Bertha Ismail - Arusha
Wakati
matani ya hapa na pale yakiendelea baina ya mashabiki wa timu kongwe nchini
Simba na Yanga, mashabiki hao Arusha
wameamua kufuta ubishi wa nani Mb’abe wa kandanda safi, ambapo Simba
wamedhiirisha umwamba wao baada ya kuwabugiza Yanga mabao 6-3.
Mchezo huo
wa kirafiki uliowakutanisha mashabiki wa simba na yanga Arusha, uliopigwa
katika uwanja wa shule ya msingi Moshono kwa lengo la kutaka kujua nani m’babe
wa soka, Simba ilidhiirisha umwamba wake baada ya kuwapiga mashabiki wa Yanga
jumla ya mabao 6-3.
Mchezo huo
ulioanza kwa kasi ya aina yake na kujaza mamia ya mashabiki, Timu ya Simba ndio
ilianza kupata mabao mawili ya haraka haraka ambapo bao la kwanza liliingizwa dakika
ya sita mwa mchezo kupitia kwa Wilfred Kadege na Robert Boniface akipiga bao la
pili dakika ya nane na kupelekea mashabiki kujigawa kwa ushangiliaji.
Wachezaji wa
Yanga walionekana kujawa makali zaidi na kuongeza kasi ya kupambana kuligusa
lango la Simba ambapo dakika ya 25 Frank Shapi alifanikiwa kuipatia timu ya
Yanga bao la kwanza ambapo hata hivyo kipigo kwao kiliendelezwa na Robert
Boniphace aliyeiandikia timu yake ya Simba bao la Tatu dakika ya 34 hali
iliyozidisha hasira za wana-Yanga hao ya kulisakama lango la Simba ambapo hata
hivyo Frank Kamili alijifunga katika harakati za kuokoa na kuiandikia timu ya Yanga
bao la pili dakika ya 39 hadi mapumziko.
Kipindi cha
pili kilianza huku timu ya Simba ikionekana na mabadiliko ya hali ya juu na
mashambulizi ya iana yake na dakika ya 68 Wilfred Kadege aliiandikia samba bao
la nne na Robert Boniphace kuandika bao
la tano dakika ya 75 hali iliyonyamazisha kelele za mashabiki wa nje wa Yanga na
shangwe za mashabiki wa samba zikitawala na kuzidi kuvuta umati wa watu
kushuhudia mtanange huo.
Baada ya
mabao hayo wachezaji wa Yanga walionekana dhahiri kujawa na ghadhabu na jazba
za hapa na pale huku wengi wakikoswa koswa na kadi za mwamuzi Gasper Getto
lakini dakika ya 78 Mrope Mrope alibahatisha bao la tatu kwa timu yake ya Yanga
baada ya kupiga shuti lisilo na matumaini ya kupata bao na dakika ya 86 Frank
Kamili alifunga wingu la mvua ya mabao kwa timu ya Simba, na kuleta matokeo ya
6-3 hadi hadi dakika 90 kutia nanga.
Wakizungumza
na gazeti hili, Kaptein wa timu ya Mashabiki wa simba Arusha, Wilfred Kadege
alisema kuwa wameamua kutumia week end hiyo kuwafunga mdomo mashabiki wa Yanga
kwamba wao ndio wababe wa kandanda baada ya kuweka matambo mengi kwa mdomo
hivyo wakaamua kuwaonesha kazi ya Simba uwanjani.
“Tumeamua
kutumia jumapili hii kuwafunga mdomo hawa watani wetu maana wamekuwa wanatamba
sana mdomoni hasa baada ya kufanikiwa kucheza Kamari ya ligi kuu na kuwa
mabingwa lakini wajue kuwa hawatufikii kwa lolote kwani kama ni zawadi ya
kucheza mpira tunawazidi baada ya kucheza mtani jembe na kombe la Zanzibar
tumeingiza zaidi ya watakachopewa kwenye ligi kuu milioni 75 sisi tumeshinda
mechi mbili tuna milioni 120.”alijitamba Kadege.
Kwa upande
wa msemaji wa timu ya mashabiki wa Yanga, Joram George alisema kuwa ingawa
mchezo huo wamepoteza lakini wanaamini Simba hawajawazidi kitu zaidi ya
kubahatisha mchezo huo baada ya wachezaji wengi wa timu yake kuwa majeruhi
ikiwemo mlinda mlango namba moja ambapo amesema ili kudhihirisha hilo wataomba
mechi ya marudiano wadhihirishe ubabe wao wa ligi kuu.
“tumepoteza
kwa bahati mbaya tu huu mchezo lakini sisi yanga ndio kila kitu na ndio maana
wanatupigia saluti tukiingia uwanjani na huu mchezo wamebahatisha baada ya
wachezaji wetu wengi kuwa majeruhi lakini tutaomba mchezo wa marudiano na
ukweli utajitenga na uongo”
Kwa upande
wake kocha wa timu ya mashabiki hao wa Yanga kwa ujumla waliounga umoja wao wa
mwangaza maveterani, Patson Mambete alisema kuwa mchuano huo wa kirafiki
ulilenga kutoa burudani ya aina yake lakini pia kumaliza ubishi wa kila siku wa
ubabe wa watu wa Simba na Yanga hapa mkoani Arusha.
Mwisho……………………..
0 comments:
Post a Comment