.

.
Wednesday, September 9, 2015

1:13 AM
Arusha . Timu ya maafande wa Jkt Oljoro inayoshiriki ligi daraja la kwanza Tanzania bara inatarajia kuchuana vikali na ndugu zao timu ya Arusha FC katika ufunguzi wa ligi maalum ya Nyerere cup inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi septemba 10 jiji Arusha.

Tiyari timu ya Arusha fc na Jkt Oljoro zimethibitisha kushiriki michuano hiyo huku kila mmoja akijitamba kuonyesha ubabe dhidi ya mwenzake na pia wakitumia mechi hiyo kutambulisha wachezaji wao kwa wapenzi wa Soka wa jiji Arusha.

Mechi hiyo ya ufunguzi kati ya Oljoro na AFC itakayochezwa jioni  katika uwanja wa Sheik Amri Abeid, ni kwa ajili ya kufungua michuano ya Nyerere cup  itakayoshirikisha Jumla ya timu Sita za vijana chini ya umri wa miaka 13, lengo kubwa ikiwa ni kumuenzi muasisi wa Taifa hili Hayati Mwl, Julius K. Nyerere.

Akizitaja timu shiriki katika ligi hiyo, mratibu wa maadhimisho hayo Bertha Ismail alisema kuwa ni pamoja na Nyota Accademy, Future Star, Kijenge Youth zingine ni Rolling stone, Young Life na Pallot.

“Maadhimisho haya huwa yanafanyika Octoba 14 kila mwaka lakini kwa mwaka huu tunafanya mwezi Septemba ili maadhimisho haya yasiathiriwe na zoezi la Uchaguzi ambapo pamoja na kumuezi Muasisi wa Taifa letu lakini ligi hii pia inalenga kuhasisha wananchi wafanye uchaguzi kwa amani bila vurugu ili sekta ya utalii hapa nchini izidi kukua”

“Katika maadhimisho haya yatakayofunguliwa na mkurugezi wa jiji la Arusha Iddi Juma yana “kauli mbiu ni Uchaguzi wa amani 2015: Taifa Moja kwa Maendeleo ya utalii” ambapo wadau mbali mbali wa maendeleo ya nchi yetu na utalii kwa ujumla watahudhuria ufunguzi na kilele ambayo ni septemba 19 na atakaefunga ni mkurugenzi wa hifadhi ya Taifa (TANAPA)  Allan Kijazi”

Bertha Alisema kuwa michuano hiyo ni utangulizi tu wa mashindano ya uandishi na uchoraji wa insha kwa wanafunzi 700 kutoka shule shule 25 za jiji la Arusha zitakazofanyika septemba 19 katika viwanja vya makumbusho jijini Arusha mashindano yaliyodhaminiwa na TANAPA, PALACE HOTEL, AICC, Bonite botllets, jiji la Arusha na TBL.
Mwisho…………..

0 comments:

Post a Comment