.

.
Wednesday, May 6, 2015

2:05 AM
Bertha Ismail  - Hanang’

Mwanariadha Emmanuel Giniki amezidi kung’ara katika mbio mbali mbali za hapa nchini, baada ya mwishoni mwa wiki hii kung’ara tena katika mbio za may day kwa kukata upepo wa km 21 kwa kutumia saa 1: 01:17 na kuwaacha wenzake zaidi ya 70.

Mbio hizo zilizofanyikia Katesh makao makuu ya wilayani hanang’ kwa ajili ya kuadhimisha sikukuu ya wafanyakazi, Giniki alifanikiwa kuwa wa kwanza kumaliza mbio hizo akifuatiwa na Msandiku Mohamed aliyemaliza kwa saa 1:03:18 na aliyeshika nafasi ya tatu ni Stephano Huche 1:03:21.

Kwa Upande wa wasichana Anjelina Tsere alifanikiwa kutwaa ushindi baada ya kumaliza mbio hizo za km 21 kwa kutumia saa 1 :16: 43 akifuatiwa kwa karibu na Rozalia Fabiano kwa kutumia saa 1:21;15 na Amina Mohamed akishika nafasi ya tatu kwa kutumia saa 1:21:43.

Mgeni rasmi katika mbio hizo ni aliyekuwa waziri mkuu zamani Fredrick Sumaye ambapo mbali na kupongeza uongozi wa riadha manyara na waandaji aliwataka kuendeleza mashindano ya mara kwa mar ili kuwaweka wanariadha katika hali ya kufanya mazoezi ya mara kwa mara na kufanikiwa kushinda mbio za kimataifa hatimaye kurudisha heshima ya mkoa huo katika historia riadha.

Kwa upande wa waandaji , Alfredo Shahanga alisema kuwa kwa sasa wameamua kuendesha mashindano ya mara kwa mara ya mchezo huo ili kuwaweka wachezaji sawa kupambana katika michuano ya kimataifa iliyoko mbele yao ikiwemo ya All afrika game hivyo waweze kujitathimini mapema.

Mwisho……………….

0 comments:

Post a Comment