Bertha Ismail - Arusha
“Nimefurahi
sana kuona jinsi kiwango changu kinapanda
na naamini hii ni mwanzo wa kutimiza ndoto zangu za kuwa mtaalamu wa mchezo wa
gofu niweze kushindana kwa kulipwa na kuwa mchezaji maarufu wa mchezo huu na
kuiwakilisha nchi yangu vema”.
Ni maneno ya
kijana mdogo aliyeko kundi la Junior Mohamed Ally alipokuwa akizungumza na
waandishi wa habari baada ya kuibuka mshindi wa jumla katika michuano ya Arusha
Open yaliyoshirikisha wachezaji 82 wa gofu kutoka mikoa mbali mbali nchini
pamoja na nchi za Dubai na Kenya.
“Mimi ndoto
zangu ni kuwa profesheno wa gofu nchini ili niweze kuwa mchezaji wa kulipwa na
kuchuana katika mashindano mbalimbali ya kitaifa na kimataifa na kuitangaza
nchi yangu hivyo watu wasishangae uwezo wangu wakalinganisha na umri wangu wa
chini ya miaka 18 bali waangalie kipaji change na ndoto zangu ambazo siri hii
ni mazoezi ya mara kwa mara kama sala kwangu”
Ally wa
Arusha ametwaa ushindi wa jumla baada ya kupata nyavu 131, (131 nett) katika kumbi 36 (36 halls) kwa siku
mbili, huku kwa daraja la kwanza Richard Gomes (Arusha) akitwaa ushindi kwa
kupata nyavu 152 nett akifuatiwa na Victor Joseph wa Dar –es-salaam kwa kupata pia nyavu 152.
Kwa upande
wa daraja la pili Prabvir Singh alitwaa ushindi kwa nyavu 146 akifuatiwa na
Muzzafer Yusufally kwa nyavu 156 wote wa
Arusha na daraja la tatu Hiten Nathwan ambae ni mwenyekiti wa Arusha Gymkana
Club kwa nyavu 150 akifuatiwa na Mona Singh kwa vyavy 151.
Akizungumzia
mashindano hayo mwenyekiti wa mashindano kutoka chama cha Gofu Taifa alisema
mashindano hayo ya Taifa yaliyoko kwenye kalenda ya TGU yana lengo la kutambua
wachezaji wazuri wa machezo huo, kukuza vipaji vya vijana wadogo sambamba na
kuvinoa vilivyopo.
“Kwanza
niseme tu nimefurahishwa na uwezo mkubwa aliyoonyesha kijana mdogo Ally
ukilinganisha na umri wake hali ambayo inatia moyo kuwa kwa sasa vilabu vina wachezaji
wazuri watakaounda timu ya nchi yetu na kuna baadhi ya wachezaji wengine
tumewaona na tutawaangalia tena kwenye michuano ya Taifa yatakayofanyika Moro
goro”
“Lengo la
mashindano hayo ya Morogoro ni kutafuta wachezaji wazuri watakaounda timu ya
Taifa itakayokaa kambini kwa kujinoa kushiriki michuano ya nchi za Afrika mashariki na kati yatakayofanyika
Octoba nchini Kenya”
Mashindano
hayo ya Arusha Open yaliyodhaminiwa na I&M bank yajulikanayo kama “I&M
Golf Arusha Open” yameshirikisha wachezaji 82 kutoka vilabu vya Arusha, Dar,
Moshi, TPC, Lugalo, Nairobi na Dubai.
Mwisho…………….
0 comments:
Post a Comment