.

.
Wednesday, May 6, 2015

2:02 AM



Bertha Ismail - Arusha

Chama cha soka wilaya ya Mbulu, Kimeipongeza shirikisho la Soka nchini kwa kutambua umuhimu wa wilaya hiyo kimichezo na kuwapa nafasi ya kuwa moja ya vituo vitatu vya michuano ya ligi ya mabingwa wa mikoa Tanzania inayotarajia kutimua vumbi may 2 mwaka huu.

Michuano hiyo ya RLC itashirikisha jumla ya timu 27 nchini katika vituo vitatu vya Mbulu (Manyara) , lindi na Sumbawanga ambapo kila kituo inatarajiwa kuwa na timu tisa ambapo kwa Mbulu kutakuwa na timu ya Madini (Arusha), alliance school (Mwanza), Bariadi united (Simiyu) zingine ni  Baruti (Mara), Lukirini fc (Geita), Mtwivila City (Iribga), RAS Kagera fc (Kagera) pamoja na Small Prison (Tanga) na Watumishi fc (Shinyanga).

Ugeni huo mkubwa umewapa motisha kubwa wakazi na viongozi wa soka wilaya ya Mbulu na kufurahia nafasi hiyo adimu huku wakitoa shukrani zao za dhati kwa shirikisho la soka Tanzania kwa kutambua mchango wao huku wakisema kutumia michuano hiyo kama mafunzo kwao.

“Kiukweli tumefurahi sana TFF kutuletea michuano hii kwani itakuwa kama fursa kwetu ya kujifunza nini wenzetu wanafanyaga na tujifunze kwa kuiga ili na sisi tusonge mbele kisoka kwani imekuwa ikituuma sana zaidi ya miaka 10 hatujaonja ligi kuu na miaka mitano hatujui ligi daraja la kwanza likoje” alisema katibu wa soka wilaya ya Mbulu Fortunatus Kalewa.

“Tunashukuru timu nyingi zimeshaweka oda ya sehemu za malazi na viwanja vya mazoezi ikiwemo timu ya madini fc ya Arusha hivyo naamini itakuwa fursa kwetu kuwaleta wachezaji wa timu mbali mbali za mkoani hapa kuja kuiba mbinu wanazotumia wenzetu katika mashindano hadi wanasonga mbele na kuwakilisha mikoa yao katika ligi za ngazi za juu”

Kituo hicho cha Mbulu mashindano ya ligi ya mabingwa wa mikoa inatarajiwa kuanza kutimua vumbi may 9 katika viwanja vya Nyerere wilayani mbulu mkoani Manyara ambao uko katika hali nzuri kimandhari na uzio ingawa majukwaa bado ni changamoto.

Mwisho………………….

0 comments:

Post a Comment