Rais Jakaya Kikwete.
Walisema alipokabidhiwa uongozi aliapa kuilinda na kuitetea katiba
ya Tanzania pamoja na kuhakikisha ustawi wa raia na rasilimali za
taifa.
Walitoa maoni hayo walipozungumza na NIPASHE kuhusu kauli yake
Jijini London wakati wa mkutano ya wanyamapori na kwenye mahojiano
maalumu na televisheni ya CNN ya Marekani na Shirika la Utangazaji la
Uingereza, BBC.
Mwenyekiti mstaafu wa Chama cha Wafanyabiashara, Wenye Viwanda na
Wakulima (TTCCIA) mkoa wa Kilimanjaro, Patrice Boysafi, akizungumzia
maelezo ya Rais alisema :
“Yeye ni mlinzi mkuu wa katiba, watu na rasilimali za nchi hii
yakiwamo meno ya tembo, alitakiwa aamuru mapapa wa ujangili wakamatwe
na kufikishwa mahakamani”.
Alisema Rais yuko juu ya mamlaka yote ndiye Amiri Jeshi Mkuu wa
Majeshi ya Ulinzi na Usalama, hivyo hana na sababu ya kumuogopa mtu
anatakiwa ataje watuhumiwa hao wanaofahamika kuwa ni waharibifu wa mali
za umma.
“Ni kiongozi mkuu ana mamlaka nikisikia amesema anawajua mapapa wa
ujangili tulitegemea atoe amri ya kuwakamata na kuwashitaki maana
ndiye Amiri Jeshi Mkuu, hana cha kuficha wala kuhofia,” alisema Boysafi.
Alihoji kama wanafahamika kwa nini hadi sasa mtandao haujavunjwa? Ni nini kinakwamisha kama wanafahamika?
Boysafi alisisitiza kuwa kuwa wanajulikana, idadi yao pamoja na
viongozi wao, hivyo Rais alitakiwa kutoa maagizo kwenye vyombo vya dola
ili washughulikiwe siyo katika televisheni wala redio za kigeni au
kwenye majukwaa ya jumuiya ya kimataifa.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa TTCIA Arusha Adolf Ulomi, alisema
wanatarajia kuona hatua zikichukuliwa baada ya Rais kueleza kuwa
wafanyabiashara hiyo wanafahamika.
Alisema kwa kuwa watuhumiwa wanajulikana na kiongozi wao yuko
Arusha, wanategemea kuona polisi na vyombo vya dola vikichukua hatua ya
kuwakamata , kushtakiwa, kuvunja mtandao na kukomesha ujangili.
Kwa mujibu wa Ulomi, kama jambo linafahamika ni wazi wana usalama
wako porini wanawatafuta majangili hao na wanachotaka ni wakamatwe na
washtakiwe.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCIA Mkoa wa Kilimanjaro, Boniface Maliki,
akizungumzia kadhia hiyo ya ujangili alisema, Rais alitoa taarifa hizo
baada ya gazeti la Daily Mail la London kuripoti ujangili, lakini
hakuwahi kuzizungumza humu nchini.
Alisema inaelezwa kuwa vigogo wa biashara hiyo wako Arusha lakini
habari zinafahamika baada Daily Mail kuishambulia Tanzania… kwanini
taarifa hazikuwahi kutolewa kabla? Na kuuliza mbona maelezo
hayakupatikana akiwa nchini?
Alisema wafanyabiashara wanataka kuona ushahidi wa mambo
yaliyozungumzwa London ukibainisha watuhumiwa na hatua zikichukuliwa
dhidi ya majangili waliochafua sifa ya taifa.
Kuhusu kuomba msaada jumuiya ya kimataifa, walisema si jambo baya
lakini kwa vile walilenga kupata vifaa vya kisasa na vyenye teknolojia
ni jambo jema.
Kwa upande wa utendaji, alisema hakuna haja ya kuomba msaada nje
kwa kuwa wapo watendaji wanaoweza kukamilisha operesheni za ulinzi wa
wanyamapori kinachotakiwa ni utashi wa kisiasa.
Wafanyabiashara wengine walimpongeza Rais Jakaya Kikwete, kwa
kugundua mtandao wa majangili 40, wakiongozwa na kinara aliyeko mkoani
Arusha na kushauri akamatwe bila kujali.
Diwani wa Kata ya Mererani, Justiny Nyari , ambaye pia ni
mfanyabiashara wa madini, alimpongeza Rais kwa jitihada za kufuatilia na
kugundua mtandao huo.
Alisema Rais anastahili pongezi kwa sababu bila kufuatilia huwezi
kugundua mtandao huo na kueleza kuwa maelezo hayo ni kweli kwa vile ni
Rais Kikwete ana mamlaka makubwa ya nchi.
Mfanyabiashara mwingine Aisha Juma, anayemiliki duka la nguo na
viatu jijini Arusha, alisema kauli ya Rais ni nzito hivyo kinachotakiwa
ni mtuhumiwa awe amejulikana , kukamatwa na kuchukuliwa hatua.
Alimpongeza Rais kwa kugundua mtandao huo na kutaka mtuhumiwa namba
moja akamatwe na ajulikane ili umma umtambue na sio kuzungumza na
kuacha suala hilo kuishia hewani. CHANZO:
NIPASHE JUMAPILI
0 comments:
Post a Comment