.

.
Wednesday, July 16, 2014

Wanafunzi wa shule ya awali wakiteta point za makundi yao kwa kubeba limao kwenye kijiko. huku mmoja wao akiwa nyuma akiokota baada ya kudondosha.

Shule za sekondary wakitetea point kwa mchezo wa riadha.

mchezo wa kuruka kwa gunia

kujaza maji kwenye chupa
kuvuta kamba kwa wazazi na walimu ambapo wazazi walishinda


mkuu wa shule ambae ni muandaaji wa siku ya michezo hiyo

kila mmoja alipokea zawadi kulingana na point zake
meneja mauzo wa pepsi Ally alipokuwa akigawa zawadi kwa vikundi

wanafunzi wa shule za awali nao walipata zawadi


Na Bertha Ismail.

Katika hali ya kukuza michezo mashuleni na kuinua vipaji vya wanafunzi shule ya Arusha Modern imeendesha mashindano maalum kwa wanafunzi wa shule hiyo kwa upande wa msingi na sekondari ikiwa ni kuadhimisha siku ya michezo shuleni.

Katika mashindano hayo yalihusisha makundi mbali mbali kutoka shule ya msingi na sekondari ya Arusha modern, ambapo kila kundi lilishiriki michezo mbalimbali ikiwemo Mpira wa miguu, mpira wa mikono, mpira  wa pete, riadha, kukimbia kwenye magunia huku wazazi na walimu kushindana kuvuta kamba.

Kwa upande wa wanafunzi wa shule za awali wakishindana kujaza maji kwenye chupa ya mililita 250, kupasua mapulizo sambamba na mashindano ya kuzunguka viti ambapo kila kundi  kupatiwa point za maksi walizopata.

Mashindano hayo yalihusisha kundi la Mandela team, Babro team, Nyerere team pamoja na Einstean team ambapo kundi la Mandela lilifanikiwa kuzibwaga makundi pinzani 3 kwa kunyakua point 173 ikifuatiwa na Babro ikinyakua point 171 huku akijipatia point 135 na kundi la Eistean ikijifuta machozi kwa point 110.

Akizungumzia mashindano hayo, mkuu wa shule ya Msingi Arusha Modern Philip Wasike alisema kuwa siku hii wameamua kuiadhimisha kwa mashindano hayo kutokana na kutambua umuhimu wa michezo hasa kwa mwanafunzi anaetumia muda mwingi kusoma hivyo ni lazima apate pia muda wa kupumzisha akili ili aweze kuelewa na kufaulu yale anayoyasoma.

Maadhimisho hayo yaliyokuwa na kauli mbiu “michezo ni ajira” Wasike Alisema kuwa mbali na hilo mashindano hayo wanakuwa wanaangalia vipaji vya wanafunzi wao ili kuweza kuunda timu za kichezo mbalimbali na kuzishindanisha na timu za michezo hiyo kutoka katika shule zingine za hapa jijini Arusha na mikoa mingine kwa ujumla.

“Kikubwa tunachokifanya hapa ni kuangalia vipaji vya wanafunzi wetu ili kuunda timu za mashindano na shule zingine ambapo tumeshapata baadhi ya majina ya wanafunzi wanaofaa katika michezo mbalimbali hivyo tunachokifanya sasa ni kupeleka barua za maombi katika shule zingine tuwe na mashindano ya hapa na pale angalau mara moja kwa wiki au mwezi” Alisema wasike.

Kwa upande wa wadhamini wakuu wa mashindano hayo, Ally Ramoudh kupitia kampuni ya Pepsi alisema kuwa kutokana na mvuto wa mashindano hayo na msisimko wake kwa wanafunzi na kuvuta umati mkubwa wa wakazi wa eneo hilo kampuni ya Pepsi itaendelea kudhamini siku hiyo ya michezo ili kufanikisha kukuza vipaji vya wanafunzi hao na kufananishwa na wachezaji maarufu kitaifa na kimataifa kwani shuleni ndio sehem ya nzuri ya kuonyesha kipaji na kukuzwa kwa urahisi.

0 comments:

Post a Comment