.

.
Monday, September 14, 2015

2:19 AM
mwandishi wetu -Arusha

TIMU ya Maafande wa JKT Oljoro ya jijini Arusha inayoshiriki ligi daraja la kwanza imeshindwa kuonyesha makali yake mbele ya wadogo zao  timu ya AFC Arusha inayoshiriki ligi daraja la pili baada ya kutoka suluhu ya bao 1-1 katika ufunguzi wa michuano ya Nyerere Cup 2015.

Mchezo huo uliofanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid, uliwashuhudia maafande hao wa Oljoro wakianza kucheka na nyavu za AFC baada ya kujipatitia bao lake kupitia kwa mchezaji Swalehe Idd alilofunga kwa njia ya Penalti mnamo dakika ya 58, iliyosababishwa na mabeki wa timu pinzani kunawa mpira katika eneo la hatari.

Vijana wa AFC walionyesha juhudi zao kwa kulishambulia lango la Oljoro ambapo walifanikiwa kusawazisha bao mnamo dakika ya 88 kupitia kwa mshambuliaji wao Wandima Malechela baada ya kuachia  shuti kali lililokwenda moja kwa moja vyavuni.
Ufunguzi huo ni utangulizi tu wa Mashindano ya vijana chini ya umri wa miaka 13 yaliyoandaliwa na kampuni ya BIMO Media yenye kauli mbiu "Uchaguzi wa Amani  2015, ndio taifa moja kwa maendeleo ya utalii nchini" na yatafikia kilele siku ya kilele tarehe 19 mwezi huu katika viwanja vya Makumbusho Arusha.

Akifungua mashindano hayo kwa niaba ya mkurugenzi wa jiji la Arusha Idd Juma,  Afisa Elimu jiji la Arusha kwa shule za sekondari Josephat Ntabindi alieleza kuwa mashindano hayo ni humimu hasa kwa watoto hao wenye vipaji kuonyesha uwezo wo huku wakikuza uelewa kwa vijana wadogo na kumuenzi hayati baba wa taifa Mwl Julias Nyerere ambaye pia alikuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha michezo hadi kugharamia kambi za timu ya Taifa kitendo ambacho kwa sasa hakipo.

Naye mkurugenzi wa kampuni ya mawasiliano ya Bimo Media Bertha Ismail alisema  maadhimisho hayo yataambatana na mashindano ya kila mwaka  ya ki- elimu  ya uandishi wa insha,makala pamoja na uchoraji  picha juu ya masuala ya utalii  kwa wanafunzi wa shule za msingi 25 zilizopo  Arusha.

“ Lengo ni  kuhamasisha uchaguzi wa mwaka huu  kufanyika kwa amani vile vile kuhamasiha watu  kuhudhuria hifadhi za utalii zilizoasisiwa na Mwl Nyerere na tunategemea Zaidi ya wanafunzi 700 watashiriki  katika shindano hilo la isha.”ismail alifafanua.

Timu za nyota academy,Future Stars,Kijenge Youth,Rolling Stone,Young Life na palloti zitachuana na washindi watakabidiwa zawadi mbalimbali ikiwemo vikombe na fedha.

Mwisho...................

0 comments:

Post a Comment