wa jana

Hata hivyo, busara ikatumika na kumuweka chini ya ulinzi kabla ya kupiga simu Polisi kumripoti. Baada ya dakika 20, Polisi walifika eneo la tukio na kumtia nguvuni Msumari na kuondoka naye kuelekea kiruo cha Polisi Msimbazi.
Katika maelezo yake ya awali wakati amepewa kibano na makomandoo wa Yanga SC, Msumari alisema kwamba aifika hapo kwa ajili ya kuwafuata Waandishi wa Habari ili azungumze nao.
Na akakiri ni mwanachama wa Simba mwenye kadi namba 4041 akitoka tawi la Tandika, na kwa sasa yeye ni Simba Ukawa, kikundi kinachoupinga uongozi uliopo madarakani.

Bunge la Tanzania laondoa adhabu ya kifo kwa wanaokutwa na dawa za kulevya

BUNGE limepitisha rasmi Muswada wa Sheria ya Udhibiti wa Dawa za Kulevya wa mwaka 2014, huku adhabu ya kifo kwa watakaokutwa na dawa hizo, ikishindikana kuingizwa kwenye muswada huo, isipokuwa mapapa na vigogo wa biashara hiyo, wameongezewa adhabu ya faini ya Sh bilioni moja na kifungo cha maisha.

Hata hivyo, baadhi ya wabunge bado wameendelea kung’ang’ania kuwa sheria hiyo ijumuishe adhabu hiyo kali ya kifo kwa wafanyabiashara, mapapa au vigogo wanofadhili biashara hiyo, kwa kuwa madhara ya dawa hizo ni makubwa na yanaathiri zaidi vijana ambao ni nguvukazi ya nchi.

Akitoa majumuisho ya michango ya wabunge kuhusu hoja ya muswada huo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge, Jenista Mhagama, alisema adhabu ya kifo haiwezekani kuingizwa kwenye sheria hiyo, kwa kuwa adhabu hiyo nchini iko kwenye makosa mawili pekee.

“Ni kweli Tanzania ni miongoni mwa nchi ambazo bado zinatoa adhabu ya kifo, lakini kwa mujibu wa sera iliyopo, adhabu ya kifo imeingizwa na kubainishwa kwenye makosa ya uhaini na mauaji pekee,” alisema Mhagama.

Makamba aendeleza majibizano na Lowassa


"Hapo juzi Niliandika katika mitandao ya kijamii hasa nikizungumzia mchezo mchafu wa kisiasa unaofanywa na kambi ya ndugu EDWARD NGOYAI LOWASA. na nipende kurudia tena kuita kwamba anachoendelea kufanywa na edward lowasa kuwahadaa wananchi watanzania sasa aone kwamba tunatambua mbinu hizo chafu.\

Ndugu zangu watanzania baada yangu kuyasema haya edward ngoyai lowasa ameendelea kujitetea hasa akiandika katika ukurasa wake ya twiter na magazeti akisema amenipuuza sababu ya pili akisema mmi ni mchanga natakiwa niendelee kulelewa nikue, Naomba kumwambia lowasa udogo wangu mmi si katika Ukombozi wa maslahi ya Watanzania ila kama kweli Nitakuwa mchanga basi uchanga wangu nauona katika Kutokuwa mchafu, Mla rushwa, Mlaghai,Asiyewahadaa watanzania kwa mwamvuli wa dini,Lakini mwisho uchanga wangu ni kutowapikia ubwabwa washabiki wa siasa za Kumsafisha aliye mchafu.

Hayo niliyotaja tu ndio niko mchanga bado na kwa hayo edward ni mkongwe kupitiliza.
Mwisho namshauri edward aache maigizo na taifa hili watanzania wanahitaji kiongozi muadilifu na si anayewapa ubwabwa na kuwatumia basi kuja kwake wakiwa hawajashika tiketi za gari waliyosafiri nayo."
January Makamba.

Nkamia atakiwa kuzungumza kiuhalisia

Arusha

Wadau wa michezo mkoani Arusha wamemtaka Naibu Waziri wa Vijana Utamaduni na Michezo atembelee na kukagua uwanja wa Sheikh Amri Abeid ajionee jinsi ulivyo katika hali mbaya kiasi cha kutokuwa katika hadhi ya kuchezewa hata mashindano ya mchangani.

Kauli ya wadau imekuja baada ya Naibu Waziri Juma Mkamia kutoa kauli kuwa uwanja wa Sheikh Amri Abeid ni katika viwanja bora vinavyotambulika na shirikisho la mpira Afrika (CAF) na unaweza kutumika na michezo ya kimataifa, kauli iliyopingwa vikali.


Viongozi wa vilabu, wachezaji na hata wadau wa soka wameshangazwa na kauli ya Mkamia na kuonyesha wasiwasi kuwa Waziri huyo hajawahi kuutembelea na kuujuwa vema uwanja huo  kwa kuukagua uwanja na miundo mbinu yake.                                                          

Eliapenda Zambia ni Mkurugenzi wa Taasisi ya michezo ya TACODA alisema kuwa hali ya uwanja ni mbaya mno kiasi kwamba ni bora kucheza katika viwanja vya mchangani kuliko uwanja wa Sheikh Amri Abeid uliotawaliwa na mashimo, vichuguu, milima na mabonde huku vyoo vikiwa tatizo.

Juu ya miundombinu ya uwanja huo pamoja na uwepo na maji ya kutosha lakini hakuna vyoo vya watazamaji na vya wachezaji vikiwa vichafu na kuweka hali ya ukungu huku baadhi ya vyumba vya choo vikigeuzwa maduka na kupangisha wafanyabiashara na kuwa sehemu ya mapato ya CCM wenye uwanja.                                                                                            
Aidha suala hilo liliwahi kupigiwa kelele na wasimamizi wa vituo vya  ligi ya Vodacom, Daraja la kwanza na viongozi wa chama cha mpira mkoa (ARFA) juu ya kurekebisha vyumba vya kuvalia wachezaji pamoja na vyoo kuweka marumaru na madirisha lakini jitihada hizo hazijazaa matunda mpaka sasa huku nyasi zikikauka kabisa na kujenga hali ya viraka.

Waziri Juma Mkamia ameingia katika tuhuma hizo baada ya kutoa majibu yenye ukakasi bungeni alipotakiwa kutoa ufafanuzi juu ya vilabu kuwa na viwanja vyake na jitihada ya serikali kuboresha viwanja vya michezo hapa nchini.

Kwa upande wake Katibu wa chama cha soka mkoa wa Arusha alisema kuwa jiografia ya uwanja huo ni nzuri ila mapungufu machache yanayoukabili uwanja huo ikiwemo sakafu ya vyumba vya kubadirishia nguo wachezaji na uhaba wa vyoo vya watazamaji.

“Ni kweli uwanja huo una mapungufu hayo ila tumeshaongea na meneja wa uwanja kuufanyia marekebisho uwanja huo kwa mujibu wa maagizo ya TFF yaliyotolewa na raisi wa TFF Jamal Malinzi mwishoni mwa mwaka jana”

Meneja wa uwanja huo Andrew Mneja alisema kuwa tiyari mikakati ya kuuboresha uwanja huo unafanyika ambapo wataufunga wiki ijayo march 25 na tiyari wakandarasi wameshakagua na wataanza maboresho karibuni ikiwemo kuumwagilia kustawisha nyasi.

Mwisho………….

Mwili wa mwanamke uliookotwa CCM mkoa bado haujatambuliwa

kamanda Liberatus Sabas


na Bertha Ismail - Arusha

Jeshi la polisi mkoani Arusha limewataka wakazi wa Arusha kujitokeza kuutambua mwili wa mwanamke mmoja mwenye umri kati ya miaka 18-20 aliyekutwa amefariki huko eneo la mjini kati jirani na ofisi ya CCM mkoa.

Akizungumza na gazeti hili, kamanda wa polisi mkoa wa Arusha, kamanda Liberatus Sabas alisema kuwa mwili huo uliohifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali ya mkoa, Mount Meru umeokotwa mapema jumatatu march 23 mwaka huu ndani ya Carvati liliopo eneo la CCM mkoa.

Alisema mwili wa mwanamke huyo bado haujatambuliwa  hadi sasa jina wala makazi yake ambapo inasadikika marehem alifariki na kukaa hapo zaidi ya wiki moja huku chanzo cha kifo kikiwa hakijafahamika hadi sasa ambapo mwili huo umegundulika kutokana na harufu kali iliyokuwa inatoka kwenye eneo hilo.

“Baada ya watu kusikia harufu hiyo ndio kuchunguzwa inapotokea na kubainika kuwepo kwa mwili huo ulioanza kuoza na jeshi la polisi kwa kushirikiana na zima moto walifanikiwa kuutoa na kuuhifadhi mount meru.

Wakati huo huo jeshi la polisi limefanikiwa kukamata magunia 11 ya madawa ya kulevya aina ya bhangi na mtu mmoja aliyekuwa akisafirisha huko maeneo ya bara bara ya Arusha / Namanga wilayani Longido mkoani Arusha.

Akizungumza na waandishi, Kamanda Sabas alisema kuwa madawa hayo yalikuwa yakisafirishwa kutoka Arusha kuelekea Longido kupitia gari Toyota land Crusa Pick-up yenye namba T.695 ARR Mali ya kampuni ya uwindaji ya Wengert Windrose iliyokuwa ikiendeshwa na Frank Faustine (40).

“Kufuatia tukio hilo, pia tunamshikilia dereva huyo Frank Faustine kwa upelelezi zaidi na akibainika kuhusika sheria itachukua mkondo wake, ila naomba kutoa wito kwa wakazi wa Arusha kuacha kujishughulisha na biashara haramu ya madawa ya kulevya na wafanye biashara halali ya kujipatia kipato” alisema Sabas

Mwisho……………….

Zitto akataliwa ACT


Kigingi hicho, kimewekwa na Mwenyekiti wa ACT aliyesimamishwa uongozi, Kadawi Limbu, akisema Zitto aliyejiunga na chama hicho siku nne zilizopita anapaswa kusubiri mpaka atakapotimiza miezi sita ya uwanachama wake.

Limbu ambaye bado anajitambua kama mwenyekiti halali wa ACT-Tanzania, ametoa tamko hilo wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

“Mimi bado ndiye mwanyekiti wa ACT- Tanzania kwa vile barua inayodaiwa kuniondoa katika nafasi ya uenyekiti haikuwa halali na ilinifanya nipeleke suala hilo mahakamani kwa ajili ya kupata muongozo,”amesema.

Kwa mujibu wa Limbu, katiba ya chama hicho inaelekeza wazi kwamba mwanachama yeyote anayetaka kugombea nafasi ya uongozi ni lazima uwanachama wake uwe umetimiza zaidi ya miezi sita tangu ajiunge na chama hicho.
“Mkiangalia mtaona Zitto ambaye amejiunga na chama hicho hivi karibuni katika mazingira tata, katiba haimruhusu kugombea nafasi yeyote katika chama chetu, nimuombe kwamba andelee kuwa mwanachama wa kawaida tu,”amesema Limbu.

Pia, amemtaka Katibu Mkuu wa ACT-Tanzania, Samson Mwigamba kuacha kuwapotosha wanachama kuhusu uchaguzi huo kwani sio wa halali kutokana na Limbu kufungua kesi ya kikatiba mahakamani kupinga kuondolewa katika nafasi ya uenyekiti.
Akizungumzia chanzo cha mgogoro huo, Limbu amesema yote hayo yamechangiwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, kutokana ofisi hiyo kufanya kazi kwa utashi huku ikitoa taarifa zinazokanganya.

Limbu amefafanua kuwa ameamua kumpeleka Msajili katika Ofisi za Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), kwa madai kuwa amekula njama katika kumpa barua ya kumzuia kuwa mwenyekiti wa chama hicho.
Ametoa angalizo kwamba atapigana hadi kufa kuliko kuona chama hicho walichokianzisha kwa gharama kubwa, kikiangukia mikononi mwa mafisadi.
“Kuna watu wanajiita wazalendo lakini ukiwafuatilia utabaini kuwa wamejivika kofia hiyo kwa ajili ya kunyang’anya haki za wenzao. Watu hao ni sawa na majambazi,”amesema.
Hata hivyo, uongozi wa ACT-Tanzania, umesema katiba yao, iliyoko kwa Msajili wa vyama vya siasa, inaonesha kwamba mwanachama yeyote anaweza kugombea nafasi yoyote ya uongozi endapo ametimiza siku saba tangu ajiunge na chama hicho.

Monday, March 23, 2015

Richard ang'ara mbio za baiskeli

na Bertha Ismail - Arusha

Bingwa wa kimataifa wa mbio za baiskeli mtanzania Richard Laizer ameng,ara katika mbio za taifa na kuibuka mshindi wa kwanza baada ya  kuwazidi washindani wenzake zaidi ya 70 kutoka mikoa sita ya Tanzania bara.

Laizer kutoka Arusha aliyerejea hivi karibuni kutoka Afrika ya kusini alitumia muda wa saa 3:27:01 kunyonga baiskeli yake umbali wa kilomita 133 na kujishindia kitita cha shilingi laki nne, akifuatiwa na anaeshikilia ubingwa wa taifa Hamis Hussein aliyemaliza wa pili kwa kutumia saa 3:28:30 na kujishindia shilingi laki mbili huku mpanda baiskeli kutoka mwanza Sunga Duba alikiibuka wa tatu kwa kutumia saa 3:28:40 kumaliza mbio na kujishindia laki moja na nusu taslim.

Mashindano hayo yaliyoandaliwa na club ya Arusha cycling kwa lengo kujifua kwa ajili ya mashindano mbalimbali ya kimataifa yalishirikisha washindani wa kitaifa na kimataifa ambapo vijana ( 20- 45) walichuana kumaliza mapema kilometa 133 huku wanawake na vijana wadogo (under 20) wakichuana kwa kilometa 80 pamoja na  wazee (45-..)ambao wengi wao walitoka mataifa ya ulaya , Amerika na Australia.

Kwa upande wa wanawake mpanda baiskeli mkongwe Sophia Hussein aliibuka mshindi wa kwanza kwa kutumia saa 3:10:05 na  kufuatiwa na mpinzani wake Sofia Adson aliyetumia saa 3:22:11 huku mpanda baiskeli chipukizi Jamila Jumanne akimaliza wa tatu kwa kutumia saa 3:55:14 wote wakiwakilisha mkoa wa Arusha.

Wageni toka nje ya nchi walitamba katika mbio za wazee baada ya Steven Charmly toka Australia kushika nafasi ya kwanza na kufuatiwa na Thaday Peterson toka Amerika aliyekuwa pili na wa tatu akiwa ni Hendry Banderland kutoka Uholanzi.

Kadhalika kwa upande wa vijana wadogo, Kijana chipukizi Kelvin Didas (14) aling’ara katika mbio hizo na kuwakilisha vema baada ya kuwatoka wenzake umbali mrefu na kufuatiwa na David Philemon huku nafasi ya tatu akiibuka Mussa Husein wote kutoka mkoani Arusha.

Akizungumza na waandishi wa habari baada yam bio hizo, katibu msaidizi wa Arusha Cyclin Club, Thaday Peterson alisema kuwa mbali na kuvutiwa na mabadiliko makubwa ya msichana Sophia Hussein aliyeshika namba moja kutokana na kumshirikisha mashindano ya kimaifa Afrika Kusini msimu uliopita lakini zaidi amevutiwa na vijana wadogo.

“Kiukweli Sophia baada ya kushiriki mashindano ya Afrika kusini ameonyesha mabadiliko makubwa, lakini ukiachana na hayo uwezo walionao hawa vijana wadogo pia ni mkubwa sana hali inayovutia kuwekeza zaidi kwao hasa katika kuwashirikisha katika mashindano ya kimaifa na hii imetufanya sisi tuwe na kiu ya kuwatafuta vijana wadogo zaidi kwa wanaume na wanawake ili kutusaidia kufanya vema zaidi”


Mwisho…………………………..

Kikosi cha kupambana na ujangili Tanzania kimepata vitendea kazi

VITA YA KUPAMBANA NA UJANGILI YASHIKA KASI,KIKOSI CHA KUPAMBANA NA UJANGILI CHAPATA SILAHA ZA KISASA

Waziri wa Maliasili na Utalii,Lazaro Nyalandu akikagua magari matano yaliyotolewa kwaajili ya kupambana na ujangili katika kanda ya Kaskazini  kwenye uwanja wa ndege wa Kilimanjaro(KIA) yakiwa na thamani ya Sh 750 milioni.

Waziri wa Maliasili na Utalii,Lazaro Nyalandu akijaribu moja ya bunduki 50 aina ya AK 47 zilizotolewa kwaajili ya kupambana na ujangili katika kanda ya Kaskazini  kwenye uwanja wa ndege wa Kilimanjaro(KIA)
Arusha.Kikosi cha kupambana na ujangili nchini kimepata vitendea kazi kutoka kwa wadau wa  sekta ya utalii vitakavyowezesha kukabiliana na matukio ya ujangili yaliyoshika kasi nchini na kuhatarisha kutoweka baadhi ya wanyama.

Miongoni mwa misaada iliyotolewa ni magari matano aina ya Land Cruser yenye thamani ya Sh 750 milioni,bunduki za kivita 50 aina ya Ak 47 na risasi 10,000 na Magazini 20 ambazo thamani haikutajwa kwa kwasababu za kiusalama.

Waziri wa Maliasili na Utalii,Lazaro Nyalandu baada ya kukagua vitendea kazi hivyo kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro(KIA) amesema vitasaidia kuongeza nguvu za kufanya doria na kupambana na ujangili kwenye mapori ya akiba nchini na kudhibiti utoroshwaji wa nyara za serikali.

Nyalandu amekiri kuwapo kwa changamoto ya mwingiliano wa maeneo yaliyohifadhiwa na makazi ya wananchi  ambayo inatatuliwa kwa mujibu wa ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM)lengo likiwa kuwa na uhifadhi endelevu ambao unaleta maendeleo endelevu kwa wananchi.

Naye Naibu Mkuu wa Kikosi cha kupambana Ujangili Kanda ya Kaskazini,Michael Msuka amesema vitendea kazi hivyo vitaongeza hari ya watumishi katika kulinda wanyamapori katika mikoa ya Arusha,Kilimanjaro,Manyara na Tanga.

Alisema vita ya kupambana na ujangili ni kubwa kwani katika kipindi cha mwezi Septemba hadi Disemba mwaka 2014 jumla ya majangili 203 walikamatwa kwenye maeneo mbalimbali nchini na kuwa wamefikishwa mahakamani na baadhi yao kutozwa faini.

Zitto kuvuta 13 ACT

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEij1lKve_Gox0Rb1blCYaX_7_SJuQKWnpYmWECkNWNgZboQPUptgXWsGyGeCiivxN0phGs62G_GWTPplHtrjPsnyzlvgIaRLUDtNu4pBLbHBs-X3GwBruGMkkFmMOnkwhIiCJiC1TeIIKQ/s1600/A.JPG

http://www.mwananchi.co.tz/image/view/-/1671040/highRes/451183/-/y5yjqd/-/zitto.jpg 

Aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto

ALIYEKUWA Mbunge wa Kaskazini, Zitto Kabwe amejiunga rasmi na chama cha siasa cha ACT, huku akisema ana kundi kubwa la watu watakaomfuata, wakiwemo wabunge 10 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano ya Tanzania.


Aidha, Diwani wa Chadema Kata ya Mabogini Moshi Vijijini, Wakili maarufu Albert Msando, naye amejiunga na chama hicho kipya, akiutema rasmi udiwani wake.

Zitto, mmoja wa wanasiasa mahiri vijana, alitangaza kuhamia ACT jana katika mkutano wake na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Alisema anajua anachokifanya, hivyo kuhamia kwake ACT si kwa bahati mbaya, huku akisema pamoja na uchanga wa chama hicho, atahakikisha kinakua kwa kasi na hata kupiku baadhi ya vyama vya siasa vyenye umaarufu kwa sasa.

Akizungumza na gazeti hili jana jijini Dar es Salaam, baada ya kuzungumza na waandishi wa habari, Zitto alisema nyuma yake wapo wabunge zaidi ya 10, watakaojiunga na ACT muda sio mrefu.

“Siko mwenyewe wapo wenye mapenzi mema na tunataka kufungua ukurasa mpya kwa nchi yetu wa siasa za kujenga nchi, wabunge mahiri wa CCM na Chadema zaidi ya 10, watajiunga nami, ila sitakutajia majina kwa sasa kwa sababu ya sheria za vyama vyao, acha wamalizie vipindi vyao vya ubunge,” alisema Zitto ambaye jana alishawishi watu 12 kujiunga ACT, akiwemo msanii nyota wa muziki wa kizazi kipya, Selemani Msindi ‘Afande Sele’.

Awali, Zitto akizungumza na gazeti hili, alisema yeye ni mwanachama rasmi wa ACT mwenye kadi ya uanachama namba 7184, na kwamba amelipia ada ya miaka 10, ya uanachama wa chama hicho, ambayo kila mwaka ada ni Sh 1,000.

“Nimejiunga rasmi na ACT na nimelipa ada ya miaka 10 ya uanachama, nawakaribisha wote wenye mapenzi mema ya kujenga nchi wajiunge nasi”,alisema Zitto. Majimbo 6 yanamsubiri.

Akizungumzia uchaguzi mkuu ujao, Zitto alisema atagombea nafasi ya ubunge kwa kuwa umri wake hauruhusu kugombea nafasi ya rais, na kwamba jimbo atakalogombea litawekwa wazi baada ya yeye kushauriana na washauri wake, kwa kuwa majimbo zaidi ya sita nchini yanamtaka agombee.

“Nitasema hapo baadaye ninagombea jimbo gani, kwa sababu majimbo mengi yananiita nikagombee; Kawe wananitaka, Segerea, Kasulu, Kahama, hivyo nitazungumza na wenzangu halafu nitasema nitagombea wapi”, alisema Zitto.

Alitetea uamuzi wake wa kuhamia ACT, akisema ni uamuzi sahihi kwa kuwa chama hicho kinaendana na kile alichokuwa anakipigania kwa miaka

Tanzania wawapiga Kenya 2-1

na Bertha Ismail - Arusha

Timu ya Tanzania veterani imewachabanga timu ya maveterani wa Kenya kwa jumla ya magoli 2-1 katika mechi ya kirafiki ya maveterani hao mapema mwishoni mwa wiki katika uwanja wa Sheik Amri Abeid ya jijini Arusha.

Timu ya Maveterani kutoka Kenya ijulikanayo kama Senious Footbal club walionesha uwezo mkubwa wa kusakata kandanda safi mithili ya Serengeti boy lakini pamoja na uwezo huo walishindwa kulinda lango lao vema na kuipa nafasi timu ya maveterani wa Tanzania “Arusha all stars” kutikisa nyavu zao dakika ya 35 kupitia kwa mchezaji wao Abdulrazaki Hussein matokeo yaliyodumu hadi mda wa mapumziko.

Kipindi cha pili kilianza huku mashambulizi makali yakielekezwa zaidi kwa lango ya Tanzania kwa mikwaju mikali ambayo hata hivyo iliokolewa na mlinda mlango mahiri wa Arusha all stars Godrich Samweli na baadae dakika ya 75 Kenya walisawazisha goli hilo kwa njia penalt iliyopigwa na Varees Aura, baada ya mchezaji wao kufanyiwa madhambi eneo la hatari.

Matokeo hayo yalionekana dhahiri kuwaamsha usingizini timu ya Arusha All stars na kuanza kuchangamkia lango la Senious fc ya Kenya ambapo mbali na mikwaju kadhaa kuchomolewa lakini dakika ya 80 Richard Lukas Manyika alifanikiwa kupiga shuti kali lililomuacha mlinda mlango wa Kenya na mpira huo kujaa nyavuni matokeo yaliyodumu hadi mwamuzi wa kati Gasper Ketto alipopuliza kipenga cha kuashiria mchezo kwisha.

Akizungumzia mechi hiyo, Katibu wa Arusha All stars alisema kuwa wameamua kuvuka mipaka ya Tanzania kwa kuwaalika maveterani wenzao wa Kenya wacheze pamoja huku ikiwa kama mazoezi kwao katika mashindano makubwa ya pasaka sambamba na kufahamiana lakini pia kujenga undugu wa kisoka baina ya nchi hizi.

“Sisi kama Arusha all stars tumevuka mipaka na kucheza na timu ya  Senious ya Kenya ambapo tunadumisha undugu wetu lakini pia ikiwa ni kama sehemu ya kutafuta marafiki wa soka ili kuendeleza soka la mkoa wetu na nchi kwa ujumla”

Mwisho……………………….

wanachama wa Yanga wawakataa wachezaji waliochezea Simba

Mwenyekiti wa tawi la yanga Arusha, Richard Elibariki Mollel amesema kuwa utafiti uliofanywa na wanachama wa yanga ikiwemo tawi la Arusha umeonyesha kuwa tangu yanga ianze kusajili wachezaji kutoka simba au waliowahi kuchezea samba timu yao ya yanga imekuwa ikifungwa na simba na shutuma kuangukia wachezaji hao.

Hivi sasa yanga inawachezaji zaidi ya watano tena wa kikosi cha kwanza waliowahi kuichezea simba na ukiangalia ndio chanzo cha yanga kugeuka vibonde kwa simba kikiwemo kipigo cha wiki iliyopita cha bao 1-0 na safari hii lawama zikiwaangukia Danny Mrwanda na kipa Alli Mustafa ‘Bartez’.

Mshabiki mkubwa wa timu ya Yanga mkoani hapa Ernest Manyilizu alisema kuwa tunaomba uongozi kama watatusikia warudie mfumo wa zamani wa kuwasajili wachezaji wakali kutoka timu zingine za mikoani kuliko kuelekeza macho yao kwa mkoa wa Dar-es-salaam hali ambayo inatutia aibu kufungwa na timu Simba kila mara kwa sisi kuwa vibonde wao.

“Mimi niseme tu kuwa uongozi wa juu wa Yanya utupe mahitaji yetu sisi mashabiki wao kwa kuachana na kusajili wachezaji waliowahi kutumika Simba kwani inawezekana wachezaji hao wakaja na mapenzi ya Simba kuitumikia Yanga hivyo ni rahisi kufanya urafiki wa kuwaachia ushindi na kama unavyojua ni bora kufungwa na timu zingine kuliko tufungwe na Simba hii ni aibu sana kutokana na sisi mbali na kuwa wakongwe wa soka lakini kumbuka ni watani wa jadi” alisema Ernest Manyilizu.

Mwanachama mwingine wa yanga Kefasi Filex “Sunguti” anasema “hata enzi za akina Nuruduni Bakari, Juma Kaseja na Athuman Idd Chuji,  yanga imekuwa ikifungwa kirahisi na wana Simba na sasa suluhisho ni kutema wachezaji wote waliowahi kuchezea Simba na kuepuka kusajili wachezaji toka kwa wapinzani wetu hao wa jadi, hivyo waangalie mpango mwingine wa kupata wachezaji wazuri ikiwemo hata kufanya mashindano maalum ya kusaka wachezaji au kutafuta nyota wakali katika timu hizi ndogo”

Mwisho………………………………..

Wednesday, March 18, 2015

Mwili wa Marsh kuhifadhiwa kwenye nyumba yake ya milele "Buriani"


MKUU wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo, leo ameongoza mamia ya wakazi wa Jiji la Mwanza na mikoa jirani ya Kanda ya Ziwa kumuuaga mwili wa marehemu Sylvester Balunzi Mashishigulu ‘Marsh’,yaliyofanyika uwanja wa Shule ya msingi Mirongo Jijini Mwanza.
Meya wa Jiji la Mwanza , Stanslaus Mabula alisema,jiji la Mwanza akielezea wasifu wa marehemu Marsh, ikimbukwe kuwa Mstahiki ndiye mlezi wa kituo cha soka cha Marsh Academy.
Mchezaji wa zamani wa Yanga na Timu ya Taifa Stars, Edibily Jonas Lunyamila (kushoto) akielezea alivyomfahamu marehemu Marsh, na kulia ni mchezaji wa zamani wa timu ya Pamba, Yanga na Taifa Stars. Fumo Felician akiwa na majonzi.
Msanii wa tasnia ya filamu nchini Steve Nyerere akitoa ushuhuda wake.

Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu akitoa salamu za rambirambi na kuelezea jinsi Marsh alivyokuwa mwaminifu na kuwa mwanachama hai hata kwenye nyanja za siasa, wengine ni makatibu wa chama hicho toka wilaya mbalimbali mkoani Mwanza.

Familia.
Viongozi na wadau wa soka.

Hassan kiraka akiwa amemshika mkono kumuongoza mmoja ya watoto wa kituo cha Marsh Academy.

Mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya H.Baba akitoa heshima zake za mwisho.
Safu ya viongozi ni huzuni tupu....
Nini hatma ya vijana hawa wa kituo cha soka cha Marsh Academy.

Huzuni kwa timu ya U17 toka kituo cha Marsh Academy.

Sehemu ya umma uliofika eneo la tukio.
Sehemu ya umati uliwakilisha makaburini.
MKUU wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo, leo ameongoza mamia ya wakazi wa Jiji la Mwanza na mikoa jirani ya Kanda ya Ziwa kumuuaga mwili wa marehemu Sylvester Balunzi Mashishigulu ‘Marsh’,yaliyofanyika kwenye makaburi ya Igoma nje kidogo ya Jiji la Mwanza.

Pia katika mazishi hayo, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga, Khamis Mgeja, aliwaongoza waombolezaji katika mazishi hayo yaliyohudhuriwa na viongozi wa serikali na  vyama vya siasa, madhehebu ya dini,wananchi, wadau wa michezo,wanasoka wa vizazi mbalimbali ,makocha na waamuzi kutoka mikoa mbalimbali nchini.

Mulongo aliwaasa waombolezaji waliojitokeza kuaga mwili wa kocha huyo kwenye uwanja wa shule ya Msingi Mirongo kuwa ,ili kumuenzi kwa vitendo ,wadau wa soka mkoani hapa wachague timu moja na uwanja utakaoitwa jina lake.

Mkuu huyo wa mkoa wa Mwanza, aliutaka uongozi wa chama cha Soka mkoa wa Mwanza (MZFA) waandae programu ya kuanzisha michuano ya mpira wa miguu itakayofanyika kila mwaka na kuiwasilisha ofisini kwake ikiwa na lengo la kumuenzi kwa vitendo ikiwa ni pamoja na kuibua vipaji vya vijana na kuviendeleza kama ilivyokuwa dhamira ya marehemu.

Aidha Mgeja akimzungumzia marehemu alisema marehemu Marsh aliwea kujitolea kuitangaza Mikoa Mara, Kagera, Mwanza, Shinyanga, Dar es salaam na  taifa katika medani ya kimataifa,wakati akifundisha vilabu mbalimbali vya hapa nchini ikiwemo timu za taifa ya vijana Serengeti boys na Taifa stars.

Kwa wake Meya wa Jiji la Mwanza , Stanslaus Mabula alisema,jiji la Mwanza litatenga viwanja vya michezo kwa ajili ya kuibua vipaji vya vijana wadogo wa lika tofauti zaidi ya 200 kwa nyakati tofauti na  ambao marehemu alikuwa akiwahangaikia  kuwalea kwa maisha ya soka katika maisha ya uhai wake.

“Amekuwa mwanzilishi wa vitalu vya kuendeleza mchezo wa soka mkoani na nchini hapa,matunda yake yameonekana kwa kutoa vijana wenye uwezo ambao wameweza kutoka nje kwenda kufanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa lakini pia wapo wanaocheza katika vilabu vya  Ligi Kuu nchini,”alisema Mabula.

Wadau mbalimbali wa soka wakiwemo wachezaji wa zamani na wa kizazi cha sasa, walionesha masikitiko yao makubwa kwa kumpoteza mtu muhimu katika familia ya soka,kwamba pengo lake haliwezi kuzibika kutokana na mchango wake wa kuendeleza mpira wa miguu nchini katika maeneo aliyofanyia kazi ya ukocha.

Diwani wa Kata ya Mirongo Daudi Mkama (CUF) alimpongeza Meya wa Jiji la Mwanza Mabula kwa moyo wake wa kujitolea na kuamua kugharamia sehemu kubwa ya mazishi ya marehemu Marsh tangu kuwasili kwake, kuagwa na kupelekwa nyumbani kwao Igoma na wananchi wa maeneo hayo kutoa heshima za mwisho kabla ya kushiriki mazishi yake yaliyofanyika makaburi ya Igoma nje kidogo ya Jiji la Mwanza.

"Munyonge munyongeni na mtu anayefanya jambo jema hatuna budi kumsifia na kumpongeza, kwa hili alilolifanya Mstahiki meya wa Jiji, Mabula la kuhakikisha mambo yote yanakwenda sawa kwa asilimia 90 ni kuonyesha ameguswa lakini kama kiongozi wa watu ametekeleza wajibu wake kwa moyo wake wa kujitolea,"alisisitiza Mkama.

Wadau wa soka kutoka mikoa mbalimbali nchini wakiongozwa na RC Mulongo, Meya Mabula, DC Baraka Konisaga (Nyamagana), DC Angelina Mabula (Iringa), Kocha na Mwakirishi wa TFF Salum Madadi, Mwenyekiti wa MZFA Jackison Songola, Mbunge wa Jimbo la Rorya - Mara Lameck Airo (CCM) kumuaga na kisha mazishi yake kuongozwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja, wananchi na wadau wengine.

Viongozi wastaafu wa soka Arusha wajipanga kugombea tena

na Bertha Ismail - Arusha

Viongozi wa zamani wa chama cha soka wilayani Arusha ADFA wanajipanga upya kuingia madarakani katika uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika wakati wowote kuanzia sasa kufuatia uongozi uliopo madarakani kumaliza muda wake.

Viongozi hao wakiongozwa na katibu wa zamani wa ADFA Robert Munis wamekuwa wakifanya vikao vya kupanga mikakati madhubuti wa kuwang,oa madarakani kamati yote ya utendaji ya ADFA kwa kigezo cha kuporomosha soka la Arusha kwa kuvipa vilabu mzigo wa michango mbali mbali ikiwemo ada kubwa ya ushiriki ligi hali ambayo timu nyingi zenye uwezo zimekwama kushiriki ligi za taifa kuanzia ngazi ya wilaya hadi mkoa.

Hadi sasa vikao zaidi ya vinne vimeshafanyika katika mgahawa maafuru unaojulikana kama Spice Inn uliopo pembezoni mwa uwanja wa Sheih Amri Abeid na kushirikisha wajumbe wa zamani wa ADFA akiwemo Hessein Lembarity aliyekuwa mwenyekiti, Abdul kondo aliyekuwa mjumbe na mkurugenzi wa rollingstone Ally Mtumwa aliyewahi kuwa mjumbe wa mkutano mkuu wa TFF.

Akizungumzia lengo lao hilo la kurudi kwenye uongozi, Robert Munis anasema yeye alistaafu kwa hiyari yake baada ya kuwa katibu kwa zaidi ya miaka 10 kutokana na kuzidiwa na maswala na kazi na familia huku akiamini atakaowaachia wataendeleza mema yale ikiwemo kuziongeza timu nyingi kushiriki ligi mbali mbali sambamba na kubuni mashindano mengine mengi kuongeza idadi ya yaliyokuwepo lakini hali haikuwa hivyo.

“Unajua mimi nilizidiwa na maswala yangu ya kazi na familia hivyo nikabidi niachie ngazi moja nishikilie familia na kazi yangu huku nikiamini hawa nitakaowaacha watafanya muendelezo lakini nasikitika sana kusikia eti soka la Arusha sasa limedorora na mashindano mengi yaliyokuwepo yamekufa hali ambayo ni mbaya sana timu kufanya mazoezi pekee kwa ajili ya ligi ya Taifa”

“Hivyo basi kama mdau wa soka mkoa huu sitakubali kuona soka la Arusha linakufa kifo cha aibu kiasi hiki kutokana na uzembe ulioko madarakani ni bora tuwaondoe turudi tufanye kazi na niombe wadau wa Arusha wajitokeze kuunga mkono hili lifanikiwe kurudisha heshima ya Arusha kuwakilishwa na timu mbili hadi taty ligi za juu (daraja la kwanza na ligi kuu)” alisema Robert alieonekana wazi kujaa jazba.

 Alisema kuwa sasa analazimika kurejea kwa kishindo baada ya kusikitishwa na kuporomika kwa soka la Arusha na kutengwa kwa soka la Arusha na wadau mbalimbali wakiwemo wafadhili, wafanyabiasha na viongozi wa kitaifa ambapo alisema kuwa chanzo cha kudorora kwa soka.


Inasikitisha mkoa wa Arusha uliowahi kuwa na timu tatu ligi kuu sasa hakuna hata timu moja na hata michezo ya kimataifa iliyokuwa ikichezwa Arusha sasa haichezwi achilia mbali kuharibika kwa uwanja wa sheikh Amri Abeid kutokana na kujaa mashimo kila upande huku vichuguu vikichipuka kila pembe na majani yake kunyauka kutokana na viongozi wa soka kufumbia macho swala hili, huku viwanja vingine tegemezi vikifungwa bila uongozi kuomba upendelea kwa timu kufanyia ,mazoezi na mashindano.

Aidha uchaguzi wa soka ngazi za wilaya za mkoa wa Arusha zinatarajiwa kuanza wakati wowote kuanzia mwezi Aprili huku wagombea wa nafasi mbali mbali wakipigana vijembe chini chini kuwania nafasi hizo lakini wengi wao wakitupia lawama uongozi wa sasa na kuwa na nia moja ya kuwang’oa madarakani.

Mwisho……………………..

Sunday, March 15, 2015

Baadhi ya wananchi wa kanda ya kaskazini waandamana hadi kwa Lowassa kumshinikiza kutangaza nia ya kugombea Urais 2015



 makundi mbalimbali ya kijamii ya mikoa ya Kaskazini, inayojumuisha mikoa ya Kilimanjaro, Tanga, Arusha na Manyara wakiwa wanaandamana kwa pamoja kuelekea kwa mbunge wa jimbo la monduli  hii leo
Katibu wa Chama cha Wasioona Mkoa wa Kilimanjaro  (TLB), Protas Soka Akisoma risala kwa niaba ya makundi hayo mbele ya mbunge wa jimbo la monduli
 Viongozi mbalimbali wa makundi ya kijamii wakiwa wanamkabidhi waziri mstaafu ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Monduli Edward Lowasa bahasha yenye fedha taslimu shilingi milioni mbili laki tano sitini na saba elfu na mia sita zilizochagwa na wananchi   kwa ajili ya kwenda kuchukuwa fomu ya kugombea nafasi ya Urais
 mbunge wa jimbo la monduli akiangalia picha ambayo ametengenezewa na  vijana kutoka makundi wakati walipomtembelea nyumbani kwake monduli kwa ajili ya kumkabidhi fedha kidogo kwa ajili ya kuchukuwa fomu ya kugombea urais

 makundi mbalimbali ya kijamii ya mikoa ya Kaskazini, inayojumuisha mikoa ya Kilimanjaro, Tanga, Arusha na Manyara wakiwa wanaandamana kwa pamoja kuelekea kwa mbunge wa jimbo la monduli  hii leo

 makundi mbalimbali ya kijamii ya mikoa ya Kaskazini, inayojumuisha mikoa ya Kilimanjaro, Tanga, Arusha na Manyara wakiwa wanaandamana kwa pamoja kuelekea kwa mbunge wa jimbo la monduli  hii leo
Mratibu wa Marafiki wa Lowasa Kanda ya Kaskazini, Noel Nnko,akiwa anamuonyesha picha ambayo ni ya kumbukumbu ya tukio la leo la kuja kumuunga mkono mbunge wa jimbo la monduli pamoja na kumuomba atangaze nia  ya kugombea nafasi ya urais
maandamano ya pikipiki yakiwa yanaelekea nyumbani kwa mbunge wa jimbo la monduli hii leo
Wananachi zaidi ya 700 kutoka makundi mbalimbali ya kijamii ya mikoa ya Kaskazini, inayojumuisha mikoa ya Kilimanjaro, Tanga, Arusha na Manyara, wamejitokeza nyumbani kwa Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli (CCM), Edward Lowasa, wakimshawishi atangaze nia ya kugombea urais kupitia chama hicho.

Wananchi hao kutoka katika Makundi mbalimbali katika  ya  mikoa hiyo yamewasili leo nyumbani kwake,Kijiji cha Ngarashi, Wilaya ya Monduli baada ya kufanya maandamano makubwa yaliyoanzia njia panda ya Monduli, wakiimba nyimbo za matumaini kwamba ‘wewe ni tumaini la walio wengi Tanzania, maamuzi na matumaini mapya, watanzania wako nyuma yako’.

Aidha akisoma risala kwa niaba ya makundi hayo baada ya kuwasili nyumbani hapo , Katibu wa Chama cha Wasioona Mkoa wa Kilimanjaro  (TLB), Protas Soka alisema kwa nia thabiti isiyo na kigugumizi asilani, wanaharakati hao pamoja na watanzania wengine wanamhitaji  (Lowasa) kwa unyenyekevu na hivyo, wanamwomba atangaze nia ya kuingia kwenye kinyang’anyiro cha Urais mwaka 2015.

“Leo watanzania tumepaza sauti zetu kwa pamoja kuanzia ngazi ya Kaya,Kitongoji,Kijiji,Kata,Tarafa,Wilaya, Kanda mpaka Taifa wakisema Viva Lowasa, Tobiko Lowasa. Kwa moyo mmoja bila kushawishiwa na mtu wala kikundi chochote;  wanaharakati hawa wamekuona wewe, mheshimiwa Edward Lowasa ndio kiongozi sahihi kwa mustakabali na manufaa ya taifa letu,”alisema Soka

Makundi hayo ambayo ni walemavu, waendesha bodaboda, walimu, wataalam wa afya, vijana na wanasiasa, walimchangia Lowasa kiasi cha shilingi milioni 2,567,600 kwa ajili ya kununua au kulipia fomu ya kugombea nafasi ya Urais pindi atakapotangaza nia.

“Kwa lugha nyingine sasa tunakuomba Mheshimiwa Lowasa sasa tunakuomba utangaze nia ya kuingia kwenye kinyang’anyiro cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,”alisema Soka.

Makundi hayo yaliyoongozwa na Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Kilimanjaro, Paul Matemu, Mratibu wa Marafiki wa Lowasa Kanda ya Kaskazini, Noel Nnko,Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana (UVCCM), mkoa wa Arusha, Robnson Meitinyiku, Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa, Fred Mushi, Askofu wa Kanisa la Calvary Assemblies of God, Christoher Madilu ambaye pia ni Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa na Abdalah Sadick kutoka mkoa wa Manyara.
Akizungumza mara baada ya kupokea makundi hayo mbunge huyo wa jimbo la monduli alisema kuwa amekubaliana nao na anatarajia kutangaza rasmi nia mwezi aprili pindi tu chama chake kitakapo ruhusu

 “Nitatangaza nia mwezi Aprili mwaka huu, pale uwanja wa Shekhe Amri Abeid mjini Arusha baada ya chama changu kupuliza kipenga. Ninachowaomba watanzania kwa sasa, mniombee katika safari yangu ya matumaini,”alisema Lowasa.