Arusha . Timu ya
maafande wa Jkt Oljoro inayoshiriki ligi daraja la kwanza Tanzania bara
inatarajia kuchuana vikali na ndugu zao timu ya Arusha FC katika ufunguzi wa
ligi maalum ya Nyerere cup inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi septemba 10 jiji
Arusha.
Tiyari timu
ya Arusha fc na Jkt Oljoro zimethibitisha kushiriki michuano hiyo huku kila
mmoja akijitamba kuonyesha ubabe dhidi ya mwenzake na pia wakitumia mechi hiyo
kutambulisha wachezaji wao kwa wapenzi wa Soka wa jiji Arusha.
Mechi hiyo
ya ufunguzi kati ya Oljoro na AFC itakayochezwa jioni katika uwanja wa Sheik Amri Abeid, ni kwa
ajili ya kufungua michuano ya Nyerere cup itakayoshirikisha Jumla ya timu Sita za vijana
chini ya umri wa miaka 13, lengo kubwa ikiwa ni kumuenzi muasisi wa Taifa hili
Hayati Mwl, Julius K. Nyerere.
Akizitaja
timu shiriki katika ligi hiyo, mratibu wa maadhimisho hayo Bertha Ismail
alisema kuwa ni pamoja na Nyota Accademy, Future Star, Kijenge Youth zingine ni
Rolling stone, Young Life na Pallot.
“Maadhimisho
haya huwa yanafanyika Octoba 14 kila mwaka lakini kwa mwaka huu tunafanya mwezi
Septemba ili maadhimisho haya yasiathiriwe na zoezi la Uchaguzi ambapo pamoja
na kumuezi Muasisi wa Taifa letu lakini ligi hii pia inalenga kuhasisha
wananchi wafanye uchaguzi kwa amani bila vurugu ili sekta ya utalii hapa nchini
izidi kukua”
“Katika
maadhimisho haya yatakayofunguliwa na mkurugezi wa jiji la Arusha Iddi Juma
yana “kauli mbiu ni Uchaguzi wa amani 2015: Taifa Moja kwa Maendeleo ya utalii”
ambapo wadau mbali mbali wa maendeleo ya nchi yetu na utalii kwa ujumla
watahudhuria ufunguzi na kilele ambayo ni septemba 19 na atakaefunga ni mkurugenzi
wa hifadhi ya Taifa (TANAPA) Allan
Kijazi”
Bertha Alisema kuwa michuano hiyo ni utangulizi tu wa mashindano ya uandishi na uchoraji wa insha kwa wanafunzi 700 kutoka shule shule 25 za jiji la Arusha zitakazofanyika septemba 19 katika viwanja vya makumbusho jijini Arusha mashindano yaliyodhaminiwa na TANAPA, PALACE HOTEL, AICC, Bonite botllets, jiji la Arusha na TBL.
Mwisho…………..
0 comments:
Post a Comment