Pages

Pages

Thursday, February 21, 2013

AZAM YAZIDI KUINYIMA USINGIZI YANGA, SIMBA YAZINDUKA MBEYA

Mcha Vialli; Mfungaji wa mabao mawili ya Azam leo

Na Prince Akbar
AZAM FC imezidi kuitia presha Yanga kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, kufuatia ushindi wa mabao 4-0 jioni ya leo dhidi ya JKT Ruvu kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
Matokeo hayo yanaifanya Azam FC itimize pointi 36, baada ya kucheza mechi 17 pia, moja zaidi ya Yangana sasa ina mabao 31 ya kufunga na 14 ya kufungwa.
Yanga inaendelea kuongoza msimamo wa Ligi Kuu, kwa wastani wake mzuri wa mabao, ingawa ina pointi sawa na Azam, 36, baada ya kucheza michezo 16, ikiwa imeshinda 11, imetoka sare tatu na kupoteza miwili, huku ikiwa imefunga jumla ya mabao 33 na kufungwa mabao 12 tu.
Kocha wa Yanga, Mholanzi Ernie Brandts alikuwepo kwenye Uwanja wa Chamazi leo kuishuhudia Azam, ambayo watacheza nayo Jumamosi ikiendeleza dozi za ‘nne nne’, kwani na mechi iliyopita, Wana Lamba Lamba pia waliilaza Mtibwa Sugar 4-1.
Hadi mapumziko, Azam walikuwa tayari mbele kwa mabao 2-0, yaliyotiwa kimaini na kiungo Khamis Mcha ‘Vialli’ na mshambuliaji John Bocco ‘Adebayor’.
Mtoto wa Kizanzibari, Mcha ‘Vialli’ ndiye aliyefungulia biahsara Azam kwa bao lake la mapema dakika ya pili, akiunganisha krosi ya kiungo aliyerudishwa kwenye safu ya ulinzi, beki ya kulia Himid Mao. 
JKT walipata nafasi ya kusawazisha bao dakika ya 10, baada ya kupata penalti, kufuatia kipa wa Azam, Mwadini Ally kumchezea rafu Samuel Kamuta, lakini mkwaju wa Kisimba Luambano ukapanguliwa na kipa huyo wa Lamba Lamba.
Baada ya kosa hilo, Azam haikusita kuwaadhibu Maafande hao na alikuwa ni mshambuliaji tegemeo wa timu hiyo, John Raphael Bocco aliyefanya kazi hiyo dakika ya 44 na ushei, alipoifungia timu yake bao la pili akimalizia pasi ya kiungo Mkenya, Humphrey Mieno. 
Kipindi cha pili, Azam walirudi na moto wao na kufanikiwa kupata mabao mawili zaidi.
Mtoto wa Kizenji, Mcha Vialli alifungua tena biashara kipindi hicho mapema tu dakika ya kwanza ya kipindi hicho, akifunga kwa shuti kali, baada ya kupokea pasi maridadi ya Bocco Adebayor.
Karamu ya mabao ya Azam leo hii ilihitimishwa na dakika ya 72 na kiungo Abdi Kassim Sadallah ‘Babbi’, aliyeingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Bocco Adebaor, ambaye alifunga bao la nne kwa shuti kali baada ya kupokea pasi ya Seif Abdallah, aliyeingia pia kipindi hicho kuchukua nafasi ya Kipre Tchetche.
Katika mchezo huo, kikosi cha Azam kilikuwa; Mwadini Ali, Himid Mao, Waziri Salum, David Mwantika, Joackins Atudo, Jabir Aziz, Kipre Tchetche/Seif Abdallah dk 67, Ibrahim Mwaipopo/Gaudence Mwaikimba dk81, John Bocco ‘Adebayor’/Abdi Kassim ‘Babbi’ dk71, Humphrey Mieno na Khamis Mcha ‘Vialli’. 
JKT Ruvu: Shaaban Dihile, Mussa Zuberi, Kessy Mapande, Kisimba Luambano/Hussein Dumba dk60, Damas Makwaya, Jimmy Shoji, Amos Mgisa/Emmanuel Pius dk 70, Nashon Naftal, Samuel Kamuta, Mussa Mgosi/William Sylvester dk60 na Hussein Bunu.
Kiemba; Mfungaji wa bao la Simba SC leo
Katika mechi nyingine za ligi hiyo, Simba SC leo ilizinduka baada ya sare mbili mfululizo na kufanikiwa kushinda 1-0 kwenyer Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya, bao pekee la kiungo Amri Ramadhan Kiemba dakika ya 36. Kwa ushindi huo, Simba imefikisha pointi 31 baada ya kucheza mechi 17.
Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga, Coastal Union imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya JKT Oljoro, mabao ya Suleiman Kassim ‘Selembe’ dakika ya 12 na Jerry Santo dakika ya 57, wakati Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza, mabao ya Freddy Lewis dakika ya 26 na Benedict Mwamlagala dakika ya 89, yameipa African Lyon ushindi wa 2-0 dhidi ya wenyeji Toto African.

YANGA WAINDEA AZAM FC BAGAMOYO


VINARA wa Ligi Kuu ya Vodacom, Yanga wameamua kwenda kambini mjini Bagamoyo kujiandaa na mechi yao dhidi ya Azam itakayochezwa Jumamosi ya wiki hii kwenye uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa habari zilizopatikana jana kutoka ndani ya klabu hiyo yenye maskani yake makutano ya motaa ya Twiga na Jangwani, wamekwenda huko kutokana na wachezaji kuhitaji mazingira bora na yenye utulivu.
Chanzo hicho kimedokeza kwamba, kutokana na ugumu wa mechi hiyo itakayozikutanisha timu zinazoshika nafasi mbili za kwanza katika logi hiyo, inatarajiwa kuwa yenye ushindani mkubwa.
“Unajua Azam ipo vizuri sana, imekuwa ikitoa upinzani mkubwa hasa inapokutana nasi. Tumeona ni bora wachezaji wakienda kufanya maanmdalizi tukiwa nje ya Dar es Salaa, tukiamini wachezaji watapata nafasi ya utulivu,” kilisema chanzo hicho.
Mechi hiyo inatarajiwa kuwa na upinzani mkubwa kwani kila timu itahitaji kushinda ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kutwaa ubingwa wa ligi hiyo iliyoanza Septemba 15.
Wakati Yanga ikitaka kutwaa taji la 23 tangu kuanza kwa ligi ya taifa mwaka 1965, Azam inasaka ubingwa wa kwanza tangu kuanzishwa kwake Juni 24, mwaka 2007.
Yanga inayoongoza ligi hiyo kwa pointi 36, itakuwa ikisaka ushindi ili kuendeleza ubabe wao kwa timu hiyo kama ilivyokuwa kwenye raundi ya kwanza ya ligi hiyo ambapo Azam ilifungwa 2-0, yakifungwa na Didier Kavumbagu na Hamis Kiiza.

FIFA YAUPIGA STOP UCHAGUZI TFF

Tenga akizungumza na Waandishi wa Habari mchana wa leo TFF. Kushoto ni Boniface Wambura, Ofisa Habari wa shirikisho hilo

Na Boniface Wambura
SHIRIKISHO la Soka Kimataifa (FIFA) limeahirisha uchaguzi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kutokana na mkanganyiko uliojitokeza katika mchakato wa uchaguzi huo.
Akizungumza na Waandishi wa Habari katika ofisi za TFF, zilizopo ndani ya Uwanja wa Karume, Dar es Salaam leo mchana, Rais wa TFF, Leodegar Tenga amesema FIFA imetuma barua ikiagiza mchakato wa uchaguzi usimame baada ya kupata malalamiko.
Amesema kutokana na mkanganyiko huo, FIFA katika barua yake ya leo, imeagiza mkutano wa uchaguzi wa TFF ambao awali ulipangwa kufanyika Februari 24 mwaka huu uahirishwe hadi hapo itakapotuma ujumbe wake nchini.
Ujumbe huo wa FIFA unatarajiwa kufika nchini katikati ya mwezi ujao (Machi) ambapo utafanya tathimini ya hali hivyo, kutuma ripoti yake katika shirikisho hilo na baadaye kutoa mwongozo wa nini kifanyike.
Rais Tenga amewaomba radhi wajumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF kwa usumbufu uliojitokeza kutokana na uamuzi huo wa FIFA, hivyo kwa sasa hakutakuwa tena na mkutano huo mpaka hapo watakapopewa taarifa nyingi.
Amesema TFF inakaribisha kwa mikono miwili uamuzi huo wa FIFA kwa sababu ni chombo ambacho cha juu kimpira duniani, na hatua hiyo ina lengo la kuhakikisha kuwa kila mhusika katika mchakato huo wa uchaguzi anapata haki yake.
“Nia yetu ni kuona watu wanatendewa haki, na nia ya FIFA ni kutafuta ukweli. Hivyo wahusika (waathirika) wajiandae, watumie wakati huu kuandaa hoja zao ili FIFA wakifika wawasikilize, wapate maelezo ya kina kuhusu utaratibu na malalamiko yaliyotolewa,” alisema Tenga.
Rais Tenga amesema timu hiyo ya FIFA itakapofika yenyewe ndiyo itakayopanga izungumze na nani kwa wakati gani, hivyo ni vizuri waathirika na vyombo vyote vilivyohusika na mchakato wa uchaguzi wakajiandaa.
Amesema ilikuwa ni muhimu suala hili likatatuliwa katika ngazi ya FIFA kwa lengo la kuhakikisha uchaguzi utakapofanyika TFF inaendelea kuwa chombo kimoja badala ya kurudi katika migogoro iliyokuwepo huko nyuma.
“Nataka tubakie kama tulivyokuwa. Malumbano yaishe. Pangeni hoja, wakija hao waheshimiwa (FIFA) muwaambie. FIFA ni chombo cha juu, nafurahi wamekubali kuingia katika hili, kwani wana shughuli nyingi wangeweza kukataa,” amesema.
Kuhusu fursa ya kufanya marejeo (review) kwenye Kamati ya Rufani ya Uchaguzi inayoongozwa na Idd Mtiginjola ambayo aliielezea Jumamosi, Rais Tenga amesema kwa vile hicho ndicho chombo cha mwisho nchini katika masuala ya uchaguzi alishauriwa kuwa kingeweza kufanya review.
“Kwa vile hakuna chombo kingine, nikashauriwa kuwa kinaweza kufanya review. Katika utaratibu wa kutoa haki, uamuzi ni lazima uwe wa wazi kwa kutoa sababu. Nilidhani hilo linawezekana, kwani Mahakama Kuu hufanya hivyo. Kwa hili uamuzi wa Mtiginjola ni sahihi,” amesema Rais Tenga.
Kamati ya Mtiginjola iliyokutana jana (Februari 18 mwaka huu) ilitupa maombi ya review yaliyowasilishwa mbele yake na waombaji uongozi watano kwa vile hakuna kipengele chochote kwenye Katiba ya TFF na Kanuni za Uchaguzi kinachotoa fursa hiyo.
Waombaji hao walikuwa Jamal Emil Malinzi aliyeenguliwa kugombea urais wa TFF na Hamad Yahya aliyeondolewa kwenye kinyang’anyiro cha kuwania uenyekiti wa Bodi ya Ligi Kuu (TPL Board).
Wengine ni walioomba kuwania ujumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF na Kanda zao kwenye mabano; Eliud Peter Mvella (Iringa na Mbeya), Farid Salim Nahdi (Morogoro na Pwani) na Mbasha Matutu (Shinyanga na Simiyu).

BAADA YA MAUWAJI YA PAROKO ZANZIBAR , ASKOFU MDEGELA AFICHUA SIRI NZITO


          Askofu Dkt Mdegela

ASKOFU wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi
yaIringa, Dk. Odernbarg Mdegela, ametoboa siri nzito kuhusu
uhalifu unaoendelea nchini, yakiwemo mauaji ya viongozi wa kidini na
uharibifu wa nyumba za ibada, kwamba upo nyuma ya vikundi kadhaa
vilivyopatiwamafunzo maalumu nje ya nchi kwa ajili ya utekelezaji wa
mpango huo.

Ingawa hakuvitaja moja kwa moja vikundi hivyo vinavyofadhiliwa
ilikutekeleza mkakati huo, Askofu Mdegela amedai kwamba vikundi
hivyo,vimepata mafunzo hayo na kwamba lengo ni kukamilisha mkakati
huo.

Kufuatia hali hiyo, Mdegela amewaandikia waraka, wanachama wote
waJumuiya ya Makanisa ya Kikristo nchini (CCT) kuanza mara moja
mfungowa saa 24 kuanzia leo (Maombi ya mnyororo), kusali dhidi ya
uhalifuhuo kwa minajili ya kuwasaidia makachero kutoka ndani na nje ya
nchikuwabaini wanaotekeleza mkakatihuo.

Dk. Mdegela alitoboa siri hiyo leo wakati akizungumza na Waaandishiwa
Habari katika kanisa kuu la kkkt lililopo eneo la Miyomboni sokoni
Manispaa ya Iringa.

”Vikundi hivyo vinataka kuichafua serikali,kuuvunja muungano na
kuifanya Zanzibar kuwa nchi  ya kidini. Serikali ichukue au isichukue
hatua, sisi tunakwenda madhabahuni na ndio maana nimeitisha maombi kwa
makanisa yote ambayo ni wanachama wa CCT,

...Ingawa matamko haya, hayawezi kumaliza tatizo isipokuwa tutasugua
goti ili kudhihirisha nguvu ya maombi,”Alisema Mdegela aliyekuwa
ameongozana na wachungaji na baadhi ya wakuu wa majimbo ya KKKT.

Kuhusu usalama wa makanisa yaliyopo chini ya KKKT na CCT, Askofu
Mdegela ameagiza kila kanisa liimarishe ulinzi kila kona kutokana na
mkakati unaotekelezwa kwa kificho na vikundi vinavyoshukiwa.

”Naagiza wekeni ulinzi kuanzia geti la mbele, la nyuma na kwenye
kengele ili wakitokea watu hao, walinzi wapige kengele na kupambana
nao. Huu ni wakati wa wakristo wote nchini kuingia na kuzama katika
maombi ya mnyonyoro kuomba amani na kuepusha vurugu za kidini
zinazoendelea nchini hivi sasa,”Alionya askofu huyo.

Alifafanua kuwa vurugu hizo, zinatokana na baadhi ya vikundi vya
kidini ambavyo amedai kwamba vinafadhiliwa na nchi zenye msimamo mkali
kutaka kuueneza dini mojawapo kwa nguvu bila kufuata utaratibu  na
sheria za uenezaji.

Askofu Mdegela amewataka wakristo kwa muda uliopo kuutumia katika
maombi na kutojiingiza katika kuonesha tofauti za ukristo bali ni
wakati wa kuungana kwa pamoja na kuingia katika maombi kwa kipindi
chote kwa ajili ya amani na utulivu.
Aliyataja matukio ya kuuawa kwa Mchungaji wa Kanisa wa kanisa la
kiroho katika mkoa mpya wa Geita,kuuawa kwa Padri Evarist
Mushi,kushambuliwa kwa risasi mwilini kwa Paroko Ambrose Mkenda,uchomaji
moto nyumba za ibada na uharibifu wa mali za makanisa kadhaa nchini ni
matokeo ya mkakati huo.

"Kanisa limeingia katika mateso na tumesema hatutalipiza isipokuwa
tunakwenda madhabahuni na kupiga tukiomba maombi ya mnyororo na
tutashinda,"Alisisitiza Mdegela.

 wanataka nchiyetu isitawalike tuwekama nchi zisizo na amani duniani.
  Tunaimani umojaninguvu utenganoniudhaifu.
 

NYUMBA MILIONI 3 ZINAHITAJIKA TANZANIA


Shirika la nyumba la Taifa limeweka mikakati ya kupunguza mahitaji ya nyumba zaidi ya milioni 3 hapa nchini kwa kuhakikisha wanajenga nyumba zaidi ya elfu 3 kila mwaka.
Hali itakayowasaidia watanzania wengi kumiliki nyumba zao.
`          
Hayo yamelezwa na Waziri wa Ardhi,nyumba, na maendeleo ya
makazi,Profesa Anna Tibaijuka hivi karibuni  wakati akizundua mradi wa nyumba za
makazi katika eneo la Levolosi ambazo zimejengwa chini ya Shirika la
nyumba sambamba na hoteli ya palace iliyojengwa kwa ubia wa NHC pamoja kampuni ya palace.
Tibaijuka alisema kuwa  mahitaji hayo ya nyumba kila mwaka
yanaongezeka kwa kiasi cha nyumba laki tatu lakini ongezeko hilo ni
lazima liweze kupunguzwa tena kwa haraka sana kwa kubuni aina
mbalimbali ya nyumba ambazo zitarahisisha makazi bora na imara

Aliongeza kuwa Hitaji ni kubwa sana la nyumba hapa nchini hivyo
jitiada za haraka sana zinahitajika katika kuhakikisha kuwa hata
nyumba ambazo zinajengwa ziweze kuwa imara na ziweze kuwasaidia hata
zaidi wananchi wa vijiijini ambao mara nyingine wanaonekana kukosa
nyumba bora na imara

Alisema kuwa kama Shirika hilo amblo kinaendeshwa lenyewe litaweza
kuwa bunifu na kujenga nyumba nyingi zaidi basi litachangia kwa
kiwango kikubwa sana ongezeko hilo la nyumba zaidi ya Laki tatu kwa
kila mwaka kuweza kupungua na hata baadhi ya miji kuweza kupangika kwa
uraisi sana

“Tanzania kwa sasa tunakabiliwa na changamoto hii lakini ni vema sasa
Shirika kwa kushirikiana na wadau mbalimbali tukahakikisha kuwa
tunasonga mbele zaidi na hata kuangalia jinsi ya kupunguza tatizo hilo
ambalo kama halitaaweza kutatuliwa kwa uraisi basi litasababisha
madhara kwa kuwa wapo baadhi ya watu ambao watakosa sehemu za
kuishi’aliongeza Tibaijuka

Katika hatua nyingine alisema kuwa nao wanasiasa wana nafasi kubwa
sana ya kushirikiana na Shirika hilo kwa kuwa bado shirika hilo
linakabiliwa na changamoto mbalimbali kama vile kushindwa kujenga
kutokana na Ardhi ambayo inauwza kwa bei ya juu sana lakini kama
watasaidiana basi wataweza kutatua changamoto hiyo ambayo nayo
inafanya shirika hilo kushindwa kuendelea kujenga nyumba nyingi zaidi

Awali mkurugenzi mkuu wa Shirika hilo Nehemia Mchechu alisema kuwa ili
kukabiliana na tatizo hilo la ongezeko la mahitaji ya Nyumba  hapa
Nchini Shirika hilo limeweka mikakati mbalimbali ya kuhakikisha kuwa
mpaka 2014 watakuwa tayari wameshajenga nyumba 15,000.

Mbali na hayo alisema kuwa kwa Mkoa wa Arusha wanatarajia kuanza
kujenga nyumba za garama nafuu katika wilaya ya Arumeru pamoja na
Arusha huku lengo halisi likiwa ni kuhakikisha kuwa mji wa Arusha
unaendelea kuboreka zaidi kwenye hadhi za kimataifa na kuachana na
ujenzi holela ambao mara nyingine unasababisha ukosefu wa nyumba.

Alisema nyumba hizo zitajengwa  maeneo ya Arusha,Dar es Salaam, Mbeya ,Mwanza na
sehemu mbalimbali za Tanzania ambapo  NHC imepata ekari 3000 Wilayani Arumeru Mashariki, eka 600 eneo la Burka na Arusha Mjini hivyo wanaeka 28,000 na kwa nchi nzima ambayo ni kwaajili ya kuendeleza miradi mbalimbali ya ujenzi.

Naye Mkurugenzi wa Hoteli ya Palace Jijini Arusha,  Hans Macha alisema
kuwa hoteli hiyo yenye ubia na shirika la nyumba na kampuni ya palace ilianza kujengwa rasmi mwaka 2008 na kumalizika 2011 ambapo liligharimu jumla ya shilingi bilioni 16 za kitanzania na wanatarajia kuajiri wafanyakazi rasmi 120 na wengine wasio rasmi.

Kwa upande wake mwenyeji wa waziri huyo ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Arusha mjini Godbless Lema aliishukuru shirika hilo na uongozi wa Palace kwa kujenga hoteli hiyo na kuahidi kutunza Amani ya Jiji ili kupata wageni wengi zaidi na kuwataka viongozi wa Mkoa kutenda haki itakayotekeleza upatikanaji wa Amani hiyo.

“Kwa kiongozi yoyote maendeleo kama haya ni ya kufurahia na kujivunia hivyo niwapongeze wote waliofanikisha mradi huu na naahidi kudumisha amani ili kupata wageni wengi zaidi wa kuja kutalii….., lakini siku zote Amani hupatikana kwenye haki hivyo haki ikitendeka Amani huja bila kipingamizi hivyo niombe tu haki itendeke kwa wananchi wetu ili Amani hii iendelee kuwepo.” Alisema Lema




MWISHO

maafisa vijana ni muhimu katika halmashauri zetu


WAZIRI  wa habari,michezo na Utamaduni,Dkt Fenela Mkangara amezitaka
Halmashauri zote ndani ya mkoa wa Arusha kuhakikisha kuwa zinajiwekea
utaratibu wa kuwa na maafisa Vijana hali itakayowasaidia kuwaunganisha vijana katika  kujadili kwa pamoja changamoto mbalimbali zinawakabili vijana
“zipo Halamshauri ambazo zinakabiliwa na masuala ya changamoto za
Vijana lakini hakuna afisa yoyote ambaye  ana uwezo wa kutatua kero za
vijana hivyo asilimia kubwa ya vijana wanabaki wakiwa  wanalalamika
ovyo juu ya Serikali”

Mkangara aliyasema hayo wiki hii Jijini hapa wakati akiongea na
viongozi mbalimbali wa Jiji la Arusha akiwemo Mkuu wa Wilaya kuhusiana
na maendeleo ya Vijana pamoja na changamoto,utatuzi wake kwa kipindi
miaka iliyopita.

Dkt Fenala alisema kuwa endapo kama Halmashauri zote za Jiji la
Arusha zitaweza kuwatumia vema hao maafisa Vijana basi zitachangia
sana maendeleo ya Vijana kwa kuwa asilimia kubwa ya vijana wa sasa
wanabaki wakiwa wanalamikia Serikali  kwa kushindwa kuyajua na
kuyatambua mambo ambayo si la kweli

Alisema kuwa kupitia Maafisa Vijana hao ambao wataweza kutatua
changamoto ikiwa ni pamoja na kuweka mikakati mbalimbali ya vijana ikiwemo ajira
lakini kwa kuwa  kwa sasa hakuna maafisa hao basi Halmashauri zinajitamba
kuwa zinawasaidia vijana hao huku vijana huko mitaani bado wanakabiliwa
na changamoto nyingi sana.

“Wizara yangu imeweka mikakati ya kuondoa matatizo ya vijana lakini
halmashauri pekee haziwezi hii kazi ni nzito jamani ni lazima
mtekeleze ahadi Raisi ya kuwa na maafisa Vijana ambao wataweza
kutukusanyia hawa vijana na kisha hata kama tunakitu cha kuwapa tuweze
kuwapata kwa ukaribu sana na pia hii itasaidia sana vijana hawa waache
kulalamika ovyo:”aliongeza Dkt Fenela

Awali Mkuu wa Wilaya ya Arusha, John Mongela alisema kuwa tatizo kubwa
la vijana hasa wa mkoa wa Arusha wanachokitaka kikubwa sana ni Pesa na
wala sio mawazo mazuri ya upataji  wa pesa na mitaji imara hivyo bado
asilimia kubwa sana ya Vijana wanabaki wakiwa wanalalamikia Serikali

Mongela alisema kuwa hali hiyo inasababisha vijana kuona kuwa Serikali
haiwathamini,lakini bado Jiji la Arusha limeweka mikakati mbalimbali
ya kuhakikisha kuwa inawapa fursa vijana wa mkoa wa Arusha sanjari na
kuwaboreshea mazingira mazuri na imara ya kufanyia biashara zao pamoja
na shuguli za kila siku.

MWISHO

Tuesday, February 19, 2013

LOWASSA APIGWA CHINI UVCCM

BARAZA Kuu la Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), jana lilitangaza majina mapya ya Wajumbe wa Baraza la Wadhamini, huku likiweka kando jina la Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kikao cha baraza hilo kilichofanyika mjini Dodoma mwishoni mwa wiki, Katibu Mkuu wa UVCCM, Martin Shigela alisema nafasi ya Lowassa aliyekuwa Mwenyekiti kwa miaka 10, inachukuliwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (pichani).

Shigella aliwataja wajumbe wengine walioteuliwa kuwa ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, Naibu Waziri wa Fedha, Janeth Mbene, Waziri wa Nchi (Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar), Mohamed Abood, Waziri asiye na Wizara Maalumu Zanzibar, Machano Othman Said na Mbunge wa Kikwajuni Hamad Masauni.

Shigela alisema katika kuteua wajumbe hao, kikao hicho cha UVCCM kilizingatia uwezo wao katika ushawishi na kuwaunganisha vijana “bila ya kuwapo kwa makundi.” Hata hivyo, hakufafanua maana ya makundi hayo.

Kuondolewa kwa jina la Lowassa ni pigo jingine kwa mwanasiasa huyo ambaye amekuwa akitajwa kuwa miongoni mwa wanaotaka kuwania urais kupitia CCM katika Uchaguzi Mkuu ujao. Jina lake pia halikupendekezwa miongoni mwa wagombea wa ujumbe wa Kamati Kuu (CC) ya CCM katika uchaguzi uliofanyika wiki iliyopita.

Lowassa alikuwa ameanza kuibuka tena kisiasa kutokana na kambi yake kupata ushindi mkubwa katika mchakato wa chaguzi za ndani za chama hicho zilizowaingiza wafuasi wake wengi kwenye nafasi za Ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) na katika jumuiya za chama hicho.

Wajumbe wengine walioachwa ni Nazir Karamagi, Dk Mary Nagu, Yusufu Ame Yusufu na Said Abuu.

Kwa upande wa Dk Nchimbi, nyota yake ya kisiasa inaonekana kung’ara kiasi cha kuanza kutajwa kuwa mmoja wa makada wa CCM wanaoweza kuteuliwa kumrithi Rais Jakaya Kikwete kupitia chama hicho katika Uchaguzi Mkuu wa 2015.

Katika uchaguzi huo wa Kamati Kuu ya CCM, Dk Nchimbi alichaguliwa kuwa mjumbe pamoja na wenzake sita kutoka Tanzania Bara, baada ya kupendekezwa na Rais Kikwete kuwania nafasi hiyo.

Itakumbukwa kwamba miaka 10 iliyopita, Dk Nchimbi katika kipindi chake cha pili cha Uenyekiti wa UVCCM, ndiye aliyependekeza jina la Lowassa kuwa mwenyekiti wa baraza hilo, mpango ambao ulipingwa na baadhi ya wanachama wakiongozwa na Nape Nnauye ambaye hivi sasa ni Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM.

Nape alifikia hatua ya kufukuzwa ndani ya jumuiya hiyo na hata alipotaka kukata rufaa alijibiwa na aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM, wakati huo Yusuph Makamba kwamba asingeweza kurejeshwa katika jumuiya hiyo, hata kama angekata rufaa mbinguni.

Kikao hicho cha Baraza Kuu la UVCCM, pia kiliteua wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji ambao ni Daud Njalu, Reuben Sixtus, Seki Kasuga, Amina Mkalipa na Mariamu Chaurembo ambao wanaingia kupitia Bara. Kwa upande wa Zanzibar waliopata nafasi hizo ni Shaka H Shaka, Bakari Vuai, Nadra Mohamed, Viwe Khamisi na Ali Nasoro.

chanzo :mwananchi

WANACHAMA WA CCM KUHAMIA CHADEMA SOON

WANACHAMA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Kijiji cha Shambarai Simanjiro Mkoa wa Manyara wametishia kuhama chama hicho baada ya baadhi ya viongozi wa kijiji hicho kudaiwa kuuza maeneo ya wazi bila utaratibu.

Wakizungumza na waandishi wa habari juzi,wanachama hao waliogoma kutaja majina yao, walisema wamefikisha kilio chao kwa uongozi wa CCM wa kata hiyo kwa kuwa viongozi wa kijiji wameto CCM lakini hakuna hatua zilizochukuliwa.

Walisema Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji hicho,Edward Wazi na Ofisa Mtendaji wa kijiji hicho, Mosses Peter wamewauzia sehemu ya malisho matajiri kutoka Arusha bila kufuata utaratibu wa kuidhinishwa na mkutano wa kijiji.

Walisema viongozi hao wameuza maeneo ya kijiji chao ikiwamo mapalio ya kupitishia mifugo na wakihoji kwa viongozi hao kwa nini wameuza maeneo yao wanatishiwa kwa maneno hivyo wanashindwa mahali pa kwenda kulalamika.

“Tumefikisha suala hilo kwa kulalamikia hadi kwenye ofisi ya CCM ya kata,kwani viongozi hawa wa kijiji wamechaguliwa kupitia chama kilichpo madarakani,lakini hakuna hatua zozote zilizochukuliwa dhidi yao,” walisema wakazi hao.

Walisema maeneo hayo yaliyouzwa yaliachwa tangu mwaka 1975 kwa ajili ya maeneo ya kupitishia na kulishia mifugo,lakini wameshangazwa na viongozi hao kuamua kuyauza kwa wafanyabiashara hao kutoka Arusha.

Hata hivyo,Mwenyekiti wa kijiji cha Shambarai,Edward Wazi na Ofisa Mtendaji wa kijiji hicho,Mosses Peter walikanusha vikali kuuza maeneo hayo ila walidai kuwa yameuzwa na wamiliki husika wa maeneo hayo hivyo wao hawahusiki.

Wazi alisema maeneo hayo siyo ya Serikali ila wamiliki wenyewe wameyauza mashamba hayo ambayo ni mali yao na wao hawana mamlaka ya kuingilia au kutoa uamuzi juu ya mashamba hayo.

Peter alisema wamiliki hao wameyauza kihalali mashamba hayo baada ya kupata shida, hivyo wao hawana uamuzi wa kumzuia mtu kuuza eneo lake kwani wenyewe hawamiliki chochote na wala hawahusiki na
ashamba hayo
-->

KANISA LACHOMWA MOTO JANA HUKU PADRI MUSHI KUZIKWA LEO

SIKU tatu baada ya kuuawa kwa kupigwa risasi Padri Evarist Mushi Mjini Zanzibar, Kanisa la The Pool of Siloam lililoko katika Shehia ya Kianga, Wilaya ya Kati, Mkoa wa Kusini Unguja, limechomwa moto na watu wasiojulikana na kuharibu madhabahu yake.

Kuchomwa moto kwa sehemu ya kanisa hilo, kumetonesha kidonda cha kifo cha Padri Mushi ambaye aliuawa kwa kupigwa risasi kichwani, Jumapili asubuhi mjini Zanzibar. Padri huyo anazikwa leo.

Akizungumza katika kanisa hilo, Naibu Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai upande wa Zanzibar ambaye pia ni Naibu Kamishna wa Polisi, Yusuf Ilembo alisema tukio hilo limetokea kati ya saa tisa usiku na saa 10 alfajiri ya kuamkia jana.


“Mlinzi aliona watu watatu wakiwa ndani ya eneo la kanisa na alipowakaribia wakaendelea kupanda ngazi kwenda juu. Baadaye walirudi na kuanza kumrushia mawe akakimbilia nje kupitia dirishani. Ghafla akaona moto unawaka, kumbe walikuwa wamechoma viti vya plastiki vilivyokuwa ndani,” alisema Naibu Kamishna Ilembo.


Mlinzi huyo, Mussa Jackson alisema: “Niliona watu watatu wakipita na baadaye wakawa wanarusha mawe, mwisho nikakimbia na kumwambia jirani na kumpigia simu mchungaji msaidizi. Wakati nakwenda kwa jirani nikaona moto mkali unawaka kanisani, sikujua wameuwashaje.”


Mchungaji Msaidizi wa Kanisa hilo, Penuel Elisha alisema tukio hilo ni la pili kwa kanisa hilo kwani mwaka 2011 zaidi ya watu 80 wakiwa na mapanga, nyundo na magongo walilivamia na kulivunja kabisa.


Alilishukuru Jeshi la Polisi kwa kuwahi kuwasaidia katika tukio la jana.
Licha ya kutotaka kuonyesha uhasama na msikiti uliopo eneo hilo, Penuel alisema siku moja kabla ya tukio hilo viongozi wa msikiti huo walihoji uhalali wa kujengwa kwa kanisa hilo.


“Siku moja kabla ya tukio la mwaka 2011, viongozi wa msikiti walihoji uhalali wa sisi kujenga kanisa hapa. Sisi tukawaonyesha vibali vyote. Lakini kesho yake kanisa likabomolewa. Hatuna mgogoro na msikiti, kwanza hayo matukio ni ya kawaida tu hapa Zanzibar,” alisema Penuel.


Alipoulizwa kuhusu kuwapo kwa uhasama kati ya msikiti na kanisa hilo, Imamu wa msikiti huo, Hassan Migirimu alikanusha akisema kuwa mzozo huo ulikuwa kati ya kanisa na Sheha Assed Mvita ambaye amefariki dunia.


“Sisi hatuna mgogoro na hilo kanisa aliyekuwa akihoji uhalali wake ni marehemu Assed Mvita. Hatujawahi kugombana na kanisa hilo hata siku moja,” alisema Imamu Migirimu.


Padri Mushi kuzikwa leo
Padri Mushi anatarajiwa kuzikwa leo eneo la Kitope na ibada ya mazishi itaanza saa nne asubuhi katika Parokia ya Mtakatifu Joseph Minara Miwili.


“Baada ya kikao cha Baraza la Walei tulikubaliana kuwa ibada ya mazishi itafanyika hapa Parokia ya St. Joseph Minara Miwili na mwili wake utazikwa Kitope wanakozi kwa viongozi wa kanisa,” Askofu wa Kanisa Katoliki Zanzibar, Augustino Shao alisema jana.
Akizungumzia sababu ya Padri Mushi kuzikwa Zanzibar badala ya kusafirishwa kwenda kwao Moshi mkoani Kilimanjaro, Askofu Shao: “Padri Mushi ameishi Zanzibar tangu akiwa na miaka 18 hivyo ni mkazi wa Zanzibar... Hakuna sababu ya kusafirishwa. Mimi ndiye niliyekuwa mlezi wake hivyo hakuna sababu ya kumpeleka kuzika kwa askofu mwingine.”

Chadema yalaani mauaji ya kidini, kuzindua sera ya majimbo

Viongozi wa Chadema wakiwa wamekaa meza kuu katika mkutano wa Uzinduzi wa Chadema Kanda ya Kaskazini uliofanyika jana katika viwanja vya Ngarenaro Arusha.

Mwenyekiti wa Chadema Mh Freeman Mbowe akiongea katika mkutano wa ufunguzi wa Kanda ya Kaskazini.




Mwenyekiti wa taifa wa Chadema, Freeman Mbowe, amekibebesha Chama Cha Mapinduzi (CCM) vurugu na mauaji ya kidini huku akiwaonya viongozi wa Chadema watakaoshiriki na kuhamasisha chuki dhidi ya dini nyingine kuwa watafukuzwa kwenye chama hicho asubuhi na mapema.
“Udini ni sera ya CCM, wamelikoroga, sasa tunataka walinywe,” alisema jana wakati akifungua mkutano wa viongozi wa majimbo 33 na mikoa ya Kanda ya Kaskazini inayojumuisha mikoa ya Manyara, Arusha, Kilimanjaro na Tanga, ikiwa ni sera yao ya majimbo.
Pamoja na kuwaonya viongozi, Mbowe pia aliwataka wanachama wa Chadema popote pale walipo wasishiriki kuwabagua wenzao kwa imani ya dini bali waheshimu imani za watu wengine.
Aidha Mbowe alisema; “Chadema inalaani vikali mauaji ya viongizi wa dini yanayotokea maeneo mbalimbali nchini…tunaitaka CCM na serikali yake kuwajibika dhidi ya mauaji hayo.”
“Kuona kiongozi wa dini akimwagiwa tindikali, akipigwa na hata kuuawa kwa sababu za kidini sio mambo ya kujivunia hata kidogo…CCM ndiyo iliyokuwa ikilea udini na hapo ndipo ilipotufikisha…tunataka CCM na serikali yake iwajibike kwa hilo.”
Alisema Mkristu hana haki ya kumhukumu Mwislamu na wala Mwislamu hana haki ya kumhukumu Mkristu, hivyo Chadema kimeamua kuchukua hatua kali dhidi ya mwanachama ye yote bila kujali wadhifa wake atakayehamasisha chuki za kidini.
Alisema sera ya udini iliaasisiwa na CCM kama mbinu yao ya kuwafanya waendelee kubakia madarakani lakini hali inavyoonekana sasa inatisha amani na umoja wa taifa.
 

Serikali Zanzibar yaahidi kuwasaka hadi kuwatia mbaroni waliohusika na mauaji ya Padri Evaristus Mushi.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein.
---
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, amepokea kwa mshtuko mauaji ya Padri Evaristus Mushi na kutoa pole kwa  waumini, ndugu jamaa, marafiki na wananchi wote wa Zanzibar kufuatia kifo hicho.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Mhe. Mohamed Aboud ameeleza hayo jana, Jumatatu, Februari 18, 2013 na kusisitiza kwamba   Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi itawasaka hadi kuwatia mikononi na hatimaye kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria wale wote waliohusika na mauaji hayo.

Waziri Aboud ameyaeleza hayo wakati alipozungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Vuga, kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein kufuatia mauaji ya  Padri Evaristus Mushi wa Kanisa Katoliki  Zanzibar Parokia ya Mtakatifu ST.Joseph, Shangani.

Hapo jana Dkt. Shein alikutana na Askofu Augustino Shao wa Kanisa Katoliki, Jimbo la Zanzibar, huko katika Ikulu Ndogo Migombani, Zanzibar  na kueleza masikitiko yake kutokana na mauaji hayo ya Padri Mushi wa Kanisa Katoliki la Zanzibar, na kuelezea haja ya kuwepo kwa uvumilivu katika kipindi hichi cha msiba.

Katika mazungumzo na waandishi wa habari,  Waziri Aboud alisema kuwa Serikali imejipanga vizuri  kupitia vyombo vyake vya ulinzi na usalama ili kuhakikisha kuwa watu wote waliohusika na mauaji hayo wanakamatwa mara moja .

“Kutokana na jiografia ya Zanzibar,Tunaelewa kwamba zipo sehemu katika kisiwa cha Zanzibar ambazo wahalifu wanaweza kuzitumia, hivyo Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na vyombo husika vitaziba mianya yote ili kupambana na uhalifu “, alisema Aboud.

Alisema matendo ya uhalifu yanafanywa katika mazingira ya usiri mkubwa kwa hivyo ili wahalifu hao wakamatwe wananchi hawana budi kutoa mashirikiano  kwa Jeshi la Polisi pale wanapohitajika.

Akijibu suali la Mwandishi, Mhe.Aboud alikanusha taarifa zilizozagaa mitaani za kuwepo silaha nyingi mikononi mwa watu wasiohusika na kuwataka wananchi kuondoa hofu. 

Sambamba na hayo, Mhe. Aboud amewataka viongozi wa dini mbali mbali  pamoja na waumini wa dini zote  hapa Zanzibar kuwa wastamilivu katika kipindi hiki kigumu cha maombolezi.
Aidha, Waziri Aboud alisisitiza haja ya kuwepo uvumilivu kwa waumini wa dini zote ili kuirejesha Zanzibar katika historia yake ya kutokuwa na migongano ya kidini.

Askofu Shao: Matukio ya uhalifu, ubaguzi na chuki dhidi ya ukristo Zanzibar yanaendelea kushamiri kwani watu waliopewa dhamana ya kulinda na kusimamia amani na usalama wa wananchi wanaishia kukemea kwa maneno tu badala ya vitendo.


Askofu wa Kanisa Katoliki Parokia ya Minara miwili Augustino Shao akizungumza na Waandishi wa habari kuhusiana na kuwawa kwa Padri Mushi huko Ofisini kwake Kanisa la Minara miwili.
--
ASKOFU wa kanisa katoliki jimbo la Zanzibar,Augostino Shao Alisema matukio ya uhalifu yanayoendelea kujitokeza nchini hasa kwa waumini na viongozi wa kanisa hilo hayahusiani na itikadi za kidini bali yanafanywa na watu wachache wasioitakia mema Zanzibar.
Hayo yamesemwa na Askofu wa kanisa hilo Augustino Shao wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Kanisa la Minara Miwili Shangani, mjini Zanzibar.
Alisema, kuongezeka kwa matukio ya uhalifu nchini, kunatokana na kutowajibika kwa watendaji wa vyombo hivyo, jambo alilosema linatoa nafasi kwa watu wenye dhamira ya kuchafua amani na utulivu uliopo nchini kutenda uhalifu.
“Matukio ya uhalifu, ubaguzi na chuki dhidi ya ukristo Zanzibar yanaendelea kushamiri kwani watu waliopewa dhamana ya kulinda na kusimamia amani na usalama wa wananchi wanaishia kukemea kwa maneno tu badala ya vitendo.pindi kunapotokea matendo hayo”, alisema Askofu Shao.

“Siwezi kuhusisha matukio haya na tofauti za dini ya kikiristo na kiislam bali ni ukosefu wa umakini kwa watendaji wa vyombo vyenye dhamnana ya kusimamia maisha ya watu.”Aliendelea kusisitiza Askofu.
Hata hivyo, alisema waumini pamoja na viongozi wa kanisa hilo hapa Zanzibar wanaendelea kuishi kwa hofu na hivyo kushindwa kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.
Aliongeza kuwa, uongozi wa kanisa hilo ulifanya juhudi za kuzungumza na watendaji wakuu wa serikali ya Zanzibar tangu lilipoanza vuguvugu la uchomaji makanisa na kufikia makubaliano ya kushirikiana katika kudhibiti hali hiyo.
Aliwataka waumini wa dini ya Kikristo na wananchi kwa ujumla kuwa wavumilivu kwa kipindi hiki cha msiba wa Padri Evaristus Mushi.
Naye Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Aziz Mohamed, alisema jeshi hilo linaendelea na upelelezi ili kuhakikisha wahusika wa tukio hilo wanakamatwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria.
Aliwataka wananchi kushirikiana na polisi jamii kutoa taarifa zitakazosaidia jeshi hilo kukamilisha zoezi hilo kwa haraka zaidi.
“Tangu kuuwawa kwa Padri Evaristus Mushi juzi Jumapili, tuliitisha kikao cha dharura kwa maafisa mbalimbali wa Polisi, tukapeana majukumu ili kuhakikisha wahusika wanatiwa mbaroni”, alieleza kamanda huyo.
Akizungumzia suala la umiliki wa silaha nchini, alisema kwa mujibu wa sheria za Tanzania hakuna mtu yeyote anayeruhusiwa kumiliki silaha ya aina yoyote isipokuwa kwa kibali maalum au taratibu zinazotambulika kisheria

PENGO: Wakristo Msilipe Kisasi Mauaji ya Padri Mushi

Kiongozi wa kanisa katoliki Tanzania, Muadhama Kadinali Polycarp Pengo
 
KIONGOZI wa kanisa katoliki Tanzania, Muadhama Kadinali Polycarp Pengo amewataka wakristo kutolipa kisasi kufuatia kuuawa kwa Padri Evarist Mushi huko Zanzibar.

Amesema wakristo kulipa kisasi hakutawasaidia kwani ni kinyume cha mafundisho ya dini ya kikristo na sheria za nchi. Kadinali Pengo ameitaka Serikali  kuwa makini na watu ambao wanataka kuivuruga amani ya nchi kwa kisingizio chochote kile.

Kiongozi huyo amevitupia lawama vyombo vya usalama wa nchi kwa kutochukua hatua za tahadhari kwani kulikuwa na ishara ya uhalifu kupitia vipeperushi vilivyosambazwa huko Zanzibar.

TAMKO LA WAKRISTO KUHUSU MAUAJI YA ASKOFU

TANZANIA CHRISTIAN FORUM (TCF) MKOA WA MBEYA
TAMKO RASMI KUTOKA KTK JUKWAA LA WAKRISTO MKOA WA MBEYA
MHESHIMIWA NDG. ABAS KANDORO,
KAMA MKUU WA MKOA NA MWAKILISHI WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHESHIMIWA JAKAYA MRISHO KIKWETE MKOA WA MBEYA, TUNAPENDA KUSOMA MBELE YAKO TAMKO RASMI LA JUKWAA LA WAKRISTO MKOA WA MBEYA (TCF).
NDUGU MKUU WA MKOA,
            “HAKI HUINUA TAIFA BALI DHAMBI NI AIBU YA WATU WOWOTE” (Mit. 14:34).
Katika mkutano wa jukwaa la Wakristo Tanzania mkoa wa mbeya ulionyika tarehe 12/02/2013 Jijini Mbeya, wajumbe tulitafakari kwa undani juu ya hali inayoendelea kujitokeza katika nchi yetu na hasa katika mahusiano baina ya dini mbili kuu UKRISTO NA UISLAMU.
Jukwaa hilo lilijumuisha taasisi zake kuu (yaani mabaraza ya Madhehebu ya Kikristo)
Tanzania Episcopal Council (TEC), Christian Council of Tanzania (CCT) na Pentecostal Council of Tanzania (PCT).Mbali na mambo yake ya kawaida jukwaa hilo lilitafakari utekelezaji wa Serikali juu ya tamko Rasmi la jukwaa la Wakristo kitaifa lililotolewa tarehe 06/12/2012 na kusomwa katika makanisa yote ya Kikristo nchini kwenye sikukuu ya Krismas tarehe 25/12/2012. Katika tafakari letu jukwaa la Wakristo wa Mkoa wa Mbeya tumeona kuwa kunabaadhi ya mienendo inayojitokeza katika nchi yetu ambayo kama isipodhibitiwa na kukomeshwa na Serikali italeta athali kubwa na hata kuondoa amani na uthabiti (Stability) wan chi.
Katika kutafakari kwa jukwaa juu ya athari zinazoweza kujitokeza, kumekuwepo na mambo yanayotendeka waziwazi yenye athari kubwa kwa amani na usitawi wa nchi na wananchi wake kwa ujumla. Kwa mfano, uchochezi, kashfa, matusi na uchokozi wa wazi unaofanywa na baadhi ya waumini wa dini ya Kiislamu kupitia vyombo vya habari vya kidini (rediona magazeti), mihadhara, kanda za video, CD na DVD pamoja na kauli zinazotolewa na viongozi wa dini hiyo kwenye baadhi ya nyumba zao za ibada(ushahidi upo kama vile uhamasishaji wa Sheikh Ilunga) pasipo serikali kuchukua hatua stahiki na badala yake kubaki kimya au kupambana na wanaofichua harakati hatarishi kwa utulivuwa nchi.
Miongoni mwa harakati hatarishi zinazosambazwa kwa njia ya CD na DVD za Sheikh Ilunga, kuhusu kuua Wachungaji, Mapadri na Maaskofu zimeanza kuwa matokeo mabaya; kwani Padri kule Zanzibar alipigwa risasi na watu walioitwa na serikali wahuni na sasa kifo
Kimetokea na mchungaji Mathayo Kachila kule Buselesele Mkoani Geita na kikundi kinacho dhaminiwa ni wanaharakati hao wa kiislamu wenye jazba na gadhabu kali inayotokana na mvutano uliopo kati ya wakristo na waislamu kuhusu nani mwenye haki kisheria KUCHINJA WANYAMA. Hatua zinazochukuliwa na Serikali hazilizishi wala kukidhi matakwa ya wananchi wapenda amani. Tuna mifano kadhaa ya matukio kama haya yaliyojitokeza kwa wanchi wenzetu moja ni ile ya mwenzetu aliyepigwa risasi kule Rungwe Ndg. John Mwankenja (Mwenyekiti wa CCM Rungwe) aliyepigwa risasi kwa mambo yanayodhaniwa kuwa ni ya kisiasa) Serikali ichukuwe hatua madhubuti kwa kutuma wachunguzi kutoka Dar es salaam kwa swala hilo na wote tuliridhika kwa hatua hizo madhubuti. Hatua kama hizo mbona hazichukuliwi katika masuala haya ya kidini na badala yake Serikali inakaa kimya au inachukua hatua ambazo kimsingi hazitatui tatizo ili wananchi waridhike na Serikali yao? Je tuseme Serikali inaangalia haiba (Personality) za watu au aina ya vikundi? Swala la uchinjaji lilipo jitokeza kule Mwanza waziri wa nchi ndg. Steven Wasira alienda na kutoa majibu mepesi katika swala zito je, tuseme aliyoyatamka huko yalikuwa ni KAULI YA SERIKALI au kauli yake mwenyewe? Na kama yake mwenyewe mbona Serikali haijakanusha waziwazi? Na kama ni kauli ya serikali hiyo haki ya kuchinja kwa waislamu inatokana na sheria zipi za nchi? Je huo ndio utawala wa sheria tuliyoahidiwa na serikali ya awamu ya nne kuwa itatenda kazi kwa kuzingatia utawala wa sheria.
Kupigwa risasi kwa Padri na kuuwawa kwa mchungaji kunathibitisha azma halamu na batili ya “Ua, chinja” mapadri, wachungaji na maaskofu iwe kwa siri au kwa wazi iliyoasisiwa na Sheikh Ilunga ambayo sio tu inahatarisha amani ya nchi lakini pia inavunja haki za kuishi za binadamu zilizoainishwa katika katiba ya serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. Aidha harakati hizi zina muelekeo wa kudhoofisha ukristo Tanzania kama sio kuumaliza kabisa. Pamoja na mambo mengine kinachosikitisha ni namna ambavyo serikali inavyoyashughulikia mambo mazito yanayotikisa amani na utulivu wa nchi. Utasikia mala ikisema “Mtu haruhusiwi kujichukulia sheria mkononi” na ndipo kikundi fulani kitaibuka na kuvunja mabucha na kuchoma nyama iliyomo humo hapo tena utasikia serikali hiyohiyo ikitoa kauli kwamba “Mvumiliane” je tunakwenda wapi?
Kwa misingi hiyo kwa nini tusite kusema kwamba serikali ya chama cha mapinduzi (CCM) inaibeba dini ya kiislamu? Kwa kuwa jukumu la serikali ya chama cha mapinduzi ni kuhakikisha kuwa wananchi wote wa Tanzania bila kujali dini zao, makabila yao na hata rangi zao wanaishi katika misingi ya uhuru, haki, udugu na amani kama raisin a watendaji wake walivyotoa kiapo mara baada ya kupewa dhamana ya kuiongoza nchi na wananchi wake kwa ujumla pasipo na ubaguzi wowote.
HITIMISHO: Ili wakristo wote nchini warudishe imani yao kwa serikali ya chama cha mapinduzi mambo yafuatayo ni lazima yachukuliwe hatua za haraka iwezekanavyo:    
  1. Tunataka Serikali izingatie utawala washeria kulingana na ahadi yake katika kushughulikia maswala ya kijamii na sio vinginevyo. Kwa kuzingatia sheria maswala ya imani na dini yapo wazi kabisa kama zilivyoanishwa kwenye katiba ibara ya 19 (1), (2) (3) (4)  na kufanya vinginevyo ni uvunjifu wa sheria.
  1. Swala la kuua lisichukuliwe kama mazoea ya kawaida na inapotokea popote ni lazima Serikali ichukuwe hatua inayostahiki kwa kuzingatia utawala wa sheria kwa kuwa wote wako sawa mbele ya sheria ibara ya 12, 13 (1) –(5).Usawa huo ni lazima uonekane katika swala la mauaji ya Mchungaji Mathayo Kachila na kama hatua zilivyochukuliwa katika mauaji ya aliyekuwa mwenyekiti wa halmashauri na mwenyekiti ya CCM Wilaya ya Rungwe Ndg. John A. Mwankenja. Hiyo ni haki ya msingi kkwa kila mtantania bila kuangali haiba (Personality) yake kama katiba ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania inavyoainisha haki xza kuishi, kulindwa na kushughuklikiwa kisheria katika ibara ya 14 na 15 pamoja na vifungu vyake viwili vidogo.
  2. Tunataka Serikali itueleze ni ushahidi gani zaidi inaoutaka kuliko ule unaopatikana kwenye CD na DVD zilizotolewa na Sheikh Ilunga kama inazingatia utawala wa sheria.
  3. Tunataka Serikali iwajibike kutolea ufafanuzi kauli ya waziri wa nchi Ndg. Steven Wasira inayohusu haki ya kuchicha kwa waislamu kama inatokana na sheria gani ya nchi?
  4. Kama Serikali inatekeleza utawala wa sheria, tunataka wakristo tuwe na machinjio na bucha zetu kulingana na imani yetu.
  5. Kama Serikali haitachukuwa hatua za makusudi katika kutekeleza madai yetu sisi kama viongozi wa dini ya kikristo tutachukua hatua ya kuwaambia waumini wetu kwamba Serikali ya chama cha mapinduzi inaibeba dini ya kiislamu na wao watajua la kufanya.
Pamoja na kutaka utekelezaji wa haraka kutoka kwa Serikali bado tunawaomba wakristo tuwe katika hali ya maombi na utulivu kwa wakati huu ambapo tumo katika vita vya kiroho ili Mungu akatuimarishie amani ambayo ni nguzo kuu ya Taifa letu. Tamko hili rasmi la jukwaa la wakristo Mbeya lisomwe katika makanisa yetu yote siku ya juma pili tarehe 24/02/2013.
Tunakuambatanishia na nakala ya Tamko Rasmi la TCF Taifa la tarehe 6/12/2012.
NDUGU MKUU WA MKOA NAWASILISHA.
Nakala kwa:
  1. Mwenyekiti wa CCM Mkoa.
  2. Tanzania Christian Furum Taifa
  3. Mwenyekiti wa the Tanganyika Law Society.
  4. Vyombo vya habari TV, Redio na magazeti