.

.
Friday, April 24, 2015

12:55 AM
Bertha Ismail – Arusha

Kamati huru ya uchaguzi wa uongozi mpya wa chama cha soka wilaya ya Arusha,  imefunga Rasmi pazia la uchukuaji fom wa kugombea nafasi mbali mbali katika chama hicho.



Zoezi la uchukuaji fom wa kugombea uongozi wa ADFA, ulianza rasmi April 15 na kufungwa mapema jana april 20 ambapo wadau wengi wa soka wameonekana kuogopa nafasi hizo zilizoachwa wazi na kupelekea idadi ndogo ya wagombea huku nafasi zingine zikikosa wagombea.



Awali wadau wengi jijini Arusha walionekana kutolea macho viti hivyo kabla tarehe ya uchaguzi kuanza lakini baada ya tarehe ya uchaguzi kutangazwa wengi wameonekana kukaa nyuma kutazama wachuaji fom bila kujishughulisha.



Akizungumza na gazeti hili, katibu wa kamati huru ya uchaguzi, Hussein Lembarity alisema kuwa nafasi zilizo wazi ni nafasi 10 ambazo kila mmoja ingefaa kuwa na wagombea watatu hadi watano lakini ambao ni zaidi ya watu 30 lakini anashangazwa na watu waliojitokeza ni watu 10 tu huku baadhi ya nafasi zikigombewa na mtu mmoja au wawili na zingine zikikosa kabisa wagombea.



“Mwanzo tulipochgauliwa tu watu wengi sana walijitokeza kuponda uongozi uliopo na kuahidi kuchukua fom za kupindua uongozi huu lakini baada ya kuanza kutoa fom watu wanachenga hali iliyopelekea nafasi zingine kukosa wagombea huku zingine zikiwa na mashaka ya kupita ila kwa sababu tumefunga pazia hilo hatuna budi kukubali matokeo na sasa ni nafasi ya kuweka pingamizi hadi april 24 kwa gharama ya 50,000”



Akitaja majina ya wagombea hao alisema kuwa nafasi ya mwenyekiti imegombewa na mtu mmoja ambae ni Omary Walii, makamu mwenyekiti mgombea mmoja Elisha Sironga huku nafasi ya katibu mkuu Zakayo Mjema akitetea nafasi yake na mpinzani ni Abdul Kondo na katibu msaidizi mgombea ni Athumani Juma na mweka hazina mmoja, Omary Kondo.



Kwa upande wa wajumbe wa mkutano mkuu wagombea ni Mwalizo Nassoro na Ayub Juma Kilabula huku nafasi ya uwakilishi wa vilabu akigombea mtu mmoja, Robert Munisi.





“Hao ndio wagombea na tumebandika majina hayo ukutani mwa uwanjan wa Sheik Amri Abeid kwa ajili ya watu kuleta pingamizi za wagombea hawa kama hawajatimiza sifa ya kugombea uongozi wa soka wilaya ikiwemo kuwa mkazi wa hapa jijini, elimu ya kidato cha nne, au kama hana uzoefu wa mpira wala taaluma ama aliwahi kuhukumiwa kwa kosa lolote”.



Uchaguzi huo wa ADFA unatarajiwa kufanyika mapema may 2 mwaka huu katika ukumbi wa viwanja vya Sheik Amri Abeid huku wajumbe na vilanu vyote vikitakiwa kulipa ada au kusajiliwa ili kuwa wajumbe halali wa mkutano huo na kupata kiongozi watakaempenda na kumwamini.





Mwishoo………………………

0 comments:

Post a Comment