Pages

Pages

Friday, May 29, 2015

Singh atwaa ubingwa wa "Northern province golf competition” 2015/2016

Mwanamichezo wa gofu za ridhaa (amacha) Prabvir Singh ameibuka kidedea katika michuano ya wazi ya siku mbili yajulikanayo kama “Northern province golf competition” na kufanikiwa kuwa bingwa wa mashindano hayo kwa mwaka 2015/2016.

Mashindano hayo ya wazi yaliyoandaliwa na chama cha gofu Tanzania, TGU (Tanzania gofu Union) kwa kushirikiana na Arusha gymkhana club (AGC) yalifanyika kwa siku mbili mwishoni mwa wiki ambapo Singh aliibuka mshindi wa jumla kwa kupiga mikwaju 141 na kufanikiwa kuwa bingwa na kuzawadiwa kombe kubwa.

Michuano hiyo iliyodhaminiwa na Benson Security System  pamoja na Sameer Parts ltd yaliweza kuwapa makombe pia mshindi wa daraja la kwanza Simon Travers aliyepiga mikwaju 149 akifuatiwa na Izak Wanyeche waliyepiga mikwaju 150.

Kwa daraja la pili Jugdish Ahluwalia “Chuchu” aliibuka mshindi kwa kupiga mikwaju 146 akifuatiwa na Kush Lodhia  149 huku daraja la tatu Rujvil Sohal akishinda kwa mikwaju 150 akifuatiwa na Alliabbas Somji aliyepiga mikwaju 151 wote wa Arusha.

Northern province golf competition yalishirikisha pia wanawake na Lina Francis wa Arusha kuibuka mshindi kwa kupiga mikwaju 148 na kwa watoto Jafari Omary wa TPC moshi kwa mikwaju 146 huku Habbib Yusufali (Arusha) akiibuka mshindi kwa upande wa wazee kwa kupiga mikwaju 168 na wote kupatiwa makombe madogo.

Zawadi za makombe pia zilitolewa kwa washindi waliovuka viwango (Cross winner) ambapo Abbas Adam wa Moshi aliibuka kwa kupiga mikwaju 154 akifuatiwa na Danniel Corpella kwa kupiga mikwaju 154 pia washindi wa siku ya kwanza Muzafar Yusufali aliibuka mshindi kwa mikwaju 72 na Minir Sheriff wa moshi alimfuatia kwa mikwaju 73.

Washiriki wa mashindano hayo 61 kutoka vilabu vya TPC na moshi club, Lugalo sambamba na Arusha walitakiwa na mgeni rasmi ambae ni mhazini wa gofu taifa Gelase Rutachibirwa kuwa wajitahidi kutafuta chipukizi wa mchezo huo watakaokuwa na viwango vizuri kuunda timu ya taifa ili kufanikiwa kushiriki katika mashindao mbali mbali ya kimataifa na kuiwakilisha nchi yetu.

Kwa upande wa mmoja wa wadhamini wa mashindano hayo kutoka Benson Security System, Nadeem Hussein alisema kuwa mashindano ya mara kwa mara kama hayo yanaweza kuwafanya wachezaji kupanda viwango na kuwa wataalam wa mchezo huo (Proffessional) na kupata ajira.

Mwisho………….

Bimo Media yaiunga mkono CCM kuandaa tamasha la amani

na Mwandishi wetu - Arusha
Uongozi wa taasisi ya BIMO Media ya Mkoani Arusha. Umeelezea kuunga mkono hatua ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupendekeza kuwepo siku maalumu ya kuadhimisha umoja na amani kitaifa.
BIMO pia imeelezea kufurahishwa na hatua ya CCM kutaka kuanzisha matamasha maalumu ya umoja na Amani yanayolenga kudumisha mshikamano nchini bila kujali itikadi za wananchi.
Mkurugenzi wa taasisi hiyo, Bertha Ismail Mollel amesema kuwa BIMO Media ilikuwa ya kwanza kuandaa matamasha haya ya Amani na kwamba tukio la kwanza lilifanyika jijini Arusha mnamo mwezi Desemba mwaka jana na kwamba kwa mwaka huu wako tayari kabisa kuungana na Chama Tawala katika kuhakikisha kuwa matamasha ya Amani yanafanikiwa kwa kiwango kikubwa hapo mwezi julai.

"Swala la amani ni jukumu la kila mtu hivyo sisi tulianza tukiwa na lengo kubwa la kuwakutanisha vijana pamoja na kuwaeleza umuhimu wa amani na wasikubali kugawanywa kwa misingi ya dini, ukabila wala siasa pia wasikubali kutumika kama magaidi katika nchi yao bali  wajenge uzalendo wa hali ya juu" alisema Bertha.

Wakati huhuo huo Msajili wa vyama vya siasa nchini, Jaji Francis Mutungi ameelezea kufurahishwa na matamasha ya Amani na hasa pale yanapowalenga vijana ambao ndio nguvu kuu ya taifa na ndio hasa wenye jukumu la kulinda Amani na kudumisha umoja nchini.
Hata hivyo Jaji Mutungi amebainisha kuwa, ni vizuri pia wanafunzi wa vyuo na shule zote nchini washirikishwe kikamilifu bila kusahasu viongozi wa dini na taasisi zake kwani huko ndiko wananchi huwakilishwa kwa wingi.
Hivi karibuni uongozi wa juu wa CCM ulipendekeza kuwepo na siku maalum kitaifa kwa ajili ya kuadhimisha umoja na Amani ambapo matuniko kadhaa yakiwemo ya michezo, matamasha ya muziki, sala maalum na mengineyo yangekuwa yanafanyika na kuwaleta pamoja wananchi katika maeneo yote nchini kujumuika bila kujali tofauti zao za kiitikadi na kisiasa.
Matamasha hayo yameelezewa kuwa ni hatua muhimu ya kuwaunganisha tena watanzania hususan katika kipindi hiki cha uchaguzi ambapo watu wengi hujikuta wamegawanyika kutokana na kampeni za wanasiasa wanaowania nafasi na nyadhifa kadhaa nchini huku wakitumia vijana kutishia uvunjifu wa amani.

mwisho........

Ukata waikwamisha Arusha kushindana michuano ya majiji Afrika na kati

Timu ya Arusha mpira wa kikapu (wa kwanza kushoto ndie katibu wa mchezo huo Mkoa)

Bertha Ismail - Arusha
Timu ya mpira wa kikapu ya Jiji la Arusha ni miongoni mwa timu za majiji za Nchi za Afrika yanayoshiriki mashindano ya mpira wa kikapu kila mwaka, lakini kwa mwaka huu Ukata unaoindama timu hiyo imeshindwa kabisa kuwakilisha katika mashindano hayo ya mwaka huu yaliyoanza kutimua vumbi katika uwanja wa ndani wa Taifa jijini Dar es salaam jana.
Akizungumza kwa uchungu mkubwa, katibu wa Mpira wa kikapu mkoa wa Arusha Bariki Kilimba aliliambia gazeti hili kuwa wameshindwa kwenda kushiriki michuano hiyo kuwakilisha jiji la Arusha kutokana na kukosa kiasi kidogo cha pesa kilichopelea huku wadau wakishindwa kuwasaidia.
“Kiukweli imeniuma sana kushindwa kushiriki mashindano haya makubwa Afrika kwa sababu tu ya kukosa kiasi kidogo cha pesa kwani bajeti yetu ilikuwa ni milioni 1.6 hivyo tulitembea kwa wadau ikiwemo jiji la Arusha na kwa mkuu wa mkoa lakini tuliambulia patupu, ila kwa sababu tuna moyo tuliamua kuchangishana kwa wale wenye uwezo ambapo tulipata laki 8 na wachezaji wengine ni wanafunzi hivyo walishindwa kuchanga na fedha ikapelea”
“kUfuatia hali hiyo tulianza kutafuta marafiki wa karibu yetu lakini wengi hawakuwa na uwezo wa kutusaidia hivyo tukaamua tu kutulia na nafasi yetu bado ipo hewani hivyo tunaomba kwa watu wenye uwezo jamani watusaidie bado tuna nafasi ya kuwakilisha jiji letu kwenye nchi  za Afrika au kampuni na taasisi zitusaidie nasi tutawatangaza kwenye nchi hizi shiriki” alisema Kilimba.
Timu hiyo ya wanaume yenye jumla ya wachezaji 10 ilianza mazoezi makubwa tangu mwezi uliopita  huku wakifanya mashindano ya mara kwa mara za kirafiki kujifua kwa ajili ya mashindano hayo ya majiji wakiwa na matumaini makubwa ya kurudi na ushindi lakini ukata umekatisha ndoto zao.
Aidha michuano ya mpira wa kikapu kutoka majiji ya Afrika yameanza jiji Dar huku timu kutoka sehemu mbali mbali zikishiriki ikiwemo majiji ya Tanga, Mwanza, Kampala, Kigali Entebe, Nairobi Mombasa, Mogadishu, Hargeisa (Somalia), Bujumbura, Garowe, Diaspora, Bentieu, Malakal,Juba, Cairo n.k.
mwisho............

Monday, May 11, 2015

Mmoja afariki kwa kutumbukia bwawani- Arusha.

mwili wa Ibrahim baada ya kuopolewa kwenye bwawa hilo na wasamaria wema baada ya wataalam wavamiaji kukosekana

Arusha. Mtu mmoja,  Ibrahim Issa (25) amekufa maji baada ya kutumbukia kwenye bwawa lenye maji linalomilikiwa na kampuni ya Kili flora lililoko eneo la Mlangarini Wilayani Arumeru mkoani Arusha.
mwili ukipelekwa pembezoni mwa bwawa tiyari kutolewa kwenye maji
baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya maua ya kili flora wakiwa wanashuhudia mwili wa mwenzao baada ya kuopolewa kwenye bwawa.

jeshi la polisi pamoja na maafisa wa zima moto wakiondoa mwili eneo la tukio kuupeleka chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya mkoa mount meru tiyari kwa mazishi
Mwili huo uliodumu kwenye maji kwa muda wa masaa 26, uliokolewa na wasamaria wema waliojitolea kuutafuta mwili huo ili kuutoa kwenye bwawa alikotumbukia lenye kina cha maji mita 20 chini na mita 500 urefu.
Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo ya Kili flora walisema  kuwa marehemu alitoka mapumziko ya kunywa chai saa nne asubuhi may 8 mwaka huu na kubeba waya aliyotengenezea ndoano kwa ajili ya kwenda kujipatia samaki lakini kwa bahati mbaya aliteleza na kuangukia ndani ya maji.
“Kwa mbali tulisikia kama kuna kelele bwawani nyuma ya mashambani na tulipokwenda kutazama tulimuona Ibrahim (Mrehem) Akiomba msaada na tukafanya juhudi za kumrushia kamba kuvuta lakini haikuwezekana kwani alishachoka na ndipo alipozama”alisema Jane Macha
Macha alisema Tulitoa taarifa kwenye uongozi kumuokoa mapema lakini hata hivyo ilishindikana kwa kutolewa ruhusa ya haraka kutokana na makao makuu ya uongozi kuwa USA, eneo ambalo ni mbali na hapa hivyo baadae uongozi ulipofika ulikuwa unasua sua kufanya taratibu za kumuokoa mapema hivyo wananchi walijitosa kwenye maji na kuanza kumtafuta  kucha bila mafanikio.
Mwenyekiti wa mtaa wa Olomitu, kata ya Mlangarine, Absalom Kambaine  alisema kuwa ingawa alichelewa kupata taarifa lakini siku ya pili asubuhi ya May, 9 alikwenda  kuomba msaada wa kuupata mwili kwa wataalam wa maafa wakiwemo jeshi la polisi, jeshi wananchi kikosi 977kj, na kikosi cha zima moto lakini hakufanikiwa kwa kile kinachodaiwa ukosefu wa vifaa.
“Kiukweli nimepata taarifa asubuhi hii nikaamka na kukimbia kimbia kwa wataalam ambapo zimamoto walifika eneo la tukio lakini walisema hawawezi kuupata mwili huo kwani hawana vifaa vya uokoaji majini pia wataalam wa kuzama, nikaenda kambi ya jeshi hii hapa karibu moshono nao wakasema hakuna wataalam wa uzamiaji majini bali wapo wavuvi pekee na hawataweza kufanya kazi hiyo hadi kibali makao makuu pia polisi walifika hapa lakini wao wakasema wamekuja kuweka ulinzi na kusubiri mwili tu” alisema mwenyekiti Kambaine.
Kwa upande wa baba mzazi wa marehem Joseph Issa alisema  kuwa hali hiyo ya mwanae kuzama na kukaa ndani ya maji kwa zaidi ya masaa 26 ni uzembe wa vikosi husika na serikali kwa pamoja kukosa vifaa vya uokoaji ndio maana maafa yanatokea mara kwa mara huku hakuna anaejishughulisha na tahadhari hivyo wanamuachia Mungu swala hilo,
Mwisho……

Wednesday, May 6, 2015

magazeti ya leo Tanzania mei 6, 2015

DSC02211 

DSC02212 
DSC02213 
DSC02214 
DSC02215 
DSC02216 
DSC02217 
DSC02218 
DSC02219 
DSC02220 
DSC02221 
DSC02222 
DSC02223 
DSC02224 
DSC02226 
DSC02227 
DSC02228 
DSC02229 
DSC02230 
DSC02231 
DSC02232 

mashabiki wa simba wapiga yanga 6-3

Bertha Ismail - Arusha

Wakati matani ya hapa na pale yakiendelea baina ya mashabiki wa timu kongwe nchini Simba na Yanga, mashabiki hao  Arusha wameamua kufuta ubishi wa nani Mb’abe wa kandanda safi, ambapo Simba wamedhiirisha umwamba wao baada ya kuwabugiza Yanga mabao 6-3.

Mchezo huo wa kirafiki uliowakutanisha mashabiki wa simba na yanga Arusha, uliopigwa katika uwanja wa shule ya msingi Moshono kwa lengo la kutaka kujua nani m’babe wa soka, Simba ilidhiirisha umwamba wake baada ya kuwapiga mashabiki wa Yanga jumla ya mabao 6-3.

Mchezo huo ulioanza kwa kasi ya aina yake na kujaza mamia ya mashabiki, Timu ya Simba ndio ilianza kupata mabao mawili ya haraka haraka ambapo bao la kwanza liliingizwa dakika ya sita mwa mchezo kupitia kwa Wilfred Kadege na Robert Boniface akipiga bao la pili dakika ya nane na kupelekea mashabiki kujigawa kwa ushangiliaji.

Wachezaji wa Yanga walionekana kujawa makali zaidi na kuongeza kasi ya kupambana kuligusa lango la Simba ambapo dakika ya 25 Frank Shapi alifanikiwa kuipatia timu ya Yanga bao la kwanza ambapo hata hivyo kipigo kwao kiliendelezwa na Robert Boniphace aliyeiandikia timu yake ya Simba bao la Tatu dakika ya 34 hali iliyozidisha hasira za wana-Yanga hao ya kulisakama lango la Simba ambapo hata hivyo Frank Kamili alijifunga katika harakati za kuokoa na kuiandikia timu ya Yanga bao la pili dakika ya 39 hadi mapumziko.

Kipindi cha pili kilianza huku timu ya Simba ikionekana na mabadiliko ya hali ya juu na mashambulizi ya iana yake na dakika ya 68 Wilfred Kadege aliiandikia samba bao la nne na  Robert Boniphace kuandika bao la tano dakika ya 75 hali iliyonyamazisha kelele za mashabiki wa nje wa Yanga na shangwe za mashabiki wa samba zikitawala na kuzidi kuvuta umati wa watu kushuhudia mtanange huo.

Baada ya mabao hayo wachezaji wa Yanga walionekana dhahiri kujawa na ghadhabu na jazba za hapa na pale huku wengi wakikoswa koswa na kadi za mwamuzi Gasper Getto lakini dakika ya 78 Mrope Mrope alibahatisha bao la tatu kwa timu yake ya Yanga baada ya kupiga shuti lisilo na matumaini ya kupata bao na dakika ya 86 Frank Kamili alifunga wingu la mvua ya mabao kwa timu ya Simba, na kuleta matokeo ya 6-3 hadi hadi dakika 90 kutia nanga.

Wakizungumza na gazeti hili, Kaptein wa timu ya Mashabiki wa simba Arusha, Wilfred Kadege alisema kuwa wameamua kutumia week end hiyo kuwafunga mdomo mashabiki wa Yanga kwamba wao ndio wababe wa kandanda baada ya kuweka matambo mengi kwa mdomo hivyo wakaamua kuwaonesha kazi ya Simba uwanjani.

“Tumeamua kutumia jumapili hii kuwafunga mdomo hawa watani wetu maana wamekuwa wanatamba sana mdomoni hasa baada ya kufanikiwa kucheza Kamari ya ligi kuu na kuwa mabingwa lakini wajue kuwa hawatufikii kwa lolote kwani kama ni zawadi ya kucheza mpira tunawazidi baada ya kucheza mtani jembe na kombe la Zanzibar tumeingiza zaidi ya watakachopewa kwenye ligi kuu milioni 75 sisi tumeshinda mechi mbili tuna milioni 120.”alijitamba Kadege.

Kwa upande wa msemaji wa timu ya mashabiki wa Yanga, Joram George alisema kuwa ingawa mchezo huo wamepoteza lakini wanaamini Simba hawajawazidi kitu zaidi ya kubahatisha mchezo huo baada ya wachezaji wengi wa timu yake kuwa majeruhi ikiwemo mlinda mlango namba moja ambapo amesema ili kudhihirisha hilo wataomba mechi ya marudiano wadhihirishe ubabe wao wa ligi kuu.

“tumepoteza kwa bahati mbaya tu huu mchezo lakini sisi yanga ndio kila kitu na ndio maana wanatupigia saluti tukiingia uwanjani na huu mchezo wamebahatisha baada ya wachezaji wetu wengi kuwa majeruhi lakini tutaomba mchezo wa marudiano na ukweli utajitenga na uongo”

Kwa upande wake kocha wa timu ya mashabiki hao wa Yanga kwa ujumla waliounga umoja wao wa mwangaza maveterani, Patson Mambete alisema kuwa mchuano huo wa kirafiki ulilenga kutoa burudani ya aina yake lakini pia kumaliza ubishi wa kila siku wa ubabe wa watu wa Simba na Yanga hapa mkoani Arusha.

Mwisho……………………..

Arusha Ryno washindwa kuwatambia Mombasa SC nyumban


wachezaji wa Arusha ryno (Tanzania- kijani) wakiwania mpira uliorushwa pamoja na timu ya Mombasa sc


Timu ya Arusha Ryno ya Tanzania imeshindwa kutamba nyumbani mbele ya timu ya Mombasa SC ya Kenya, baada ya kulazwa kwa point 28-26 katika mchezo wa awali wa mfululizo wa mashindano ya Rugby yanayoshirikisha timu za nchi za Afrika mashariki.
Arusha Ryno ilishindwa kutamba katika uwanja wake wa nyumbani wa TGT ulioko kisongo jijini Arusha kwa mara ya kwanza mbele ya Mombasa katika michuano hiyo ya mchezo wa Rugby ya nchi za Afrika mashariki ijulikanayo kama “Hatch cup” iliyochezwa mapema mwishoni mwa wiki.
Timu ya Arusha ryno wakimiliki mpira
Akizungumza baada ya michuano hiyo, Kaptein wa timu ya Arusha Ryno, Justine Robert alisema kuwa tangu kuanza kwa mashindano hayo kwa zaidi ya miaka mitatu hawajawahi kufungwa na timu ya Mombasa lakini kwa leo hali hiyo imetokea hali inayowatia uchungu sana na kuahidi kufanya vizuri katika mechi ya marudiano.
“Kiukweli hatujawahi kufungwa na hawa jamaa lakini imetokea hivyo niahidi kwa sababu ni mechi ya awali na kuna marudiano tutafanya vema na tutaanza mazoezi makali kwa ajili ya kuwafunga mabingwa watetezi ambao ni “Dar-es-salaam Leopard” may 9 mwaka huu hivyo mashabiki wetu wasikate tama kwani kombe hili la “Hutch cup” linakuja Arusha”
Kwa upande wake kaptein wa timu ya Mombasa SC, Chris Atingo alisema kuwa wanayo furaha kwa mara ya kwanza kumfunga timu ya Arusha Ryno kwani kwa miaka kadhaa sasa wamekuwa vibonde mbele ya timu hiyo hali iliyowalazimu kufanya mazoezi ya usiku na mchana kuhakikisha wanakuwa mlima mkali.
“Leo tunayo furaha kumfunga Arusha kwani miaka kadhaa sasa wamekuwa wakitufunga hali ambayo imefikia sehem tukasema iwe mwisho na tukaamua kufanya mazoezi usiku na mchana na matunda ya mazoezi yetu tumeyaona na tutaendelea ili kumfunga pia dar- Leopard na Arusha tutakapomkaribisha nyumbani kwetu Mombasa hivyo karibuni na ninyi waandishi muone vibonde wamegeuka mlima” alisema Chris wakishangiliana na timu wenzake.
Aidha michuano hiyo ya mchezo wa Rugby inayohusisha nchi za Afrika mashariki kwa mwaka huu zimeshiriki timu tatu za Dar, Arusha na Mombasa yakiwa na malengo ya kuwafanya vijana chipukizi kuwaonesha mbinu za mchezo huo katika mashindano ili waweze kuiga na kuyatekeleza ili kushinda wanaposhiriki katika mashindano ya kimataifa ambapo timu za nchi hizi zimekubaliana kushirikiana kukuza mchezo huu.
timu ya vijana wadogo walioko chini ya mradi wa kukuza na kuendeleza mchezo wa Rugby Arusha wakichuana kabla ya mechi ya wakubwa ambapo hata hivyo vijana wa Pallot waliibuka bingwa chini ya young Ryno 24-10
Awali katika mchezo wa kuwakaribisha miamba hao wa Mombasa na Arusha, timu ya vijana wadogo chini ya umri wa miaka 15 walioko chini ya mradi wa kuendeleza mchezo wa Rugby Arusha (Arusha Rugby Development Programme- ARDP) waliminyana kati ya timu ya Pallot na “Young Ryno” ambapo hata hivyo pallot waliwabigiza wenzao kwa point 24-10.
Michuano hiyo ya Rugby Hutch cup imeanza imeanza mwanzoni mwa mwezi huu ambapo timu ya Mombasa SC waliwakaribisha mabingwa watetezi Dar- leopard ambapo miamba hiyo ilishindwa kutambiana na kutoka suluhu ya point 12- 12 ambapo wanatarajia kurudiana jijini Dar mwishoni mwa mwezi huu wa may.
Mwisho…………….

michael wapania kuvunja rekodi za riadha miaka 40 iliyopita

Bertha- Arusha

Wanariadha wa kimataifa Michael Gwandu na Michael Michael Danford wa Arusha wameanza mazoezi makali ya kuhakikisha wanavunja rekodi ya kitaifa za mbio fupi, ya kuruka chini na viunzi iliyodumu kwa zaidi ya miaka 40 sasa.

Wanariadha hao wanaojifua katika viwanja vya sheik amri abeid kwa kuruka viunzi na kuruka chini na mitupo wamesema kuwa wamekuwa mabingwa wa mchezo huo kwa miaka zaidi ya tano sasa hivyo kwa sasa mwaka huu wanajifua kwa ajili ya kuvunja rekodi ya taifa ya michezo hiyo.

“Sisi tunajinoa makali kwaajili ya kuvunja rekodi za kitaifa kwanza na baadae dunia katika mbio fupi, kuruka na mitupo ambapo mbali na kuwashinda wapinzani wetu wa mikoa mingine lakini pia ni kuvunja rekodi ya kitaifa zilizowahi kuwekwa ikiwemo ya kuruka chini iliyowekwa na Raphael Mlewa mwaka 1971”

Kwa upande wa kocha wa wanariadha hao Samweli Tupa alisema kuwa wanariadha hao wamekuwa wakichukua ubingwa wa mara kwa mara katika mashindano ya kitaifa na jumuiya ya madola lakini cha kushangaza wengi wameshindwa kuvunja rekodi zilizowekwa kipindi cha nyuma hali ambayo ameamua kuwanoa wachezaji wake wavunjerekodi hizo.

“Kuna rekodi zimewekwa miaka zaidi ya 40 sasa kama mirujko mitatu iliwekwa rekodi mwaka 1970 na John Kanondo na kuruka viunzi kwa mita 110 lakini cha kushangaza rekodi hizo hazijavunjwa licha ya kila siku kujisifia wachezaji wetu kufanya vizuri kwa kuwa wa kwanza wakati rekodi za miaka ya ukolono bado ipo”

alisema kuwa kwa sasa wanariadha hao mbali na kufanya mazoezi ya peke yao pia watashiriki katika mashindano mbali mbali ikiwemo ya may 25 ya kitaifa itakayochagua wachezaji watakaowakilisha nchi katika mashindano ya wazi ya Uganda mwezi june.

Hata hivyo kochaTupa aliiomba serikali kusaidia mchezo huo kama awali ili uweze kuendelea kurudi na medali nyingi na kuvunja rekodi za dunia kama awali na kusema kuwa Tanzania inashindwa kufanya vizuri kutokana na kukosekana kwa sapoti kutoka serikalini kama ilivyokwa nchi kama Kenya, Unganda, n.k.



mwisho…………….

GINIKI AZIDI KUNG'AA KITAIFA

Bertha Ismail  - Hanang’

Mwanariadha Emmanuel Giniki amezidi kung’ara katika mbio mbali mbali za hapa nchini, baada ya mwishoni mwa wiki hii kung’ara tena katika mbio za may day kwa kukata upepo wa km 21 kwa kutumia saa 1: 01:17 na kuwaacha wenzake zaidi ya 70.

Mbio hizo zilizofanyikia Katesh makao makuu ya wilayani hanang’ kwa ajili ya kuadhimisha sikukuu ya wafanyakazi, Giniki alifanikiwa kuwa wa kwanza kumaliza mbio hizo akifuatiwa na Msandiku Mohamed aliyemaliza kwa saa 1:03:18 na aliyeshika nafasi ya tatu ni Stephano Huche 1:03:21.

Kwa Upande wa wasichana Anjelina Tsere alifanikiwa kutwaa ushindi baada ya kumaliza mbio hizo za km 21 kwa kutumia saa 1 :16: 43 akifuatiwa kwa karibu na Rozalia Fabiano kwa kutumia saa 1:21;15 na Amina Mohamed akishika nafasi ya tatu kwa kutumia saa 1:21:43.

Mgeni rasmi katika mbio hizo ni aliyekuwa waziri mkuu zamani Fredrick Sumaye ambapo mbali na kupongeza uongozi wa riadha manyara na waandaji aliwataka kuendeleza mashindano ya mara kwa mar ili kuwaweka wanariadha katika hali ya kufanya mazoezi ya mara kwa mara na kufanikiwa kushinda mbio za kimataifa hatimaye kurudisha heshima ya mkoa huo katika historia riadha.

Kwa upande wa waandaji , Alfredo Shahanga alisema kuwa kwa sasa wameamua kuendesha mashindano ya mara kwa mara ya mchezo huo ili kuwaweka wachezaji sawa kupambana katika michuano ya kimataifa iliyoko mbele yao ikiwemo ya All afrika game hivyo waweze kujitathimini mapema.

Mwisho……………….

Mbulu wachekelea RCL




Bertha Ismail - Arusha

Chama cha soka wilaya ya Mbulu, Kimeipongeza shirikisho la Soka nchini kwa kutambua umuhimu wa wilaya hiyo kimichezo na kuwapa nafasi ya kuwa moja ya vituo vitatu vya michuano ya ligi ya mabingwa wa mikoa Tanzania inayotarajia kutimua vumbi may 2 mwaka huu.

Michuano hiyo ya RLC itashirikisha jumla ya timu 27 nchini katika vituo vitatu vya Mbulu (Manyara) , lindi na Sumbawanga ambapo kila kituo inatarajiwa kuwa na timu tisa ambapo kwa Mbulu kutakuwa na timu ya Madini (Arusha), alliance school (Mwanza), Bariadi united (Simiyu) zingine ni  Baruti (Mara), Lukirini fc (Geita), Mtwivila City (Iribga), RAS Kagera fc (Kagera) pamoja na Small Prison (Tanga) na Watumishi fc (Shinyanga).

Ugeni huo mkubwa umewapa motisha kubwa wakazi na viongozi wa soka wilaya ya Mbulu na kufurahia nafasi hiyo adimu huku wakitoa shukrani zao za dhati kwa shirikisho la soka Tanzania kwa kutambua mchango wao huku wakisema kutumia michuano hiyo kama mafunzo kwao.

“Kiukweli tumefurahi sana TFF kutuletea michuano hii kwani itakuwa kama fursa kwetu ya kujifunza nini wenzetu wanafanyaga na tujifunze kwa kuiga ili na sisi tusonge mbele kisoka kwani imekuwa ikituuma sana zaidi ya miaka 10 hatujaonja ligi kuu na miaka mitano hatujui ligi daraja la kwanza likoje” alisema katibu wa soka wilaya ya Mbulu Fortunatus Kalewa.

“Tunashukuru timu nyingi zimeshaweka oda ya sehemu za malazi na viwanja vya mazoezi ikiwemo timu ya madini fc ya Arusha hivyo naamini itakuwa fursa kwetu kuwaleta wachezaji wa timu mbali mbali za mkoani hapa kuja kuiba mbinu wanazotumia wenzetu katika mashindano hadi wanasonga mbele na kuwakilisha mikoa yao katika ligi za ngazi za juu”

Kituo hicho cha Mbulu mashindano ya ligi ya mabingwa wa mikoa inatarajiwa kuanza kutimua vumbi may 9 katika viwanja vya Nyerere wilayani mbulu mkoani Manyara ambao uko katika hali nzuri kimandhari na uzio ingawa majukwaa bado ni changamoto.

Mwisho………………….