mwandishi wetu -Arusha
TIMU ya Maafande
wa JKT Oljoro ya jijini Arusha inayoshiriki ligi daraja la kwanza imeshindwa
kuonyesha makali yake mbele ya wadogo zao
timu ya AFC Arusha inayoshiriki ligi daraja la pili baada ya kutoka suluhu
ya bao 1-1 katika ufunguzi wa michuano ya Nyerere Cup 2015.
Mchezo huo
uliofanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid, uliwashuhudia maafande hao wa
Oljoro wakianza kucheka na nyavu za AFC baada ya kujipatitia bao lake kupitia
kwa mchezaji Swalehe Idd alilofunga kwa njia ya Penalti mnamo dakika ya 58,
iliyosababishwa na mabeki wa timu pinzani kunawa mpira katika eneo la hatari.
Vijana wa
AFC walionyesha juhudi zao kwa kulishambulia lango la Oljoro ambapo
walifanikiwa kusawazisha bao mnamo dakika ya 88 kupitia kwa mshambuliaji wao
Wandima Malechela baada ya kuachia shuti
kali lililokwenda moja kwa moja vyavuni.
Ufunguzi huo ni
utangulizi tu wa Mashindano ya vijana chini ya umri wa miaka 13
yaliyoandaliwa na kampuni ya BIMO Media yenye kauli mbiu "Uchaguzi wa
Amani 2015, ndio taifa moja kwa maendeleo
ya utalii nchini" na yatafikia kilele siku ya kilele
tarehe 19 mwezi huu katika viwanja vya Makumbusho Arusha.
Akifungua
mashindano hayo kwa niaba ya mkurugenzi wa jiji la Arusha Idd Juma,
Afisa Elimu jiji la Arusha kwa shule za sekondari Josephat Ntabindi
alieleza kuwa mashindano hayo ni humimu hasa kwa watoto hao wenye vipaji
kuonyesha uwezo wo huku wakikuza uelewa kwa vijana wadogo na kumuenzi
hayati baba
wa taifa Mwl Julias Nyerere ambaye pia alikuwa mstari wa mbele katika
kuhamasisha
michezo hadi kugharamia kambi za timu ya Taifa kitendo ambacho kwa sasa
hakipo.
Naye
mkurugenzi wa kampuni ya mawasiliano ya Bimo Media Bertha Ismail alisema maadhimisho hayo yataambatana na mashindano
ya kila mwaka ya ki- elimu ya uandishi wa insha,makala pamoja na
uchoraji picha juu ya masuala ya utalii kwa wanafunzi wa shule za msingi 25
zilizopo Arusha.
“ Lengo
ni kuhamasisha uchaguzi wa mwaka
huu kufanyika kwa amani vile vile
kuhamasiha watu kuhudhuria hifadhi za
utalii zilizoasisiwa na Mwl Nyerere na tunategemea Zaidi ya wanafunzi 700
watashiriki katika shindano hilo la
isha.”ismail alifafanua.
Timu za
nyota academy,Future Stars,Kijenge Youth,Rolling Stone,Young Life na palloti
zitachuana na washindi watakabidiwa zawadi mbalimbali ikiwemo vikombe na fedha.
0 comments:
Post a Comment