JOSE KAMILION KUNOGESHA SHINDANO LA KUMSAKA REDD'S MISS ARUSHA KESHO KATIKA VIWANJA VYA TRIPLE A
MMOJA wauguzi wa hospitali ya maria stopes Hamza Mzira akiwa anagawa vipeperushi kwa warembo
Dr,Sober Mzighani akiwa anawapa elimu warembo wanaogombania
ulibwende wa jiji la Arusha waliotembelea hospitali ya maria stopes
Picha ikionyesha warembo wakiwa
wanatembelea baadhi ya ofisi za hospitali hiyo
warembo
wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wauguzi wa hospitali hiyo wakati
walipomaliza kupewa elimu
warembo
wanaogombania taji la redd’s miss arusha wakiwa na mrembo ambae anasubiri
kuachia ngazi ya urembo wa jiji la arusha Glory Stephen nje ya
hospitali ya maria stopes
Picha ikionyesha warembo wakiwa wanatembelea baadhi ya ofisi za hospitali
hiyo
WAREMBO 13 wa Redd’s Miss Arusha 2014 jana wametembelea kituo cha uduma za afya cha Maria stopes kwa ajili ya kujifunza Afya ya uzazi wa mpango na maradhi mbalimbali ya saratani ya kizazi
Akiongea na warembo hao Msimamizi wa hospitali hiyo ya mariastopes ya jijini
hapa Dr,Sober Mzighani alisema kuwa
hospitali yao imeamua kutoa elimu hiyo kwa warembo hawa ambao ni vijana ili
waweze kusambaza ujumbe kuhusu uzazi wa mpango na afya ya uzazi.
Alisema kuwa elimu hii watatoa kwa
vijana wote ili wasambaze kwa wananchi nchi wote uku akisema kuwa
,vijana wengi ndio wananguvu na uwezo wa
kusambaza taarifa hizi kwa jamii .
Kwa upande wa mrembo ambaye anashikilia taji la Redd’s missArusha Glory Stephen
alisema kuwa anawashukuru sana wauguzi
wa maria stopes kwa jinsi walivyowapa elimu kwani wengi wao walikuwa awajui
elimu ya uzazi .
Alisema kuwa vijana wengi wamekuwa wafanya ngono uzembe wengine wamekuwa
wanapata mimba pasipo mpangilio lakini kwa kutumia elimu hii na kwa kutumia
nafasi zao ambazo wanazo watajitaidi kuelimisha wengine kuhusiana na uzazi wa
mpango
Kwa upande wa muaandaji wa Redd’s
Miss Arusha, Faustine Mwandago, alisema kuwa warembo hao ni washindi
waliotokana na mashindano ya ngazi ya vitongoji yaliyomalizika hivi karibuni.
Mwandago, aliwataja warembo hao kuwa ni Janeth Alex (20), Neema Urio (19),
Lilian Deus (18), Leila Thomas (19), Husna Hamis (20), Happyness Tarimo (19), Eveline
Baasa (19), na Marry Joel (21).
Wengine ni Neema Charles (19), Dyness Peter (21), Rahisa Mboye (21), Joselyn
Mirashi (21), na Amber Gladys (20).
Mwandago alisema kuwa shindano hilo litasindikizwa na burudani ya aina yake
kutoka kwa msanii anaewika katika nchi za afrika mashariki Jose kamilione pamoja na wasanii mbalimbali
wa Mkoa wa Arusha.
Shindano hili la kusaka mlimbwende wa mkoa wa Arusha (Redd’s miss Arusha)
linatarajiwa kufanyika Juni 7 katika viwanja vya ukumbi wa Triple A na kiingili
katika shindano hili vip watalipa kiasi cha shilingi 60000 huku viti vya
kawaida wakilipa 30000.
0 comments:
Post a Comment