.

.
Wednesday, May 6, 2015

2:15 AM
Bertha- Arusha

Wanariadha wa kimataifa Michael Gwandu na Michael Michael Danford wa Arusha wameanza mazoezi makali ya kuhakikisha wanavunja rekodi ya kitaifa za mbio fupi, ya kuruka chini na viunzi iliyodumu kwa zaidi ya miaka 40 sasa.

Wanariadha hao wanaojifua katika viwanja vya sheik amri abeid kwa kuruka viunzi na kuruka chini na mitupo wamesema kuwa wamekuwa mabingwa wa mchezo huo kwa miaka zaidi ya tano sasa hivyo kwa sasa mwaka huu wanajifua kwa ajili ya kuvunja rekodi ya taifa ya michezo hiyo.

“Sisi tunajinoa makali kwaajili ya kuvunja rekodi za kitaifa kwanza na baadae dunia katika mbio fupi, kuruka na mitupo ambapo mbali na kuwashinda wapinzani wetu wa mikoa mingine lakini pia ni kuvunja rekodi ya kitaifa zilizowahi kuwekwa ikiwemo ya kuruka chini iliyowekwa na Raphael Mlewa mwaka 1971”

Kwa upande wa kocha wa wanariadha hao Samweli Tupa alisema kuwa wanariadha hao wamekuwa wakichukua ubingwa wa mara kwa mara katika mashindano ya kitaifa na jumuiya ya madola lakini cha kushangaza wengi wameshindwa kuvunja rekodi zilizowekwa kipindi cha nyuma hali ambayo ameamua kuwanoa wachezaji wake wavunjerekodi hizo.

“Kuna rekodi zimewekwa miaka zaidi ya 40 sasa kama mirujko mitatu iliwekwa rekodi mwaka 1970 na John Kanondo na kuruka viunzi kwa mita 110 lakini cha kushangaza rekodi hizo hazijavunjwa licha ya kila siku kujisifia wachezaji wetu kufanya vizuri kwa kuwa wa kwanza wakati rekodi za miaka ya ukolono bado ipo”

alisema kuwa kwa sasa wanariadha hao mbali na kufanya mazoezi ya peke yao pia watashiriki katika mashindano mbali mbali ikiwemo ya may 25 ya kitaifa itakayochagua wachezaji watakaowakilisha nchi katika mashindano ya wazi ya Uganda mwezi june.

Hata hivyo kochaTupa aliiomba serikali kusaidia mchezo huo kama awali ili uweze kuendelea kurudi na medali nyingi na kuvunja rekodi za dunia kama awali na kusema kuwa Tanzania inashindwa kufanya vizuri kutokana na kukosekana kwa sapoti kutoka serikalini kama ilivyokwa nchi kama Kenya, Unganda, n.k.



mwisho…………….

0 comments:

Post a Comment