.

.
Friday, August 15, 2014


Mashindano ya vilabu bingwa Afrika Mashariki na Kati maarufu kama kombe la Kagame yanaendelea mjini Kigali.

Timu ya Azam Fc ya Tanzania ni moto wa kuotea mbali hasa baada ya kuweka nguvu zake kubwa katika kuhakikisha anabaki juu baada ya jana kukataa kufungwa na kutoka sare ya kufungana magoli 2 na Atlabara ya Sudan Kusini katika katika mashindano ya kombe la Kagame .
Mechi ilichezwa katika uwanja wa Nyamirambo jijini Kigali.
Azam wameongoza mchezo na kumaliza kipindi cha kwanza wakiwa mbele kwa goli 1 lililotiwa kimiani na mshambuliaji Borou kunako dakika ya 44.
Goli hilo lilikombolewa na mshambuliaji Thomas kunako dakika ya 48 kabla ya Martin Bonny kufunga goli la pili la Atlabara kunako dakika ya 54
Azam imesubiri dakika ya 85 kumuona mshambuliaji wake Kavumbagu akirudishia matumaini ya angalau kupata alama moja.
AZAM inaongoza kundi la A ikiwa na alama 5 ikifwatiwa na Rayon Sport ya Rwanda yenye alama 4.
Mechi iliyotangulia imeshuhudia sare ya goli moja kati ya timu ya Adama City ya Ethiopia na KMKM ya Zanzibar.
Goli hilo lilifungwa kimiani na mshambuliaji Wendesoni Mishido kunako dakika ya 60 ya mchezo.
Matumaini ya Adam City kusonga mbele yakazimwa na Juma Faki aliyekomboa goli hilo kunako dakika ya mwisho.
Kesho pia zitachezwa mechi mbili KCCA ya Uganda itamenyana na Atletico ya Burundi huku APR ya Rwanda ikizipiga na Telecom ya Djibuti.
Police FC ya Rwanda ndiyo timu pekee iliyokwisha jihakikishia tiketi ya kufuzu katika robo fainali hata kabla ya mechi za mchujo kumalizika.

0 comments:

Post a Comment