Waasi wa M23 ambao Rwanda inadaiwa kuwaunga mkono
Rwanda imetuhumu wanajeshi kutoka Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwa
kufanya uchokozi baada ya kundi moja kuvuka mpaka.
Hali iliyosababisha makabiliano katika eneo tete la mpakani kati ya nchi hizo mbili. .
AidhaMmoja
wa wanajeshi wa Congo alipigwa risasi wakati mmoja wa Rwanda
alijeruhiwa katika ufyatulianaji wa risasi. Tarrifa hii ni kwa mujibu
wa msemaji wa jeshi.
Msemaji wa jeshi la DRC alidokeza kuwa makabiliano yalikuja baada ya wanajeshi wa DRC kuvuka mpaka kununua vileo.
Rwanda
imekuwa ikikana kuhusika na vita vinavyoendelea Mashariki mwa DRC
lakini wafadhili kadhaa wamesitisha msaada kwa Rwanda baada ya Umoja wa
Mataifa kutoa madai kuwa wanawapa silaha waasi na kufadhili kundi la
M23.
Takriban watu 500,000, wametoroka makwao Mashariki mwa DRC tangu mwezi Aprili,wakati kundi la M23 lilipoanza mapigano.
0 comments:
Post a Comment