Mwenyekiti
wa Jukwaa la Katiba Tanzania Bw, Deus Kibamba (katikat)akizungumza na
waandishi wa habari leo ofisini kwake jijini Dar es salaam(hawapo
pichani) juu ya Uharakishaji wa Mchakato wa Katiba ambapo amesema kuwa
unaanza kuleta Fujo na kuathiri ushiriki wa Wananchi katika uundaji wa
Katiba mpya. Bw, Kibamba amesema kuwa, kuna makundi maalumu
ambayo yananyimwa haki ya kushiriki katika kutoa michango yao katika
mchakato wa Katiba Mpya, ambapo ametaja baadhi ya makundi hayo kuwa ni
Kundi la watu wenye ulemavu wasioweza kusikia na kuongea wanaoshindwa
kutoa maoni kwa kukosa wakalimani wa lugha ya Alama, ambapo amesema kuwa
hata matangazo yaliyotolewa kupitia Redio na Televisheni yameshindwa
kuwafikia watu wenye Ugumu wa Kusikia.
Jukwaa la Katiba limependekeza kuwa Matangazo yote ya Kwenye
Luninga yapatiwe wakalimani/ wafasili wa lugha ya Alama ili wasiosikia
pia waweze kufwatilia kupitia Runinga.
Kibamba amelitaja kundi lingine ambalo halijatendewa haki na
Tume ya Katiba kuwa ni Watanzania walioko Magerezani wakiwa kama
wafungwa au mahabusu.
“Kundi hili limenyimwa haki
kwa Miaka Mingi sana, Jukwaa la Katiba tuliwafikiria mapema, na tulitaka
tupate Ruhusa ya Magereza ili tukakusanye Maoni yao lakini tuliahidiwa
kuwa Tume itakusanya maoni yao ila mpaka sasa Tume imemaliza mchakato wa
Kukusanya Maoni pasipo kukusanya maoni ya Wafungwa”, amesema Kibamba
Jukwaa la Katiba limezidi
kusisitiza kuwa hawana imani kwamba Mchakato wa Katiba utakamilika
ifikapo 26 Aprili 2014 kutokana na Mapungufu yaliyopo.(kulia)mratibu wa
jukwa la katiba Bi.Diana Kidala.(kushoto)Bw.Israel Ilunde,
Baadhi
ya waandishi wa habari walioudhuria katika mkutano huo leo jijini Dar
es salaam wakifuatilia taarifa hiyo kutoka kwa Bw. Deus Kibamba.
0 comments:
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.