wachezaji wa Arusha ryno (Tanzania- kijani) wakiwania mpira uliorushwa pamoja na timu ya Mombasa sc |
Timu ya Arusha Ryno ya Tanzania imeshindwa kutamba nyumbani
mbele ya timu ya Mombasa SC ya Kenya, baada ya kulazwa kwa point 28-26 katika
mchezo wa awali wa mfululizo wa mashindano ya Rugby yanayoshirikisha timu za nchi
za Afrika mashariki.
Arusha Ryno ilishindwa kutamba katika uwanja wake wa nyumbani
wa TGT ulioko kisongo jijini Arusha kwa mara ya kwanza mbele ya Mombasa katika
michuano hiyo ya mchezo wa Rugby ya nchi za Afrika mashariki ijulikanayo kama
“Hatch cup” iliyochezwa mapema mwishoni mwa wiki.
Timu ya Arusha ryno wakimiliki mpira |
Akizungumza baada ya michuano hiyo, Kaptein wa timu ya Arusha
Ryno, Justine Robert alisema kuwa tangu kuanza kwa mashindano hayo kwa zaidi ya
miaka mitatu hawajawahi kufungwa na timu ya Mombasa lakini kwa leo hali hiyo
imetokea hali inayowatia uchungu sana na kuahidi kufanya vizuri katika mechi ya
marudiano.
“Kiukweli hatujawahi kufungwa na hawa jamaa lakini imetokea
hivyo niahidi kwa sababu ni mechi ya awali na kuna marudiano tutafanya vema na
tutaanza mazoezi makali kwa ajili ya kuwafunga mabingwa watetezi ambao ni
“Dar-es-salaam Leopard” may 9 mwaka huu hivyo mashabiki wetu wasikate tama
kwani kombe hili la “Hutch cup” linakuja Arusha”
Kwa upande wake kaptein wa timu ya Mombasa SC, Chris Atingo
alisema kuwa wanayo furaha kwa mara ya kwanza kumfunga timu ya Arusha Ryno
kwani kwa miaka kadhaa sasa wamekuwa vibonde mbele ya timu hiyo hali
iliyowalazimu kufanya mazoezi ya usiku na mchana kuhakikisha wanakuwa mlima
mkali.
“Leo tunayo furaha kumfunga Arusha kwani miaka kadhaa sasa
wamekuwa wakitufunga hali ambayo imefikia sehem tukasema iwe mwisho na tukaamua
kufanya mazoezi usiku na mchana na matunda ya mazoezi yetu tumeyaona na
tutaendelea ili kumfunga pia dar- Leopard na Arusha tutakapomkaribisha nyumbani
kwetu Mombasa hivyo karibuni na ninyi waandishi muone vibonde wamegeuka mlima”
alisema Chris wakishangiliana na timu wenzake.
Aidha michuano hiyo ya mchezo wa Rugby inayohusisha nchi za
Afrika mashariki kwa mwaka huu zimeshiriki timu tatu za Dar, Arusha na Mombasa
yakiwa na malengo ya kuwafanya vijana chipukizi kuwaonesha mbinu za mchezo huo
katika mashindano ili waweze kuiga na kuyatekeleza ili kushinda wanaposhiriki
katika mashindano ya kimataifa ambapo timu za nchi hizi zimekubaliana
kushirikiana kukuza mchezo huu.
Awali katika mchezo wa kuwakaribisha miamba hao wa Mombasa na
Arusha, timu ya vijana wadogo chini ya umri wa miaka 15 walioko chini ya mradi
wa kuendeleza mchezo wa Rugby Arusha (Arusha Rugby Development Programme- ARDP)
waliminyana kati ya timu ya Pallot na “Young Ryno” ambapo hata hivyo pallot
waliwabigiza wenzao kwa point 24-10.
Michuano hiyo ya Rugby Hutch cup imeanza imeanza mwanzoni mwa
mwezi huu ambapo timu ya Mombasa SC waliwakaribisha mabingwa watetezi Dar-
leopard ambapo miamba hiyo ilishindwa kutambiana na kutoka suluhu ya point 12-
12 ambapo wanatarajia kurudiana jijini Dar mwishoni mwa mwezi huu wa may.
Mwisho…………….
0 comments:
Post a Comment