Imebainika kuwa mila na desturi hasa kwa jamii ya
kimasai bado ni changamoto kubwa
inayofanya kushuka kwa kiwango cha elimu wilayani Monduli mkoani Arusha
mratibu elimu kata ya Moita wilayani Monduli bwana Swati alipokuwa akisoma taarifa ya hali ya elimu katika kata hiyo tangu mwaka 2007 hadi 2012 mwaka huu |
Akifafanua kwa watoto wa kike alisema kuwa baadhi ya watoto
wa kike wakishafanyiwa tohara hujiona ni mtu mzima na kuona elimu haina maana kwake badala yake
huenda kuolewa kwa kufuata msukumo wa wazazi wake na kuacha shule.
Aidha kwa watoto wa
kiume wakishafanyiwa tohara hujiona ni watu wazima hivyo hudharau walimu hasa
wa kike na pia kutotaka kujichanganya na wengine wasiotahiriwa hali ambyo mazingira ya shule
humshinda na kuamua kuacha na kwenda kuchunga ngombe za wazazi wao kutokana na
shuleni hakuna sheria za kuwatenga waliotahiriwa na wasiotahiriwa.
Aliongeza kuwa hali hiyo pia huungwa mkono na wazazi wao
hali aambayo imekuwa usumbufu mkubwa kwa baadhi ya walimu pamoja na maafisa
elimu pindi wakiwafuatilia nyumbani kwao.
baadhi ya watu waliohudhuria kwenye kikao hicho wakiwemo wanahabari Deo Macha na Kessy Lukumai |
Kwa upande wake aliyekuwa mgeni rasmi katika kikao hicho,
mkuu wa wilaya ya Monduli, Jowika Kasunga aliwataka walimu wa shule za
sekondari na misingi zilizoko katika kata ya Moita kutokuwafanya wanafunzi
wanaowafundisha kama watumwa wa mapenzi badala yake wawafundishe na kuwachukua kama watoto wao.
Kasunga alisema kuwa baadhi wa walimu hasa wa kiume wamekuwa
na tabia ya kuwarubuni watoto wa kike na kujenga nao mahusiano ya kimapenzi huku
kwa baadhi ya walimu wa kike huhalalisha baadhi ya watoto kwenda kuolewa kwa
kuhongwa hela na waoaji hali ambayo hufanya mahudhirio ya watoto hao kuwa duni
na baadae kuacha shule.
Kasunga pia amewataka walim hao kuona matatizo ya wanafunzi
kama matatizo yao kwani kasoro mbalimbali zinazojitokeza kwa walimu ndizo
zinazowakumba na wanafunzi ikiwemo mwalimu kutimiza majukumu yake kwa zaidi ya
asilimia 50 ambapo wanafunzi nao humaliza shule wakiwa hawajui hata kusoma wala
kuandika na kwa baadhi ya watoto wa jamii ya kimasai baadhi humaliza hawajui
hata lugha ya Kiswahili wala kuandika jina lake.
Kutokana na mwenendo huo mkuu huyo aliwatahadharisha walimu
hao kuwa endapo fani ya ualimu inawashinda basi ni bora wakatafute shughuli
zingine za kufanya kama ujasiriamali, ubaamedi
au hata biashara nyingine kuliko kuendelea kudidimiza elimu katika kata hiyo la
sivyo watachukuliwa hatua kali za kisheria.
baadhi ya watu waliohudhuria kikao hicho |
0 comments:
Post a Comment