.

.
Sunday, November 4, 2012

8:40 AM
Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete (katikati) akiwa na  waziri wa ujenzi Dr John Magufuli (kulia) na kushoto ni mwakilishi wa benki ya dunia Philip ambao ndio wazamini wakubwa wa mradi huo wa barabra
Rais Kikwete akisalimiana na mkuu wa wilaya ya Karatu Mh, Daudi Felex Mtibenda (Kijiko) huku mkuu wa wilaya ya Ngorongoro Elias Wawa Lali akiusubiri kwa ham mkono huo wa salamu punde baada ya Rais kutua katika viwanja vya uzinduzi wa barabara

RAIS wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, amemsifu Waziri Mkuu mstaafu na Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, kuwa ni mbunge hodari sana, hivyo atashirikiana naye kumaliza tatizo la maji katika wilaya hiyo.


Rais Kikwete alitoa sifa hizo kwa Lowassa jana wakati akihutubia wananchi eneo la Nanja, Kata ya Monduli, kabla ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa barabara ya Minjingu –Arusha uliogharim zaidi ya bilioni 98.

Rais Kikwete (kulia) akipewa kamba na mtumishi wa TANROAD kama zawadi ya ngo'ome wawili jike na dume Wakati wa uzinduzi wa barabara hiyo ya minjungu
Rais Kikwete akipanda mti wa ukumbusho baada ya uzinduzi wa barabara ya minjingu
Mkuu wa Mkoa Magessa Mulongo ( kushoto) naye alipanda mti kama ukumbusho wa barabara hiyo ya minjingu
Mea wa jiji la Arusha Gaudiece Lyimo akinawa mikono baada ya kupanda mti wake wa ukumbusho baada ya zoezi hilo kuanzishwa na Rais Kikwete
.


                                                                                                                             
Katibu wa vijana CCM mkoa (UVCCM) Mh, Salum Kidima akiwa na (kulia) akiwa na mwenyekiti wa UWT wilaya ya Monduli, bi. Mariam na vijana wengine wa umoja huo wakiwa na nyuso za tabasam kusubiri kwa Rais kuwepo mkoani hapa
Mmiliki wa blog hii ya BERTHA BLOG, Bertha Isamail (kushoto), akisalimiana na Rais Kikwete katika uzinduzi wa barabara ya Minjingu
                                                             

0 comments:

Post a Comment