Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed
Shein,akimuapisha Bw.Vuai Mwinyi Mohamed,kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kati
Unguja,Ikulu Mjini Zanzibar leo .[Picha na Ramadhan Othman Ikulu.]
RAIS
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed
Shein leo amemuapisha Bwana Vuai Mwinyi Mohammed kuwa Mkuu wa Wilaya ya
Kati Unguja.
Hafla
hiyo ilifanyika Ikulu mjini Zanzibar na kuhudhuriwa na viongozi mbali
mbali akiwemo Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe. Pandu Ameir Kificho,
Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe.Omar Othman Makungu na Mkuu wa Mkoa wa Mjini
Magharibi Mhe. Abdalla Mwinyi Khamis.
Wengine
waliohudhuria katika hafla hiyo ni Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis
Haji, Meya wa Manispaa ya Mji wa Zanzibar, Mstahiki Khatib Abdulrahman
Khatib, Washauri wa Rais pamoja na viongozi wengine wa Serikali.
0 comments:
Post a Comment