Mwanamichezo
wa gofu za ridhaa (amacha) Prabvir Singh ameibuka kidedea katika michuano ya
wazi ya siku mbili yajulikanayo kama “Northern province golf competition” na
kufanikiwa kuwa bingwa wa mashindano hayo kwa mwaka 2015/2016.
Mashindano
hayo ya wazi yaliyoandaliwa na chama cha gofu Tanzania, TGU (Tanzania gofu
Union) kwa kushirikiana na Arusha gymkhana club (AGC) yalifanyika kwa siku
mbili mwishoni mwa wiki ambapo Singh aliibuka mshindi wa jumla kwa kupiga mikwaju 141 na
kufanikiwa kuwa bingwa na kuzawadiwa kombe kubwa.
Michuano
hiyo iliyodhaminiwa na Benson Security System
pamoja na Sameer Parts ltd yaliweza kuwapa makombe pia mshindi wa daraja
la kwanza Simon Travers aliyepiga mikwaju 149 akifuatiwa na Izak Wanyeche
waliyepiga mikwaju 150.
Kwa daraja
la pili Jugdish Ahluwalia “Chuchu” aliibuka mshindi kwa kupiga mikwaju 146
akifuatiwa na Kush Lodhia 149 huku
daraja la tatu Rujvil Sohal akishinda kwa mikwaju 150 akifuatiwa na Alliabbas
Somji aliyepiga mikwaju 151 wote wa Arusha.
Northern
province golf competition yalishirikisha pia wanawake na Lina Francis wa Arusha
kuibuka mshindi kwa kupiga mikwaju 148 na kwa watoto Jafari Omary wa TPC moshi
kwa mikwaju 146 huku Habbib Yusufali (Arusha) akiibuka mshindi kwa upande wa
wazee kwa kupiga mikwaju 168 na wote kupatiwa makombe madogo.
Zawadi za
makombe pia zilitolewa kwa washindi waliovuka viwango (Cross winner) ambapo
Abbas Adam wa Moshi aliibuka kwa kupiga mikwaju 154 akifuatiwa na Danniel
Corpella kwa kupiga mikwaju 154 pia washindi wa siku ya kwanza Muzafar Yusufali
aliibuka mshindi kwa mikwaju 72 na Minir Sheriff wa moshi alimfuatia kwa
mikwaju 73.
Washiriki wa
mashindano hayo 61 kutoka vilabu vya TPC na moshi club, Lugalo sambamba na
Arusha walitakiwa na mgeni rasmi ambae ni mhazini wa gofu taifa Gelase
Rutachibirwa kuwa wajitahidi kutafuta chipukizi wa mchezo huo watakaokuwa na
viwango vizuri kuunda timu ya taifa ili kufanikiwa kushiriki katika mashindao
mbali mbali ya kimataifa na kuiwakilisha nchi yetu.
Kwa upande
wa mmoja wa wadhamini wa mashindano hayo kutoka Benson Security System, Nadeem
Hussein alisema kuwa mashindano ya mara kwa mara kama hayo yanaweza kuwafanya
wachezaji kupanda viwango na kuwa wataalam wa mchezo huo (Proffessional) na
kupata ajira.
Mwisho………….
0 comments:
Post a Comment