mwili wa Ibrahim baada ya kuopolewa kwenye bwawa hilo na wasamaria wema baada ya wataalam wavamiaji kukosekana |
Arusha.
Mtu mmoja, Ibrahim Issa (25) amekufa maji baada ya kutumbukia kwenye
bwawa lenye maji linalomilikiwa na kampuni ya Kili flora lililoko eneo
la Mlangarini Wilayani Arumeru mkoani Arusha.
mwili ukipelekwa pembezoni mwa bwawa tiyari kutolewa kwenye maji |
baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya maua ya kili flora wakiwa wanashuhudia mwili wa mwenzao baada ya kuopolewa kwenye bwawa. |
jeshi la polisi pamoja na maafisa wa zima moto wakiondoa mwili eneo la tukio kuupeleka chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya mkoa mount meru tiyari kwa mazishi |
Mwili
huo uliodumu kwenye maji kwa muda wa masaa 26, uliokolewa na wasamaria
wema waliojitolea kuutafuta mwili huo ili kuutoa kwenye bwawa
alikotumbukia lenye kina cha maji mita 20 chini na mita 500 urefu.
Baadhi
ya wafanyakazi wa kampuni hiyo ya Kili flora walisema kuwa marehemu
alitoka mapumziko ya kunywa chai saa nne asubuhi may 8 mwaka huu na
kubeba waya aliyotengenezea ndoano kwa ajili ya kwenda kujipatia samaki
lakini kwa bahati mbaya aliteleza na kuangukia ndani ya maji.
“Kwa
mbali tulisikia kama kuna kelele bwawani nyuma ya mashambani na
tulipokwenda kutazama tulimuona Ibrahim (Mrehem) Akiomba msaada na
tukafanya juhudi za kumrushia kamba kuvuta lakini haikuwezekana kwani
alishachoka na ndipo alipozama”alisema Jane Macha
Macha
alisema Tulitoa taarifa kwenye uongozi kumuokoa mapema lakini hata
hivyo ilishindikana kwa kutolewa ruhusa ya haraka kutokana na makao
makuu ya uongozi kuwa USA, eneo ambalo ni mbali na hapa hivyo baadae
uongozi ulipofika ulikuwa unasua sua kufanya taratibu za kumuokoa mapema
hivyo wananchi walijitosa kwenye maji na kuanza kumtafuta kucha bila
mafanikio.
Mwenyekiti
wa mtaa wa Olomitu, kata ya Mlangarine, Absalom Kambaine alisema kuwa
ingawa alichelewa kupata taarifa lakini siku ya pili asubuhi ya May, 9
alikwenda kuomba msaada wa kuupata mwili kwa wataalam wa maafa wakiwemo
jeshi la polisi, jeshi wananchi kikosi 977kj, na kikosi cha zima moto
lakini hakufanikiwa kwa kile kinachodaiwa ukosefu wa vifaa.
“Kiukweli
nimepata taarifa asubuhi hii nikaamka na kukimbia kimbia kwa wataalam
ambapo zimamoto walifika eneo la tukio lakini walisema hawawezi kuupata
mwili huo kwani hawana vifaa vya uokoaji majini pia wataalam wa kuzama,
nikaenda kambi ya jeshi hii hapa karibu moshono nao wakasema hakuna
wataalam wa uzamiaji majini bali wapo wavuvi pekee na hawataweza kufanya
kazi hiyo hadi kibali makao makuu pia polisi walifika hapa lakini wao
wakasema wamekuja kuweka ulinzi na kusubiri mwili tu” alisema mwenyekiti
Kambaine.
Kwa
upande wa baba mzazi wa marehem Joseph Issa alisema kuwa hali hiyo ya
mwanae kuzama na kukaa ndani ya maji kwa zaidi ya masaa 26 ni uzembe wa
vikosi husika na serikali kwa pamoja kukosa vifaa vya uokoaji ndio maana
maafa yanatokea mara kwa mara huku hakuna anaejishughulisha na
tahadhari hivyo wanamuachia Mungu swala hilo,
Mwisho………
0 comments:
Post a Comment