Timu ya
Arusha fc inayoshiriki ligi daraja la pili msimu ujao wa ligi ya Tanzania bara
imejikuta ikihitaji zaidi ya milioni 28 kwa ajili ya kugharamia timu hiyo hadi
kumalizika kwa SDL msimu wa 2015/2016, hivyo kuwaomba wadau watoe ushirikiano
wao kuhakikisha fedha hizo zinapatikana.
Zaidi ya
hayo wamewaomba wadau wa soka mkoani Arusha, kujitokeza katika kudhamini
chochote katika timu hiyo ili kuwezesha kuwatangaza katika mikoa yote
watakayocheza lengo ikiwa ni kutimiza azma yao ya kupanda hadi ligi daraja la
kwanza.
Hayo
yamejiri katika mkutano maalum wa wadau wa timu hiyo iliyofanyika hivi karibuni
katika viwanja vya Sheik Amri Abeid uliokuwa na lengo la kujadili namna ya
kuanza maandalizi ya ligi yao ya daraja la pili ikiwemo kufanya usajili,
kutafuta kocha sambamba na benchi la ufundi na viongozi.
Katika
mkutano huo uliohudhuriwa na wadau mbali mbali, Katibu Omari Kombo alisema kuwa
hadi kumalizika kwa ligi timu inahitaji milioni 28 kwa ajili ya kugharamia
usajili, malazi, usafiri pamoja na posho za wachezaji hivyo wadau watoe
ushirikiano wao kuhakikisha hili linafanikiwa ikiwemo kutafuta wafadhili wa
ndani na nje ya mkoa.
Katika
mkutano huo wadau pia waliamua kuteua viongozi watakao isimamia timu hiyo hadi
watakapo chagua viongozi wapya kwa mujibu wa katiba ya timu hiyo ambapo Abass Utanga
alipewa nafasi ya mwenyekiti, Wille Mollel makam mwenyekiti, Salim Kombo katibu
mkuu, Charles Mwaimu katibu msaidizi, Dr Kilavu mweka hazina.
Pia kamati
ya usajili na ufundi walioteuliwa ni Denis Shemtoi, Denis Nyambele, John
Change, Idd Mkulu, Azizi Nyoni, na Ally Wingi ambao Ndio watakao hakikisha AFC
inakuwa katika hali ya ushidani zaidi ya msimu ulipita na kufanikiwa kupanda
ligi daraja la kwanza.
SDL msimu wa
2015/2016, inayotarajia kuanza kutimua vumbi mwezi wa kumi tarehe 17 kwa mujibu
wa taarifa iliyotolewa na TFF huku AFC ikiwa imepangwa kundi B pamoja na
Alliance FC [Mwanza], Madini FC [Arusha], Bulyanhulu FC [Shinyanga], JKT
Rwankome [Mara], na Pamba ya Mwanza.
Mwisho…………….
0 comments:
Post a Comment