Pages

Pages

Wednesday, April 30, 2014

TLP kutimua viongozi wake watatu wa wilaya

Na Bertha Mollel- Arusha

Chama cha Tanzania Labour Party (TLP) Mkoani Arusha, kimewatimua viongozi wake watatu wa ngazi ya wilaya kwa madai ya kuvunja katiba ya chama pia  kushindwa kutekeleza majukumu yao badala yake wamekuwa wakiharibu hali ya hewa kila kukicha sambamba na kuwagonganisha viongozi wa mkoa wa chama hicho.

Timua timua hiyo imefanyika mapema jana kwenye mkutano mkuu wa kamati ya utendaji wa mkoa, ambapo waliwajadili viongozi hao wa wilaya akiwemo mwenyekiti wa TLP wilaya ya Arusha mjini na kuonekena kutokustahili kuendelea kuwa viongozi wa chama hicho badala yake warudi kama wananchama wa kawaida.
Viongozi hao walioenguliwa uongozi wa TLP wilaya ya Arusha mjini pamoja na aliyekuwa mwenyekiti wa TLP Michael Kivuyo ambae pia ni diwani wa kata ya Sokon One,  Salma Jumanne aliyekuwa katibu sambamba na Festo Kimaro aliyekuwa katibu mwenezi wa TLP wilaya.
Hata hivyo mkutano huo ulitumia fursa hiyo kuwachagua viongozi wa mda watakaokaimu nafasi hizo ambapo kwa upande wa nafasi ya mwenyekiti, itashikiliwa na Deo Mwakishi, na nafasi ya katibu itashikiliwa na Kinanzaro Mwanga huku nafasi ya Katibu mwenezi ikiwakilishwa na Deogratius Peter Silayo.

Wajumbe hao walisema kuwa wameamua kuchukua uamuzi huo kutokana na viongozi hao kuwa sehemu ya kusababisha migogoro katika chama hicho sambamba na kudidimiza chama kwa kushindwa kutekeleza majukumu yao ikiwemo hata kusimamisha wagombea kwenye nafasi mbalimbali za serikali zinapotangazwa hali ambayo inadhoofisha chama hicho.
Mmoja wa wajumbe wa kikao hicho Deo Mwakishi alisema kuwa miongoni mwa matatizo yanayosababishwa na viongozi hao ni pamoja na kugonganisha viongozi wa juu wa chama hicho na viongozi wa mkoa ikiwemo ubadhirifu wa fedha za kodi ya pango la ofisi iliyopitia kwa aliyekuwa mwenyekiti wa wilaya Michael Kivuyo na kumpatia katibu wake Salma.
Alisema kuwa fedha za kulipia kodi ya pango walijichanga zaidi ya shilingi laki sita na kuongezewa na mwenyekiti wa chama hicho taifa mh,  Eliatonga Mrema lakini fedha hizo zilipowadia zilipotea katika mazingira ya kutatanisha mikononi mwa viongozi hao wa wilaya hali iliyopelekea kufungiwa ofisi na sasa hawana ofisi ya mkoa wala ya wilaya kutokana na kudaiwa kodi.
“mbali na hayo katiba ya chama imekuwa ikivunjwa hasa baada ya kumsingizia mwenyekiti wa mkoa Leonard Makanzo kuwa ameiba fedha za chama zaidi ya shilingi milioni 5 lakini wakashindwa kuthibitisha fedha hizo chanzo chake badala yake wanawashawishi wajumbe wa halmashauri kuu ya mkoa kumkataa mwenyekiti walipoaibika zaidi ni juhudi zao zilipogonga mwamba wakaamua kumwita mwenyekiti na kumtangazia kuwa wamemfukuza uongozi na wamemteua Deo Humay kama mwenyekiti wa mda hiyo sheria imetoka wapi”
Akizungumzia mkutano huo kwa waandishi wa habari mwenyekiti wa TLP mkoa wa Arusha Leonard Makanzo alisema kuwa mkutano huo pamoja na kujadili maswala na chama lakini pia kimewajadil viongozi wake wa wilaya na wajumbe kubaini chanzo cha migogoro ni wao hivyo wakawaondoa na kuwachagua wengine wa mda.
“Itakumbukwa kuwa hata hao tuliowaondoa akiwemo mwenyekiti wa wilaya Kivuyo hakuwahi kuchaguliwa bali walipewa nafasi hizo kwa mda kutokana na viongozi waliokuwepo kuhama chama aukukiuka katiba hivyo hata hao tuliowaweka kwa mda wameshindwa kuwakilisha nafasi zao kwa kutekeleza majukumu yao badala yake wamekuwa wakituharibia tu hali ya hewa lakini leo imefikia mwisho”
“Lakini mimi niseme tu kwamba hawa viongozi tuliowaondoa leo watabaki kama wanachama wa kawaida na wanaruhusiwa kugombea nafasi zozote za uongozi wa serikali na chama pindi nafasi zikitangazwa” alisema Makanzo.
Kuhusu swala la kutimuliwa ofisi kutokana na kudaiwa kodi na sasa wako wanarandaranda mtaani kwa kukosa mahala pa kuhudumia wanachama wao, mwenyekiti huyo alisema kuwa “ kwa sasa tunatafuta ofisi nyingine tutakayoweza kumudu gharama za kulipia hivyo baada ya tu ya mda mfupi tutakuwa na ofisi mpya tena nzuri zaidi”
Alitumia nafasi hiyo kuwataka wanachama wa TLP kuwa na imani na chama hicho kwani kinafanya mabadiliko hayo kuboresha chama hasa kwa kuwapata viongozi wazalendo watakaokisaidia chama kufika mbali ikiwemo kushika nafasi mbalimbali za uongozi kuwahudumia.
Kwa upande wake aliyekuwa mwenyekiti wa Chama hicho wilaya alipoongea na waandishi wa habari alisema kuwa yeye hana ugomvi na mtu kugombania cheo,
“Mimi sina taarifa halisi ya sababu ya wao kuniondoa oungozi lakini kama wameona ni sawa sina ugomvi nao bali nataka tu kujua sababu kiundani basi.

Merry Baasa miss kataru 2014

 Mrembo Eveline katika picha ya pamoja  na wenzake waliotwaa tatu bora, ambapo kwa upande wa kushoto ni Happy Tarmo na kulia ni Merry Joel
 
Mrembo Evaline Baasa (19) amefanikiwa kutwaa taji ya Ulimbwende wa wilaya ya Kataru kwa mwaka 2014 na kuwabwaga wenzake wanane katika kinyanganyiro kilichofanyika katika ukumbi wa Ngorongoro Camp uliopo mjini hapa.

Evaline amekua mrembo wa kwanza kwa wilaya hiyo tangu kuanzishwa kwa wilaya ya karatu ambapo alibahatika kujinyakulia kitita cha shilingi laki tano na pia kuingia katika shindano la miss Arusha linalotarajiwa kufanyika mwezi june sambamba na hilo amepata udhamini wa maandalizi yote kwa ajili ya kushiriki shindano lililoko mbele yake.

Mshindi wa pili alikuwa Happy Tarmo (19) ambaye alijinyakulia fedha taslim shilingi laki tatu na kufuatiwa na Merry Joel (21) aliyezawadiwa shilingi laki mbili na mshindi wa nne ikienda kwa  Veronica John (21) na washiriki wenzake watano ambapo alipata kifuta jasho cha shilingi elfu themanini  kila mmoja.
 
warembo, wakionyesha vazi la usiku kwa pamoja ambapo wa kwanza kulia ni Eveline Baasa, anaefuata ni merry joel, Asha Bonivenrute,  Upendo Mtweve, Veronika Joel, Scolastika Fransis, Janeth Jackson, Glorry Aloyce, Happy Tarmo.
Hili lilikuwa shindano la kwanza kwa wilaya ya Karatu ambalo lilikuwa kivutio kikubwa kwa wakazi wa wilaya hiyo kufuatia ushindani mkubwa uliojitokeza kwa washiriki wote kuwa na sifa zote hali iliyowapa kazi ya ziada majaji waliokuwa wakiongozwa na mratibu wa miss kanda ya kaskazini Faustine Mwandago.

Mashabiki wa tasnia ya urembo mjini Karatu waliokuwa wakiongozwa na diwani wa Karatu mjini Jubilate Mnyenye walilipuka kwa shangwe baada ya jaji mkuu Mwandago kumtangaza mlimbwende Evaline kuwa ndiye  mshindi wa miss Karatu 2014 matokeo yaliyoungwa mkono na wadau wote wa tasnia ya urembo waliohudhuria onyesho hilo.
, Mlimbwende Eveline Baasa akiwa katika picha ya pamoja na majaji wa shindano hilo wakiongozwa na jaji mkuu Faustine Mwandago ( watatu kutoka kulia aliyvalia shati la mistari)

Hili linakuwa shindano la kwanza kwa ngazi ya kitongoji cha wilaya ya Karatu kwa mkoa wa Arusha wenye vitongoji vitatu ambavyo ni Karatu, Monduli na kituo cha Arusha mjini ( Arusha city center).

Aidha baada ya kitongoji cha Karatu kumpata mrembo wake, wiki ijayo kinyang’anyiro cha pili  kitafanyika kitongoji cha monduli na kitongoji cha mwisho kitakua cha arusha city  kitakachofanya baadae mwaka huu ikiwa ni mchakato wa kumpata miss Arusha.


Aidha kila kitongoji kitatoa warembo wane kila kitongoji ambapo kutakuwa na jumla ya warembo 12 ambapo watashiriki katika kinyanganyiro cha kumsaka mrembo wa mkoa wa Arusha


Mgeni rasmi katika shindano hilo la miss Karatu alikua ni mhifadhi mkuu wa mamlaka ya Ngorongoro Fredy Manongi ambaye aliwakilishwa na afisa uhusiano wa mamlaka ya hifadhi ya ngorongo Adam Akyoo ambaye aliwataka warembo kutumia fursa walionayo kupambana na ujangili kwa kutoa taarifa za watu wanajishughulisha na ujangili.

Akyoo alisema kuwa kupambana na ujangili siyo lazima kushika mitutu ya bunduki kumzuia mwindaji bali utoaji wa elimu pia unaweza kusaidia kupunguza kama si kumaliza kabisa tatizo la ujangili nchini.

Mrembo Evelini Baasa ( aliyekaa) akiwa na washiriki wenzake Hapy Tarmo kushoto na Merr Joel Kulia, Na wa kwanza kushoto ni aliyekuwa mwakilishi wa  mgeni rasmi Adam Akyoo, na wa mwisho kulia ni diwani wa Karatu mjini Jublet Mnyenye

Kwa upande wake diwani wa karatu mjini, Jublet Mnyenye alisema kuwa amefurahishwa na waandaji wa kinyang’anyiro hicho cha kumsaka mlimbwende wa Karatu pia karatu mjini kuwa wenyeji wa mashindano hayo kwa mara ya kwanza wilayani humo ambapo ameahidi kusapoti mashindano hayo mara nyingine yatakapofanyika kwa kujitolea ukumbi, zawadi za washindi pamoja na maandalizi yote kwa ujumla.

Kinyanganyiro hicho cha aina yake kilichoburudishwa na msanii Snura “mama wa majanga” kilidhaminiwa na Makampuni mbalimbali na wadau wa urembo wilayani humo wakiwemo  kinywaji cha Redd’s, ZARA tour, hifadhi ya mamlaka ya Ngorongoro, Beauty point Cosmetics pamoja na mdau wa ulimbwende Mh, Steven Siay.

Snura "mama wa majanga" alitoa burudani ya aina yake katia shindano hilo

Tae Kwond kupata wakufunzi kutoka Japan



na Bertha mollel -Arusha
 
Kamati ya Olympic Tanzania (TOC) imeahidi kuwapa Shirikisho la mchezo wa tae kwon do Tanzania TTF wataalmu na wakufunzi  wa mchezo huo toka korea na japani ukiwa ni mkakati wa kukuza na kuendeleza mchezo huo wa kupigana karate ya kutukia mikono na mateke.

Rais wa TTF Ally Ramudh akizungumza na Tanzania Daima  mkoani hapa alisema kuwa kamati hiyo ya TOC imeona jinsi Tanzania tulivyo na juhudi za mchezo huo ingawa hatujui utaalam wake sana hali iliyowavutia na  kuahidi kuleta wataalam watakaotuwezesha kujua zaidi.

Alisema mpango huo unaodhaminiwa na kamati ya Olypic ya kimataifa (IOC) umetokana na mafanikio ya kukubalika kwa mchezo huo ambao kwa mara ya kwanza utatoa wawakilishi wa Tanzania katika mashindano yajayo ya Olympic.

Kwa mujibu wa Ramudh wataalam hao wanatarajiwa kutua nchini mwanzoni mwa mwezi wa sita, watazunguka Tanzania nzima kufundisha na kuhamasisha mchezo wa tae kwon do ambapo asili yake ni nchini korea na hong kong.

Akizungumzia juu ya mchezo huo Rais huyo wa TTF alisema kwa sasa mchezo huo umekubalika na kukua kwa kasi kwani sasa unafundishwa katika taasisi mbalimbali za kiusalama kama makampuni ya ulizi na hata katika majehi ya ulinzi na usalama ikiwemo katika majeshi yetu ya polisi.

Tae kwo ndo ni mcheza wa kujilinda kwa kushambulia kwa kutumia mikono na miguu na umejijengea umaarufu mkubwa kwa kuwawezesha mchezaji wa mchezo huu kujilinda hata akishambuliwa na kundi la watu wenye silaha.

Mchezo huo wa Tae kwo ndo ni jamii ya michezo ya  karate ,kong fu na kick boxing wenye asili ya china,korea na japan ambapo humwezesha mtu pia kuwa m’bunifu katika kujihami ambao pia huleta burudani katika kuucheza na kuungalia watu wakiucheza.

Tuesday, April 22, 2014

Bunge kuendeshwa fastafasta


SHARE THIS STORY
0
Share


Ni bahati mbaya kwamba Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linalotarajiwa kuanza kikao chake Mei 6, mwaka huu mjini Dodoma litalazimika kuendeshwa ‘fastafasta’ kutokana na kutengewa siku chache kukamilisha shughuli zake. Kama inavyofahamika kwa wengi, utaratibu wa sasa unalitaka Bunge hilo kuwa limejadili na kupitisha Bajeti ya Serikali pamoja na Sheria za Fedha ifikapo mwishoni mwa Juni kila mwaka, ili kuruhusu bajeti husika kuanza kutumika Julai Mosi, ambayo ndiyo siku ya kwanza ya mwaka mpya wa fedha.
Tunazo sababu mbili za msingi tunaposema ni bahati mbaya Bunge la Bajeti kulazimika kuendeshwa ‘fastafasta’. Kwanza ni ukweli kwamba mijadala kuhusu Bajeti Kuu ya Serikali na bajeti za wizara mbalimbali haitakuwa ya kina kutokana na ufinyu wa muda. Pili, kutokana na ufinyu huo wa muda, kuna uwezekano mkubwa Bajeti Kuu ya Serikali na za wizara nyingi kubwa na nyeti kama Ofisi ya Waziri Mkuu ambayo inatumia zaidi ya theluthi moja ya bajeti nzima ya Serikali, zikapitishwa zikiwa na takwimu za kupikwa na za kufikirika zilizobuniwa na watumishi wasio waaminifu wanaoendesha mitandao ya wizi wa fedha za Serikali.
Hatari itakayotokana na hali hiyo ni kupatikana kwa bajeti zisizokuwa na uhalisia, kwani hata Kamati za Bunge zimepewa wiki moja tu kujadili bajeti husika, badala ya wiki tatu. Matokeo ya kazi za kurashiarashia namna hiyo ni kulifanya Bunge kuwa mhuri wa kupitisha madudu na kuhalalisha vitendo vya wizi, ufisadi na ubadhirifu wa fedha za Serikali. Ratiba ya Bunge hilo inaonyesha kuwa, Bunge la Bajeti litakutana kwa siku 52, zikiwa pungufu kwa siku 28, ikilinganishwa na mkutano kama huo mwaka jana.
Swali la kujiuliza hapa ni hili: Kwanini Bunge limefikia hali hiyo? Pamoja na Uongozi wa Bunge kusema siku nyingi zimetumika kwenye shughuli za Bunge Maalumu la Katiba, halisemi kwanini mamlaka husika haikushauriwa kuahirisha Bunge hilo la Katiba ambalo limetumia siku 67 katika malumbano na mijadala isiyokuwa na tija kwa taifa. Bunge la Bajeti lingepewa kipaumbele kwa sababu ndilo uti wa mgongo wa shughuli za Serikali na taasisi zake.
Sisi tunadhani kwamba yalikuwa makosa makubwa kuwaacha mawaziri na wabunge wa Bunge la Muungano wakijikita katika siasa na itikadi za vyama ndani ya Bunge Maalumu la Katiba, huku wakijua fika kwamba Bunge la Bajeti lazima liwe limepitisha Bajeti na kumaliza mkutano wake ifikapo mwishoni mwa Juni. Pamoja na kutambua kwamba kutofanya hivyo kunaweza kusababisha majanga kwa taifa, bado waliona kipaumbele ni siasa na malumbano yasiyoisha kuhusu ‘kura iwe ya siri au ya wazi’ na ‘muundo wa serikali mbili au tatu’. Hayo ndiyo matokeo ya kuweka siasa mbele na kudidimiza uchumi.
Sasa nini kifanyike? Spika anaweza kujaribu kuokoa jahazi kwa kutoruhusu porojo bungeni. Mawaziri wawasilishe bajeti fupi lakini zilizosheheni takwimu sahihi na tafakuri jadidi. Michango ya wabunge ilenge kwenye hoja na wasipewe muda wa kupongezana na kuwatambulisha marafiki, mashemeji na kadhalika. Iwapo kanuni na ratiba vitapanguliwa ili vikao vifanyike mchana na usiku, siku za kazi na za mapumziko, itawezekana kupatikana kwa bajeti zilizochambuliwa barabara, zenye mwelekeo na endelevu.
mwananchi

Chadema wamshukuru Rais Kikwete




Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wilayani Karatu kimeeleza kufurahishwa kwake na mchango unaotolewa na Rais Jakaya Kikwete katika kuchochea maendeleo bila upendeleo.
Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, ilisema kuwa pongezi hizo zilitolewa jana mchana na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu, Lazaro Titus Massey wakati wa sherehe za uzinduzi wa jengo la Halmashauri hiyo mjini Karatu. Halmashauri ya Wilaya ya Karatu inaongozwa na Chadema.
“Ni lazima tutoe shukurani kwako kwa sababu bila wewe kuwa Rais wa Tanzania, sisi Karatu tusingepata jengo hili. Pamoja na kwamba Halmashauri yetu ni Chadema bado umeamua kuchangia maendeleo ya wilaya yetu kwa kuchangia kiasi kikubwa ujenzi wa jengo hili. Sisi hata robo ya fedha za ujenzi huu hatukuweza kuzitoa,” alisema Massey huku akishangiliwa na wananchi.
Jengo la Halmashauri ya Wilaya ya Karatu limegharimu Sh1.412 bilioni na kati ya hizo, Serikali imetoa Sh1.394 bilioni na halmashauri imechangia Sh18 milioni.
Rais Kikwete alisema sera ya Serikali yake ni kusambaza maendeleo kwa Watanzania wote bila kujali misimamo yao ya kisiasa wala kuongozwa na hisia nyingine mbali na ukweli kuwa kila mtu anataka maendeleo.

Sunday, April 20, 2014

polisi wakana askari kufukuzwa


TIMUATIMUA ya askari wa Jeshi la Polisi iliyotangazwa wiki iliyopita na  Kamanda wa  Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani  nchini, Mohamed Mpinga, imemuibua Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Ulrich Matei, na kusema hatambui kama kuna askari wake wamefukuzwa kazi.
Kauli ya Kamanda Matei imekuja huku kukiwa na malalamiko kutoka kwa askari waliofukuzwa kuwa baadhi ya viongozi wao wa mikoa wamefikia uamuzi huo kinyume cha sheria na mapendekezo ya waendesha mashitaka wa Jeshi la Polisi waliosikiliza mashitaka yao.
Matei alisema anachojua kwa askari wa mkoa wake kuna kesi inaendelea na bado haijamalizika.
“Kwangu hakuna aliyefukuzwa, waliopo kesi zao bado zinaendelea. Lakini mbona mnaandika sana mambo ya jeshi letu? Tunahangaika usiku na mchana kwa ajili ya ulinzi na taarifa kama hizi zinawakatisha wengine tamaa, kwani hata majeshi mengine yanafukuza, lakini hawaandikwi kama sisi,” alisema Matei.
Askari hao walioomba wasitajwe majina walisema uamuzi wa kuwaondoa kazini umefanywa kwa lengo la makamanda kujikosha kwa mkuu wa jeshi hilo nchini, IGP Ernest Mangu, hivyo kumuomba atumie busara kuhakikisha haki inatendeka dhidi yao.
Hivi karibuni Kamanda Mpinga akizungumza na waandishi wa habari, alisema kikosi chake kimewafukuza kazi askari 10 kwa tuhuma za kwenda kinyume na maadili ya jeshi hilo ikiwa ni pamoja na kubainika kufanya vitendo vinavyoashiria rushwa.
Ingawa katika mkutano huo Kamanda Mpinga hakutaja majina ya  askari hao, Tanzania Daima imedokezwa kuwa waliokuwa katika mkumbo huo ni 15 na si 10, kwamba hali ya kupunguza idadi na kuacha kutaja majina ilikuwa na lengo la kuwaokoa baadhi ya askari wenye undugu na baadhi ya viongozi wa juu wa jeshi hilo.
Majina ya askari waliotimuliwa ni Koplo Japhari, Koplo, Swaumu, Koplo Zua Koplo Johari, Pc Prisca, Pc Charles  na Pc Christina ambao wanaotoka Mkoa wa Kipolisi Temeke na wengine ni Pc Hawa, Pc Evarist Pc Athumani,  Pc Johanes Cp Frank,  Sg Robison  na Cp  Salehe wanaotoka Mkoa wa Pwani.
Polisi waliofukuzwa kutoka Mkoa wa Temeke walisema msingi wa tuhuma zao zilianza Machi mwaka huu katika kikao cha makamanda wa polisi Tanzania kilichofanyika mkoani Kilimanjaro na kuhudhuriwa na IGP Mangu.
Chanzo cha habari kilieleza katika mkutano huo, mikanda mbalimbali ya video ilitolewa kwa ajili ya kujiridhisha juu ya mienendo ya askari wanapofanya kazi huku mikoa ya Temeke, Pwani na Morogoro makamanda wake wakitakiwa kuzipitia kwa umakini taarifa zilizoonyeshwa na kufanya uamuzi wa haki kwa watakaobainika kufanya makosa.
“Temeke kulikuwa na mikanda miwili, mmoja ulikuwa  haueleweki na kwa kweli ulikuwa mbaya na  mwingine ulikuwa unaonyesha askari wakiwa wanaongea na dereva wa daladala na kisha kuanza kuandika kwenye kitabu cha malipo, na haya ndiyo yaliyozingatiwa na mwendesha mashitaka katika kesi ya kipolisi mpaka akapendekeza adhabu ya wengine kushushwa vyeo na wengine kukatwa mishahara ya siku saba,” kilisema chanzo chetu ndani ya jeshi hilo.
Hata hivyo, inadaiwa mapendekezo yaliyotolewa na mwendesha mashitaka wa mahakama ya kipolisi Mkoa wa Temeke yalipuuzwa na Kamanda wa Polisi wa mkoa huo, Englibert Kiondo, na kuamua kuwafukuza kazi askari nane.
Alipoulizwa Kamanda Kiondo sababu ya kupuuza mapendekezo ya hukumu ya wanasheria walioendesha kesi katika mahakama ya kijeshi, alisema mahakama hiyo inaendeshwa kwa siri na kwamba anayetoa uamuzi ni yeye.
“Unazungumziaje uamuzi wa mahakama ya kijeshi? Nani kakwambia habari hizo wakati kesi zinaendeshwa kwa siri? Mimi siwezi kuzungumzia mambo hayo, na kama kuna mtu anaona ameonewa akate rufaa milango ipo wazi kwa Afande IGP,” alisema Kamanda Kiondo.
tanzania daima

wananchi wapewe jukumu la kuamua kuhusu muungano

MVUTANO wa muundo wa serikali mbili au tatu uliogubika Bunge Maalumu, umelifanya Baraza la Mahusiano ya Dini mbalimbali kwa Amani Tanzania (IRCPT), kutaka kura ya maoni ifanyike ili wananchi waamue muundo wa muungano.
Baraza hilo limebainisha kuwa viongozi wa dini watakubali kupiga kura ya maoni kuhusu mapendekezo ya Katiba ambayo yamezingatia maoni yaliyotolewa na wananchi.
Msimamo wa baraza hilo umo ndani ya kitabu cha mapendekezo kwa wajumbe wa Bunge Maalumu kuhusu rasimu ya Katiba, walichokisambaza juzi kwa wajumbe wa Bunge Maalumu.
Mratibu wa baraza hilo, Thomas Goda, alisema miongoni mwa taasisi zinazounda baraza hilo ni Baraza la Waislamu Tanzania (Bakwata), Baraza la Kikistro Tanzania (CCT), Baraza la Makanisa ya Kipentekosti Tanzania (BMKT), Tanzania Asian Development Association (TADA) na Tanzania Episcopal Conference (TEC).
Goda, alisema kuwa wajumbe wa baraza lao walikutana Machi 26, mwaka huu jijini Dar es Salaam ambapo  waliijadili na kuichambua rasimu ya Katiba inayojadaliwa hivi sasa na wajumbe wa Bunge Maalumu.
Alisema baada ya kujadili na kuchambua rasimu hiyo wamebaini giliba za kisiasa, malumbano, jazba, tofauti za kiitikadi na kutozingatia kanuni ndizo zimetawala majadiliano ya Bunge Maalumu hivyo kutia doa safari ya kupatikana Katiba yenye kujumuisha makundi mengi.
Alibainisha kuwa wameandika kitabu chenye kurasa 12 kwa lugha ya Kiswahili na Kiingereza zilizo na mapendekezo 14.
Tanzania Daima Jumapili, imepata nakala ya kitabu hicho ambacho katika ukurasa wa sita pendekezo namba moja linawataka wajumbe waheshimu rasimu ya Katiba iliyobeba maoni ya wananchi na kuifanyia kazi kwa lengo la kuiboresha.
Pendekezo jingine ni kuwataka wajumbe wajadiliane kwa upendo, kuheshimiana na kuthaminiana bila kuathiriwa na mawazo pandikizi, masilahi binafsi, vyama, kabila au eneo la mjumbe.
Katika ukurasa wa nane wa kitabu hicho, 3.1, baraza hilo linataka wananchi waachiwe waamue  kwa kupitia kura ya maoni juu ya muundo wa serikali.
Mapendekezo hayo pia yanataka Katiba itatambue uwepo wa mamlaka ya Mungu, sifa za rais awe mwana ndoa, ndoa ni kati ya mume na mke, itoe mwongozo wa matumizi ya rasilimali za taifa na ukusanyaji kodi, rais anayemaliza muda wake aondolewe kinga kama sehemu ya kujenga uadilifu na uwajibikaji.
Katika ukurasa wa 11 kitabu hicho kinataka kiongozi aliyefukuzwa au kujiuzulu kwa kukiuka miiko na maadili ya uongozi asigombee na asiteuliwe tena katika nafasi yoyote ya uongozi.
Mengine ni katiba itenganishe kuingiliana kwa mihimili mikuu mitatu ya dola; Serikali, Bunge na Mahakama (uteuzi wa wabunge watano usifanywe na rais, mawaziri wasiwe wabunge).
Katiba itambue kwa makusudi kuwepo uwakilishi  wa baraza la viongozi wa dini na wazee wenye busara kuishauri serikali mambo ya kisheria na mambo yote nyeti ya kitaifa.
Viongozi wote wanaoteuliwa au kuchaguliwa nafasi ya uongozi, uadilifu wao lazima uthibitishwe na Tume ya Maadili kabla ya kuteuliwa au kuchaguliwa.
Naye mjumbe wa baraza hilo, Ali Mose, alisema wameingiwa na wasiwasi mkubwa kama Katiba iliyotarajiwa itapatikana, kwakuwa watu wameweka mizizi ya kiitikadi ambayo inakwamisha wajumbe kusikiliza hoja za upande mwingine.
Alisema kuna hatari ya kupatikana kwa Katiba isiyoyaunganisha makundi yote, jambo ambalo ni hatari na doa, kwa kuwa Katiba inajengwa katika misingi ya maridhiano.
‘Viongozi wa dini tuna jukumu la kuwaunganisha wajumbe ili maridhiano yafikiwe na taifa lipate Katiba nzuri itakayowafurahisha  Watanzania wote,” alisema.

Thursday, April 17, 2014

UTATA KESI YA MSHITAKIWA WA WIZI WA TWIGA



MATUMAINI ya kumpata mshitakiwa namba moja katika kesi ya kusafirisha wanyama hai wakiwamo twiga wanne kwenda nchini Qatar, Kamran Ahmed, yameyeyuka baada ya jana mshitakiwa huyo kutofika tena mahakamani.
Mshitakiwa huyo amekuwa hafiki  mahakamani  kwa mara ya nne sasa huku kukiwa hakuna taarifa rasmi za kutofika kwake kutoka kwa wadhamini wake wala wakili wake, Edmund Ngemela.
Kesi hiyo ilikuja kwa kutajwa jana mbele ya Hakimu Mkazi, Simon Kobelo, anayesikiliza shauri hilo na baada ya mshitakiwa huyo kushindwa kufika mahakamani.
Mahakama imepanga kuanza kusikiliza kesi hiyo mfululizo Mei 6 na 7 mwaka huu.
Wakili wa Serikali, Patrick Mwita, aliiambia mahakama jana kuwa mshitakiwa huyo hakufika mahakamani na kusisitiza hati ya kukamatwa iendelee kuwa pale pale kama ilivyoamuliwa na mahakama.
Tayari upande wa mashitaka umeanza kufuatilia anwani za wadhamini wa mshitakiwa huyo, ili wakamatwe kutokana na kutofika mahakamani kutoa taarifa juu ya mshitakiwa huyo kama masharti ya dhamana yanavyoagiza.
Washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni Hawa Mang’unyuka, Martin Kimath na Michael Mrutu ambao wote wako nje kwa dhamana.
Washitakiwa hao kwa pamoja wanadaiwa kusafirisha wanyama hao hai Novemba 26, mwaka 2010 kwenda Qatar kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), wanyama wanaodaiwa kukamatwa maeneo ya Mto wa Mbu, Elboret na Engaruka wilayani Monduli, mkoani Arusha.
Wanyama hao wenye thamani ya sh milioni 170.5 wanadaiwa kusafrishwa kwenye maboksi marefu ndani ya ndege kubwa ya jeshi la Qatar.