na Mwandishi wetu - Arusha
Uongozi wa
taasisi ya BIMO Media ya Mkoani Arusha. Umeelezea kuunga mkono hatua ya Chama
Cha Mapinduzi (CCM) kupendekeza kuwepo siku maalumu ya kuadhimisha umoja na amani
kitaifa.
BIMO pia
imeelezea kufurahishwa na hatua ya CCM kutaka kuanzisha matamasha maalumu ya
umoja na Amani yanayolenga kudumisha mshikamano nchini bila kujali itikadi za
wananchi.
Mkurugenzi
wa taasisi hiyo, Bertha Ismail Mollel amesema kuwa BIMO Media ilikuwa ya kwanza
kuandaa matamasha haya ya Amani na kwamba tukio la kwanza lilifanyika jijini
Arusha mnamo mwezi Desemba mwaka jana na kwamba kwa mwaka huu wako tayari
kabisa kuungana na Chama Tawala katika kuhakikisha kuwa matamasha ya Amani yanafanikiwa
kwa kiwango kikubwa hapo mwezi julai.
"Swala
la amani ni jukumu la kila mtu hivyo sisi tulianza tukiwa na lengo
kubwa la kuwakutanisha vijana pamoja na kuwaeleza umuhimu wa amani na
wasikubali kugawanywa kwa misingi ya dini, ukabila wala siasa pia
wasikubali kutumika kama magaidi katika nchi yao bali wajenge uzalendo
wa hali ya juu" alisema Bertha.
Wakati huhuo
huo Msajili wa vyama vya siasa nchini, Jaji Francis Mutungi ameelezea
kufurahishwa na matamasha ya Amani na hasa pale yanapowalenga vijana ambao ndio
nguvu kuu ya taifa na ndio hasa wenye jukumu la kulinda Amani na kudumisha
umoja nchini.
Hata hivyo
Jaji Mutungi amebainisha kuwa, ni vizuri pia wanafunzi wa vyuo na shule zote
nchini washirikishwe kikamilifu bila kusahasu viongozi wa dini na taasisi zake
kwani huko ndiko wananchi huwakilishwa kwa wingi.
Hivi
karibuni uongozi wa juu wa CCM ulipendekeza kuwepo na siku maalum kitaifa kwa
ajili ya kuadhimisha umoja na Amani ambapo matuniko kadhaa yakiwemo ya michezo,
matamasha ya muziki, sala maalum na mengineyo yangekuwa yanafanyika na kuwaleta
pamoja wananchi katika maeneo yote nchini kujumuika bila kujali tofauti zao za
kiitikadi na kisiasa.
Matamasha
hayo yameelezewa kuwa ni hatua muhimu ya kuwaunganisha tena watanzania hususan
katika kipindi hiki cha uchaguzi ambapo watu wengi hujikuta wamegawanyika
kutokana na kampeni za wanasiasa wanaowania nafasi na nyadhifa kadhaa nchini huku wakitumia vijana kutishia uvunjifu wa amani.
0 comments:
Post a Comment